Tatizo kubwa la baadhi ya watu ni kufikiria kuwa watu wengine ni miungu watu na wanafaa kuabudiwa tu bila kukosolewa pamoja na makosa mengi wanayoyafanya kama binadamu.
Hili halikubaliki kwani hakuna mwanadamu yeyote aliyeumbwa kufanya mema tu siku zote. Hivyo Tundu Lissu kama alimkosoa Nyerere, (Japo hakumtukana kama waongo wengine wanavyodai humu), ni sawa kabisa kwani Nyerere hakuwa Mungu bali alikuwa ni binadamu tu kama wengine na ndio maana hatunaye humu duniani leo hii.
Nyerere kama binadamu yeyote alikuwa na mapungufu yake na ndio maana hakuweza kuishi milele sasa leo wengine kutaka kumtumia kama mtaji feki wa kisiasa ni ujinga tu na ufinyu wa mawazo.
Mfano tu ni kuwa kuna makosa makubwa matatu ambayo aliyafanya na athari zake zimekataa kuondoka hadi leo na inaonekana itachukua muda mrefu sana kwa hizo athari kuondoka.
1. Alilazimisha sera yake ya Azimio la Arusha na matokeo yake kudumaza kabisa uchumi na kuua uwekezaji.
2. Alibuni siasa mbovu ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kumuiga dikteta Mao wa China na kupelekea kusondeka watu kwenye vijiji vya ujamaa kwa nguvu na kusababisha watu kupoteza mali na wengine kufariki dunia.
3. Alilazimisha vita na Uganda ili kumrejesha madarakani rafiki yake dikteta Milton Obote na matokeo yake kutia kitanzi uchumi wa nchi isipone hadi leo hii.
Hayo mapungufu yanatuonyesha vizuri kuwa Nyerere alikuwa ni mtu mwenye mapungufu tena sana tu na kuwa wasioweza kumkosoa ni wanafiki tu na wachumia tumbo kwani hakuwa Malaika.
Kwa sisi tunaoamini ktk ukuu wa Mungu kamwe hatutakubali ujinga au upumbavu wa mtu yeyote kuabudiwa kwani kufanya hivyo ni sawa na kuabudu sanamu na ni dhambi kubwa sana mbele za Mwenyezi Mungu.
You should not worship idols: Exodus 20:3; Leviticus 19:4; 26:1; Psalm 16:4; Isaiah 45:20; Jonah 2:8; Matthew 4:10; Luke 4:8; 1 John 5:21; Corinthians 10:14; Colossians 3:5; and Revelation 9:20 etc.
Wanadamu tumezidi sana kumchezea Mungu kwa kuwa hatumuoni kwa macho tunafikiri hayupo na badala yake watu tunaowaona kwa macho ndiyo tunafikiri ni yeye na tunathubutu eti kuwaabudu hadi viongozi wa kidini leo hii wanaabudu watu (Sanamu) tena mbele za waumini wao, very stupid. Tuache huu Upumbavu.