TANZIA Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

TANZIA Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

Mwenyezi Mungu ampe pumziko la Amani. Huwezi kuandika simulizi la siasa za Tanzania na changamoto za utawala wake bila kuweka mchango na nafasi ya Lowassa katika chama tawala na katika upinzani. Nawaombea faraja familia, ndugu na Jamaal kufuatia msiba huu. Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa Amani, Amina.
 
So sad,mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani,ni njia ya wanadamu wote.Nichukue nafsi hii binafsi kuipa pole familia ya mh Lowasa,ndugu jamaa na marafiki.
 
Kwani komredi alikuwa bado Chadema hadi kufariki kwake?

Mie Nijuavyo alirudi nyumbani baada ya nyumbani kunoga, so viongozi wa CDM huu msiba hauwahusu.
Tupo kwenye maridhiano huu msiba unawahusu sana chadema hasa ikizingatiwa marehemu aliwahi kusajiliwa kwa mkopo mwaka 2015 kabla kurejea lumumba FC .
 
Waziri Mkuu Mjiuzuru?
Unat
Huyo waziri mkuu hakustaafu, Bali alijiuzulu kwa kashfa, Sasa bendera inapepea nusu mlingoti kwa kipi? Au ni kisiasa zaidi?
Ndio maana siku zote napingana na wanaCHADEMA Kwa sababu hawatumii akili kwenye hoja zao na hii comment ni mfano tosha wa akili za CHADEMA.

Nakupa ufafanuzi hapa ili utambue Kwa nini tunasema aliyestaafu na sio aliyejiuzulu na kama utaendelea kuwa mbishi wa kutokuelewa nitakushangaa.

Kwanza, katiba haijatoa muda wa kikatiba wa mtu aliyechaguliwa kama Waziri mkuu tofauti na Urais hivyo kipindi cha muda wowote atakaohudumu Waziri mkuu atakuwa kastaafu. Je, Waziri mkuu anatakiwa kustaafu baada ya muda gani?

Pili, Kuna mstari mwembamba sana unaotafautisha kujiuzulu na kustaafu na kujiuzulu Kwa lugha nyepesi ni kustaafu mapema. Tuachane na sababu iliyofanya Lowassa kujiuzulu tuje kwenye kujenga picha kubwa zaidi hivi Lowassa angeomba kujiuzulu Kwa sababu ya ugonjwa kutokana na umri mkubwa ,je Bado ungesema aliyejiuzulu au aliyestaafu?

Tatu, kitafsiri kustaafu ni neno linalotumika kuashiria ukomo wa mtu kwenye nafasi yake na Lowassa alikoma kwenye nafasi hiyo ndani ya kipindi na Kwa kuwa katiba haikueleza Waziri mkuu anatakiwa kukaa muda gani kisheria basi inatosha kusema alistaafu.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Apumzike Kwa Aman
 
Mwenyezi Mungu ampe pumziko la Amani. Huwezi kuandika simulizi la siasa za Tanzania na changamoto za utawala wake bila kuweka mchango na nafasi ya Lowassa katika chama tawala na katika upinzani. Nawaombea faraja familia, ndugu na Jamaal kufuatia msiba huu. Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa Amani, Amina.
Aamin mzee mwanakijiji .
 
Ina maana kwa wale wagombea wa urais wa 2015 wenye ushawishi kwa namna yeyote tungefiwa na rais madarakani.
Nacheki kwenye orodha hapa;
1. Magufuli John
2. Membe Benard
3. Sitta Samwel
4. Mahiga Augustino
5. Ramadhani Augustino
6. Lowasa Edward

Watanzania Ilikuwa haiepukiki kupitia impossible moment ya kufiwa na rais madarakani ingawa wao kwa wao walikuwa wanatabiriana mabaya.
Pascal Mayalla
Yeah! Inafikirisha sana....huenda hili lisingeepukika.

Anyway yote ni maisha tu.
 
Ila inasemekana ni tajiri sana ni bilionea sasa kapata wapi mali yote hiyo na kazi yake alikua mtumishi wa umma? Alikua anafanya biashara gani huko serikalini?
Huyo katoka kwenye familia ya kitajiri tangu akiwa mtoto na biashara amefanya sana tu, si aina ya watu ambao walihitaji kujitafuta sana ili watoboe kama ilivyo kwa makupuku wengi hapa Tz.

Ni kama ilivyo kwa Mbowe tu.

Mtu wa pekee ambaye utakuwa sahihi kushangaa utitiri wa mali alizojilimbikizia ni JK kwasababu hata historia ya familia yake inakataa.
 
Mungu akulaze mahala pema peponi Mzee wangu Edward Ngoyayi Lowassa, Byee byee Baba Lowassa.

Mwaka 2015 nilikuwa supporter wako mkubwa sana, hakika nilikufuata toka CCM na kukupigia kampeni mitandaoni na majukwaani upate kura kwani niliamini ulikosa haki yako CCM wakati ule, ingawa wengi tulikuwa CCM ila ulipata kura zetu 2015, CCM wengi tuliumia sana, yote sasa ni historia, nilikupenda kama mwanasiasa shupavu katika CCM na nje ya CCM, busara zako zilikuwa za hali ya juu sana, ni mwanasiasa uliyejua kudhibiti sana ulimi wako, umeondoka Lowassa ila moyoni mwangu uko hai daima sitakusahau asilani, ulijaa wema sana na mchapakazi wa kweli.

Mungu akulinde daima na milele yote, Amen


View: https://youtu.be/8nibWz0XLlw?si=bx_vXZzJwZDEUXZl



View: https://youtu.be/RgKAFK5djSk?si=MCxe6lhOMuM56eM5
 
R.I.P Umepigania sana uhai wako lakini hamna namna nyakati zimekwenda na ashukuriwe aliye juu Kwa zawadi ya maisha.
 

EDWARD NGOYAI LOWASSA AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kugombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mtoto wake Fredrick Lowassa amethibitisha na Makamu wa Rais, Philip Mpango amelitangazia Taifa.

Pia, Lowassa aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2008 na kuweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza kujiuzulu.

WASIFU WA EDWARD NGOYAI LOWASSA
Edward Ngoyai Lowassa anatoka katika jamii ya Wafugaji Kaskazini mwa Tanzania. Alizaliwa August 26 mwaka 1953 katika Kijijini cha Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha. Edward Lowasa ni mtoto wa tatu wa Mzee Ngoyayi.

Kitaaluma Lowasa ni msomi , akiwa na shahada kwanza kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam na shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Bath huko Uingereza (1983-1984).

Uzoefu katika siasa
Ingawa baba yake alikuwa mfugaji aliwahi pia kufanya kazi kama tarishi katika serikali ya wakoloni.

Alijiunga na chama cha CCM mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka wa 1977.

Kabla ya kugombea Ubunge , aliwahi kutumikia Jeshi la Tanzania na hata kupigana katika vita kati ya Tanzania na Uganda vilivyopelekea Idd Amin kuondolewa madarakani.

Baada ya hapo alikuwa Mtumishi wa Umma kwa miaka kadhaa kabla kuteuliwa kuwa Mbunge kuwajilisha Vijana na kujiunga rasmi na siasa.

Mwaka wa 1990 alijitosa ulingoni kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la uchaguzi la Monduli.

Alifanyikiwa kwa miaka yote hii Lowassa ameendelea kulishikilia jimbo hilo la uchaguzi hadi alipolazimika kuliachia ili kuwania Urais.

Mwaka 2015 alipowania Urais haikuwa mara yake ya kwanza kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani mwaka 1995, alikuwa miongoni mwa watangaza nia 15, hata hivyo nafasi ikachukuliwa na Benjamin William Mkapa.

Hata hivyo tofauti na matarajio ya wafuasi wake, Mwaka 2005, Lowassa hakuwania nafasi hiyo, badala yake aliunga mkono rais anayemaliza muda wake Jakaya Kikwete.

Je Lowassa amewahi kuwa nani katika nyadhifa alizozipitia Kiserikali?
Edward Ngoyayi Lowassa amewahi, kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Ardhi na Maendeleo ya Makazi pamoja na nafasi nyinginezo.

Lakini pia nafasi za juu alizowahi kuzipata ni pamoja na kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka Febuari 7 mwaka 2008, alipolazimika kujiuzulu baada ya madai ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa ya Kampuni ya Richmond, Madai ambayo bwana Lowassa aliyakanusha hadi sasa.

Katika siasa, Lowassa anafahamika kama mtu wenye misimamo mikali,kwa kile anachokiamini mwenyewe kama siasa zinazo ambatana na maamuzi magumu.

Licha ya kuwa mwanachama wa CCM kwa miaka 38, bwana Lowassa aliwashangaza wanachama wa CCM kwa uamuzi wake wa kukihama chama hicho. Hatua iliyochangiwa na yeye kutoridhrishwa na jinsi uteuzi wa wagombea urais wa kilichokuwa chama chake ulivyoendeshwa.

Alijiunga na chama cha kikuu cha upinzani cha CHADEMA. Kilichukuwa mojawapo ya vyama vinne vya upinzani vinavyounda umoja uitwao, UKAWA katika Uchaguzi wa mwaka 2015

Kufuatia uamuzi wake wa kubadili chama, Edward Lowasa amelazimika pia kubadili msimamo wake wa kisiasa na kuwa mpinzani wa chama tawala na sera aliziunga mkono na kuzitumikia awali, jambo ambalo linawatatanisha wakosoaji wake .

Hii ilikuwa mara yake ya pili kujaribu kuingia ikulu.

===========​


EDWARD NGOYAI LOWASSA HAS PASSED AWAY

Former Prime Minister of Tanzania and presidential candidate for CHADEMA in 2015, Edward Ngoyai Lowassa has passed away after a long illness. His son Fred Lowassa has confirmed.
Lowassa served as the Prime Minister of Tanzania from 2005 to 2008 and set a record as the first Prime Minister to resign voluntarily.

Profile of Edward Ngoyai Lowassa:
Edward Ngoyai Lowassa was born on August 26, 1953, in the village of Ngarashi, Monduli District, Arusha region, Tanzania. He was the third child of Mr. Ngoyayi.

Educational Background:
Lowassa was an educated individual, holding a bachelor's degree from the University of Dar es Salaam and a master's degree from the University of Bath in the UK (1983-1984).

Political Experience:
Lowassa joined the ruling party CCM immediately after completing his university education in 1977. He served in the Tanzanian military and participated in the war between Tanzania and Uganda that led to the removal of Idi Amin from power.

He later became a public servant before being appointed as a Member of Parliament representing youth and officially entering politics. He successfully contested for the Monduli constituency seat and held it until he resigned to run for the presidency.

In 2015, he ran for the presidency under CHADEMA, which was not his first attempt at the presidency. He had previously contested in 1995 but was not successful.
Lowassa held various government positions, including Minister of Water and Livestock Development, Minister of Lands and Human Settlement Development, and others. He served as the Prime Minister of Tanzania from 2005 to February 7, 2008, when he resigned amid corruption allegations related to the Richmond scandal, which he denied.
Known for his strong political stance and decision-making, Lowassa surprised many by leaving CCM due to dissatisfaction with the party's candidate selection process. He joined the opposition party CHADEMA and was part of the coalition UKAWA in the 2015 elections.

His switch in allegiance raised questions about his political principles and loyalty. This was his second attempt at the presidency.

Rest in peace, Edward Lowassa.​

Kufuatia Msiba huu mzito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 5 za maombolezo kuanzia leo tarehe 10 Februari ambapo bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa heshima ya marehemu.
Pole sana kwa mkewe kipindi chote hicho cha kupumua kwa mashine hakukata tamaa, Joseph haule alirejea EL yeye imeshindikana kazi yake Mola
 
Back
Top Bottom