Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 25,874
- 36,030
Ok.. Nyerere ana makosa lakini si kwa ukali na lugha ile aliyotumia Lisu katika kumkosoa!Nyerere kafanya mazuri mengi, na ana makosa mengi tu.
Na alilalamika watu wanaangalia makosa yake, wanaacha kuangalia mazuri.
Hapo napingana naye, watu wanatakiwa waaangalie makosa ya viongozi. Bila kuangalia makosa ya viongozi hawawezi kuyarekebisha.
Mazuri hayahitaji kurekebishwa sana, hivyo hayatakiwi kupewa kipaumbele katika kuangaliwa.
Nyerere ninamuheshimu kwa mengi mazuri aliyofanya.
Lakini, nikisikia kuna mwanasiasa anamkosoa Nyerere, nashukuru kwamba kuna mtu ana uthubutu wa kumkosoa Nyerere.
Mtei hakueleza Tundu Lisssu alisema nini.
Sitaunga mkono kumtusi Nyerere. Nyerere alikuwa ni kati ya viongozi waliojiheshimu na kuheshimu watu sana, sana tu. Angeweza kuwa dikteta mkubwa lakini hakuamua kufanya hivyo.
Ukitaka kuelewa umuhimu wa Nyerere, na alivyojiheshimu, linganisha kauki za Nyerere na za Magufuli halafu uone tofauti. Kama rais Mwinyi alisema yeye ni kichuguu na Mwalimu Nyerere ni mlima Kilimanjaro, basi Magufuli ni punje moja ya mchanga!
Lakini, Nyerere katika siasa, alifanya makosa mengi tu. Hata yeye mwenyewe alikubali hilo.
Sasa kama Nyerere mwenyewe alikubali kwamba alifanya makosa (mfano alikubali utaifushaji wa mashamba makubwa ulikuwa na mapungufu makubwa, serikali iliyachukuwa bika ya kuwa na uwezo wa kuyaendesha).
Mtu kama huyo ambaye mwenyewe kakubali makosa, kwa nini wengine wasimseme makosa yake?
Yani kwa akili ya Lisu, alimuweka Nyerere kwenye kapu moja na kina Msukuma,
Kwangu mimi Lisu ni msomi anaetumia usomi wake kudanganya wapumbavu.
