Edwin Mtei aliposikitishwa na Tundu Lissu kumtusi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Ndugu andiko hili la single mother sio zuri wapo watu wengi tu hawana maadili na wamelelewa na wazazi wao wote wawili. Kimsingi maadili ndio nguzo kubwa ya jamii yoyote.
Siyo maadili tu, hata historia ya nchi hi wengi hawaijui fika.
Marekani leo wale Founding Fathers wanahaeshimiwa sana.
Sisi tunafanya mzaha hata wnegine kama Tundu Lissu kudiriki kumtukana Mwalimu, halafu leo wanautaka urais!
Not to zis extenti!!
 
Siyo maadili tu, hata historia ya nchi hi wengi hawaijui fika.
Marekani leo wale Founding Fathers wanahaeshimiwa sana.
Sisi tunafanya mzaha hata wnegine kama Tundu Lissu kudiriki kumtukana Mwalimu, halafu leo wanautaka urais!
Not to zis extenti!!
Kumtusi na kumkashifu mtu kamwe hakuwezi kufanya mtu anae tusi kupanda juu nchi yoyote au jamii inajengwa kwa nidhamu kuheshimiana na kuvumilina pia na siku zote neno ni dogo kabla halijatoka mdomoni likesha toka kubwa hilo.
 
Where is the standard for rating? Compared to his successors, He must be overrated! Who else at his performance level.
 
Unazungumziaje kipengele cha ubunge/udiwani kupingika,uraisi kutokupingika(ambacho kiliwekwa wakati wake)?
Absolutely wrong! Vyama vingi kuanza Nyerere hakuwa madarakani. Naona tunaandika kwa hisia tu bila uhakika.
 
Ukisoma maneno yaliyowekwa kwamba yalisemwa na Mtei, anazungumzia kutukana. Hasemi kukosoa. Tundu alitukana na amekuwa na tabia ya kutukana akiamini ndo kukosoa. Ukisema pumbavu ni tusi siyo kukosoa.
 
Ona haka nako baada ya kusoma civics ya form four basi kanajiona kanajua sana,!

Dogo unapata jeuri ya kubwabwaja hapa na hako katecno kako sababu ya Nyerere!
 
Nyerere kafanya mazuri mengi, na ana makosa mengi tu.

Na alilalamika watu wanaangalia makosa yake, wanaacha kuangalia mazuri.

Hapo napingana naye, watu wanatakiwa waaangalie makosa ya viongozi. Bila kuangalia makosa ya viongozi hawawezi kuyarekebisha.

Mazuri hayahitaji kurekebishwa sana, hivyo hayatakiwi kupewa kipaumbele katika kuangaliwa.

Nyerere ninamuheshimu kwa mengi mazuri aliyofanya.

Lakini, nikisikia kuna mwanasiasa anamkosoa Nyerere, nashukuru kwamba kuna mtu ana uthubutu wa kumkosoa Nyerere.

Mtei hakueleza Tundu Lisssu alisema nini.

Sitaunga mkono kumtusi Nyerere. Nyerere alikuwa ni kati ya viongozi waliojiheshimu na kuheshimu watu sana, sana tu. Angeweza kuwa dikteta mkubwa lakini hakuamua kufanya hivyo.

Ukitaka kuelewa umuhimu wa Nyerere, na alivyojiheshimu, linganisha kauki za Nyerere na za Magufuli halafu uone tofauti. Kama rais Mwinyi alisema yeye ni kichuguu na Mwalimu Nyerere ni mlima Kilimanjaro, basi Magufuli ni punje moja ya mchanga!

Lakini, Nyerere katika siasa, alifanya makosa mengi tu. Hata yeye mwenyewe alikubali hilo.

Sasa kama Nyerere mwenyewe alikubali kwamba alifanya makosa (mfano alikubali utaifushaji wa mashamba makubwa ulikuwa na mapungufu makubwa, serikali iliyachukuwa bika ya kuwa na uwezo wa kuyaendesha).

Mtu kama huyo ambaye mwenyewe kakubali makosa, kwa nini wengine wasimseme makosa yake?
 
Mkuu kuna majambazi hapa wanalazimisha mtu awe perfect 100%. Kuwa rais wa kwanza kwenye nchi masikini ambayo haina misingi yoyote ni kazi ngumu.
Imagine mtu alikuwa na complete power na hakufanya wizi wala kutengeneza circle yake, hawaoni alichofanya Kenyatta Sr. Rais kaleta umoja, kaondoa uwezekano wa matabaka, ukabila na udini, mwishoni kaona uwezo wake umefika kikomo kaondoka mwenyewe huku wakimuomba abaki, kawapa uhuru kwa njia ya amani kabisa. Mtu kama Nyerere ni underrated kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla.
Sasa kuna watu walitaka afanye kila kitu as if yeye ni Mungu. Sasa kaondoka, benki na viwanda alivyoacha vingine vishauzwa na kufirisika. Katiba aliyoacha bado inatumika, hivi kuna rais anagusa lifestyle ya nchi kama Mwalimu? Kama alikosea mbona hawawezi kukosoa makosa yake miaka yote tangu aondoke.
 
Mkuu inaonekana haujui Lissu aliongea maneno gani hadi Mzee Mtei kujitokeza hadharani na kukemea na kutoa angalizo au muongozo.

Kama umemuelewa Mtei tatizo siyo kumkosoa Nyerere bali kumkashifu au kumtukana au kumdhalilisha au kumdhihaki.
Nyerere amekosolewa na wengi tu na bado atakosolewa, hiyo haijawahi kuwa dhambi au kosa. Tatizo unatumia lugha gani.

Kwenye kuchagua lugha ya kukosoa hapo Lissu amekosa karama hiyo, huwa anajisahau na kutumia lugha isiyo sahihi na isiyo na staha na kuheshimiana.
Mara nyingi hulipuka kwa mihemko hasa pale anapo ona wanaomshangilia na kumshabikia wapo wengi.
Ana mihemko flani na mizuka iliyopitiliza, pamoja na kuhisi yeye anajua au ana akili sana kuliko watu wote walio mzunguka.
 
Nakumbuka zilikuwa kashfa kubwa.

Kuna mtu ana rekodi ya maneno halisi aliyosema Tundu Lissu?
 
Nakumbuka zilikuwa kashfa kubwa.

Kuna mtu ana rekodi ya maneno halisi aliyosema Tundu Lissu?
Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya haramu na vya halali hakuviweza.
Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.
Mkuu inawezekana mimi mawazo yango yanaegemea upande mmoja (biased) lakini unafikiri kulikuwa na ulazima wa kutumia maneno makali kama "msanii wa kisiasa", "alizoea vya haramu vya halali hakuviweza" ?

Lazima upime mazingira ya mahali unapo ongelea na mtu unayemzungumzia au kumkosoa.

Kiukweli hoja za Lissu kuhusu Nyerere na muungano zilikuwa haki tu kuhoji au kumkosoa lakini hayo maneno ya mipasho aliyotumia kama ya kwenye taarabu au kijiweni dhidi ya mtu aliyekufa tena mtu mkubwa katika jamii inayo mheshimu sana.
 
Nyerere alibariki matokeo ya uchaguzi Zanzibar kuchakachuliwa mwaka 1985.

Idris Abdul Wakil alishindwa kupata kura za kutosha, akiwa mgombea pekee.

Matokeo ya kweli yalifika mpaka Daily News, yakionesha Wakil kashindwa.

Nyerere akaamuru serikali itoe matokeo tofauti yanayoonesha Wakil kashinda.

Tangu wakati huo CCM imekuwa ikiiba kura Zanzibar.

Kwa huo mfano mmoja tu, Nyerere alifanya udanganyifu.

Sipo upande wa Nyerere wala wa Tundu Lissu, wote wana mapungufu.

Nipo katika kutafuta ukweli.
 
Mtei who??
 
Namimi naafikiana na wewe kuhusu maoni yako au ya Lissu kuhusu Nyerere isipokuwa kwa mtazamo wangu naona lugha aliyotumia Lissu ndiyo tatizo.
Siku zote lugha tu anayotumia ndiyo humtia dosari, na hilo tatizo wanafanana sana na bwana mkubwa fulani anayemkosoa sana.

Kwa mfano aliyomkosoa Nyerere kuhusu muungano yana mashiko kabisa na tena aliweka na ushahidi wa kutetea hoja au tuhuma zake. Shida lugha isiyo ya staha.
Mimi na wenzangu humu JF au vijiweni tunaweza kutumia lugha hiyo bila shida ila siyo yeye kwa wadhifa wake na mahali pale. yeye ni muomba kura na alikuwa anaitwa Mheshimiwa Tundu Lisssu mbunge ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…