Edwin Mtei aliposikitishwa na Tundu Lissu kumtusi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Edwin Mtei aliposikitishwa na Tundu Lissu kumtusi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Ndugu andiko hili la single mother sio zuri wapo watu wengi tu hawana maadili na wamelelewa na wazazi wao wote wawili. Kimsingi maadili ndio nguzo kubwa ya jamii yoyote.
Siyo maadili tu, hata historia ya nchi hi wengi hawaijui fika.
Marekani leo wale Founding Fathers wanahaeshimiwa sana.
Sisi tunafanya mzaha hata wnegine kama Tundu Lissu kudiriki kumtukana Mwalimu, halafu leo wanautaka urais!
Not to zis extenti!!
 
Kumtusi na kumkashifu mtu kamwe hakuwezi kufanya mtu anae tusi kupanda juu nchi yoyote au jamii inajengwa kwa nidhamu kuheshimiana na kuvumilina pia na siku zote neno ni dogo kabla halijatoka mdomoni likesha toka kubwa hilo.
 
Nyerere is overrated. Kwa umasikini huu wa kutupwa. Kuipeleka nchi vitani (akimpigania Obote arudi madarakani baada ya kupinduliwa Na IDD Amini). Nyerere alitengeneza kuogopeka na viongozi wa chini. Wakampamba .

Hint: katiba ya 1977

Udiwani,unapingika kortini
Ubunge,unapingika

Uraisi,hapana. Akitangazwa,imeisha hiyo.
Yeye alikuwa raisi. If you know you know
Where is the standard for rating? Compared to his successors, He must be overrated! Who else at his performance level.
 
Tusiishi katika ukomo wa kifikira kuendana na historia ya nchi yetu. Ndiyo! Mwl. Nyerere ni Muasisi na Baba wa Taifa letu, na alikuwa kiongozi mashuhuri kwa wakati wake, ambaye alilitetea sana utu wa watu nchini, barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.

Lakini hiyo siyo sababu ya kumfanya akose wakosoaji wa misimamo yake. Kama binadamu awaye yeyote yule, alikuwa na madhaifu yake. Na jambo hili linathibitika kupitia kauli yake mwenyewe kabla mauti hayamkuta. Alikuwa "remorseful" kwa baadhi ya maamuzi yake kama kiongozi, hasa kwa yale yaliyoleta matokeo hasi.

Kwa hiyo Tundu Lissu naye ni kiongozi mwenye sifa zake ktk taifa lake. Na pia mwenye maono yake ya kulipeleka taifa letu ktk "next frontier" kupitia mapungufu ya kihistoria ambayo anaamini kwa dhati yalitokana na Baba wa Taifa. Tuzipime "constructive criticisms" zake. Wala tusizibeze kwa kauli za jumla jumla tu.

Tuje na hoja mujarabu hapa jukwaani na kuainisha wapi amekosea. Sio hoja za juu za kutumiwa na mabeberu. Kama hizo "claims" ni za kweli, wakosoaji wa TL waainishe ni lini, wapi na kwa vipi anahusika.
Ukisoma maneno yaliyowekwa kwamba yalisemwa na Mtei, anazungumzia kutukana. Hasemi kukosoa. Tundu alitukana na amekuwa na tabia ya kutukana akiamini ndo kukosoa. Ukisema pumbavu ni tusi siyo kukosoa.
 
Huwezi mfananisha lissu na dictator Nyerere au Mtei , lissu sio zero brain kama Mbowe na mtei na Nyerere.

Hii constitution ya 1977 ni wazi kuwa Nyerere alikuwa zero brain kama bashite na Mbowe.

Hakuna Uhuru aliopgania After second world war Tanganyika was under trusteeship of UNO.

UNO ndo wametupa Uhuru sio huyu muhuni wa ccm na Asp na Tanu.

Tundu Lissu 2020-2025 for president.
Ona haka nako baada ya kusoma civics ya form four basi kanajiona kanajua sana,!

Dogo unapata jeuri ya kubwabwaja hapa na hako katecno kako sababu ya Nyerere!
 
Nyerere is overrated. Kwa umasikini huu wa kutupwa. Kuipeleka nchi vitani (akimpigania Obote arudi madarakani baada ya kupinduliwa Na IDD Amini). Nyerere alitengeneza kuogopeka na viongozi wa chini. Wakampamba .

Hint: katiba ya 1977

Udiwani,unapingika kortini
Ubunge,unapingika

Uraisi,hapana. Akitangazwa,imeisha hiyo.
Yeye alikuwa raisi. If you know you know
Nyerere kafanya mazuri mengi, na ana makosa mengi tu.

Na alilalamika watu wanaangalia makosa yake, wanaacha kuangalia mazuri.

Hapo napingana naye, watu wanatakiwa waaangalie makosa ya viongozi. Bila kuangalia makosa ya viongozi hawawezi kuyarekebisha.

Mazuri hayahitaji kurekebishwa sana, hivyo hayatakiwi kupewa kipaumbele katika kuangaliwa.

Nyerere ninamuheshimu kwa mengi mazuri aliyofanya.

Lakini, nikisikia kuna mwanasiasa anamkosoa Nyerere, nashukuru kwamba kuna mtu ana uthubutu wa kumkosoa Nyerere.

Mtei hakueleza Tundu Lisssu alisema nini.

Sitaunga mkono kumtusi Nyerere. Nyerere alikuwa ni kati ya viongozi waliojiheshimu na kuheshimu watu sana, sana tu. Angeweza kuwa dikteta mkubwa lakini hakuamua kufanya hivyo.

Ukitaka kuelewa umuhimu wa Nyerere, na alivyojiheshimu, linganisha kauki za Nyerere na za Magufuli halafu uone tofauti. Kama rais Mwinyi alisema yeye ni kichuguu na Mwalimu Nyerere ni mlima Kilimanjaro, basi Magufuli ni punje moja ya mchanga!

Lakini, Nyerere katika siasa, alifanya makosa mengi tu. Hata yeye mwenyewe alikubali hilo.

Sasa kama Nyerere mwenyewe alikubali kwamba alifanya makosa (mfano alikubali utaifushaji wa mashamba makubwa ulikuwa na mapungufu makubwa, serikali iliyachukuwa bika ya kuwa na uwezo wa kuyaendesha).

Mtu kama huyo ambaye mwenyewe kakubali makosa, kwa nini wengine wasimseme makosa yake?
 
Ebwana eh kwahiyo mpo hapa kusema Nyerere ni overrated. Na reference yenu ni kisa urais haupingwi mahakamani.

Huyu mtu alisuffer coup attempts, mbili. He survived them. Kuhakikisha hayo hayajirudii ikatungwa hiyo sheria. Na nyingine nyingine.

Hivi ni dikteta gani anatoa second chance kwa waliotaka kumpindua? Tena kesi inaenda kushughulikiwa mahakamani, na mmoja wao mpaka kuna barabara ina jina lake. Idi Amin, Gnassingbe, Kagame, Bongo, Papa Doc, Ceausescu na wengine waliwafanya nini hata waliowahisi kua wanataka kuwapindua?

Baada ya Nyerere ni rais gani mwingine kwa hapa Tz baada yake unafikiri atakufa huku hajamaliza deni la nyumba yake? Ambaye itabidi rais atakayefuata amfanyie renovation ya nyumba yake?

Mmoja hapo juu anasema alituingiza vitani kisa Obote arudi madarakani. Hiyo haijawahi kua sababu, Amin alivamia Kagera. Kagera ni Tz, a nigga just broke into our country na mlitarajia afanye nini? Akapige magoti? Akamuimbie wimbo hadi Amin achoke aiachie Kagera?

Kutokana na yeye ndiyo elimu ilisambazwa kwa wote unlike wamisionari ambao kwa elimu ilikua kimkakati. Leo unakutana na Profesa kutoka Lindi na kitabu alipiga enzi za Nyerere kwa gharama za serikali.

Magufuli alisema Lisu anatumika (logically) kwenye lile sakata la makinikia, ulimsikia Lisu akipinga? Now Tz is getting paid na alichosema Lisu cha Miga and other shit is nowhere near happening.

Kuna watu wanaishi kwa kukaririshwa. Education is out there, jisomee, siyo kitu kakukarirish mpuuzi mmoja tu na wewe unang'ang'ania hicho hicho.
Mkuu kuna majambazi hapa wanalazimisha mtu awe perfect 100%. Kuwa rais wa kwanza kwenye nchi masikini ambayo haina misingi yoyote ni kazi ngumu.
Imagine mtu alikuwa na complete power na hakufanya wizi wala kutengeneza circle yake, hawaoni alichofanya Kenyatta Sr. Rais kaleta umoja, kaondoa uwezekano wa matabaka, ukabila na udini, mwishoni kaona uwezo wake umefika kikomo kaondoka mwenyewe huku wakimuomba abaki, kawapa uhuru kwa njia ya amani kabisa. Mtu kama Nyerere ni underrated kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla.
Sasa kuna watu walitaka afanye kila kitu as if yeye ni Mungu. Sasa kaondoka, benki na viwanda alivyoacha vingine vishauzwa na kufirisika. Katiba aliyoacha bado inatumika, hivi kuna rais anagusa lifestyle ya nchi kama Mwalimu? Kama alikosea mbona hawawezi kukosoa makosa yake miaka yote tangu aondoke.
 
Tusiishi katika ukomo wa kifikira kuendana na historia ya nchi yetu. Ndiyo! Mwl. Nyerere ni Muasisi na Baba wa Taifa letu, na alikuwa kiongozi mashuhuri kwa wakati wake, ambaye alilitetea sana utu wa watu nchini, barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.

Lakini hiyo siyo sababu ya kumfanya akose wakosoaji wa misimamo yake. Kama binadamu awaye yeyote yule, alikuwa na madhaifu yake. Na jambo hili linathibitika kupitia kauli yake mwenyewe kabla mauti hayamkuta. Alikuwa "remorseful" kwa baadhi ya maamuzi yake kama kiongozi, hasa kwa yale yaliyoleta matokeo hasi.

Kwa hiyo Tundu Lissu naye ni kiongozi mwenye sifa zake ktk taifa lake. Na pia mwenye maono yake ya kulipeleka taifa letu ktk "next frontier" kupitia mapungufu ya kihistoria ambayo anaamini kwa dhati yalitokana na Baba wa Taifa. Tuzipime "constructive criticisms" zake. Wala tusizibeze kwa kauli za jumla jumla tu.

Tuje na hoja mujarabu hapa jukwaani na kuainisha wapi amekosea. Sio hoja za juu za kutumiwa na mabeberu. Kama hizo "claims" ni za kweli, wakosoaji wa TL waainishe ni lini, wapi na kwa vipi anahusika.
Mkuu inaonekana haujui Lissu aliongea maneno gani hadi Mzee Mtei kujitokeza hadharani na kukemea na kutoa angalizo au muongozo.

Kama umemuelewa Mtei tatizo siyo kumkosoa Nyerere bali kumkashifu au kumtukana au kumdhalilisha au kumdhihaki.
Nyerere amekosolewa na wengi tu na bado atakosolewa, hiyo haijawahi kuwa dhambi au kosa. Tatizo unatumia lugha gani.

Kwenye kuchagua lugha ya kukosoa hapo Lissu amekosa karama hiyo, huwa anajisahau na kutumia lugha isiyo sahihi na isiyo na staha na kuheshimiana.
Mara nyingi hulipuka kwa mihemko hasa pale anapo ona wanaomshangilia na kumshabikia wapo wengi.
Ana mihemko flani na mizuka iliyopitiliza, pamoja na kuhisi yeye anajua au ana akili sana kuliko watu wote walio mzunguka.
 
Mkuu inaonekana haujui Lissu alongea maneno gani hadi Mzee Mtei kujitokeza hadharani na kukemea na kutoa angalizo au muongozo.

Kama umemuelewa Mtei tatizo siyo kumkosoa Nyerere bali kumkashifu au kumtukana au kumdhalilisha au kumdhihaki.
Nyerere amekosolewa na wengi tu na bado atakosolewa, hiyo haijawahi kuwa dhambi au kosa. Tatizo unatumia lugha gani.

Kwenye kuchagua lugha ya kukosoa hapo Lissu amekosa karama hiyo, huwa anajisahau na kutumia lugha isiyo sahihi na isiyo na staha na kuheshimiana.
Mara nyingi hulipuka kwa mihemko hasa pale anapo ona wanaomshangilia na kumshabikia wapo wengi.
Ana mihemko flani na mizuka iliyopitiliza, pamoja na kuhisi yeye anajua au ana akili sana kuliko watu wote walio mzunguka.
Nakumbuka zilikuwa kashfa kubwa.

Kuna mtu ana rekodi ya maneno halisi aliyosema Tundu Lissu?
 
Nakumbuka zilikuwa kashfa kubwa.

Kuna mtu ana rekodi ya maneno halisi aliyosema Tundu Lissu?
Tundu Lissu amepasua jipu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge Maalum.
Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya haramu na vya halali hakuviweza.
Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.

Mkuu inawezekana mimi mawazo yango yanaegemea upande mmoja (biased) lakini unafikiri kulikuwa na ulazima wa kutumia maneno makali kama "msanii wa kisiasa", "alizoea vya haramu vya halali hakuviweza" ?

Lazima upime mazingira ya mahali unapo ongelea na mtu unayemzungumzia au kumkosoa.

Kiukweli hoja za Lissu kuhusu Nyerere na muungano zilikuwa haki tu kuhoji au kumkosoa lakini hayo maneno ya mipasho aliyotumia kama ya kwenye taarabu au kijiweni dhidi ya mtu aliyekufa tena mtu mkubwa katika jamii inayo mheshimu sana.
 
Nyerere alibariki matokeo ya uchaguzi Zanzibar kuchakachuliwa mwaka 1985.

Idris Abdul Wakil alishindwa kupata kura za kutosha, akiwa mgombea pekee.

Matokeo ya kweli yalifika mpaka Daily News, yakionesha Wakil kashindwa.

Nyerere akaamuru serikali itoe matokeo tofauti yanayoonesha Wakil kashinda.

Tangu wakati huo CCM imekuwa ikiiba kura Zanzibar.

Kwa huo mfano mmoja tu, Nyerere alifanya udanganyifu.

Sipo upande wa Nyerere wala wa Tundu Lissu, wote wana mapungufu.

Nipo katika kutafuta ukweli.
 
Tundu Lissu na rekodi yake ya kisiasa, ati sasa naye anautaka Urais.
...............

APR
17

EDWIN MTEI ASIKITISHWA NA ALAANI KITENDO CHA TUNDU LISSU KUMTUKANA BABA WA TAIFA, MWL. NYERERE

Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.

Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.

Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke:

Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao.

Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.

Edwin Mtei,

Founder Chairman of CHADEMA.
Mtei who??
 
Nyerere alibariki matokeo ya uchaguzi Zanzibar kuchakachuliwa mwaka 1985.

Idris Abdul Wakil alishindwa kupata kura za kutosha, akiwa mgombea pekee.

Matokeo ya kweli yalifika mpaka Daily News, yakionesha Wakil kashindwa.

Nyerere akaamuru serikali itoe matokeo tofauti yanayoonesha Wakil kashinda.

Tangu wakati huo CCM imekuwa ikiiba kura Zanzibar.

Kwa huo mfano mmoja tu, Nyerere alifanya udanganyifu.

Sipo upande wa Nyerere wala wa Tundu Lissu, wote wana mapungufu.

Nipo katika kutafuta ukweli.
Namimi naafikiana na wewe kuhusu maoni yako au ya Lissu kuhusu Nyerere isipokuwa kwa mtazamo wangu naona lugha aliyotumia Lissu ndiyo tatizo.
Siku zote lugha tu anayotumia ndiyo humtia dosari, na hilo tatizo wanafanana sana na bwana mkubwa fulani anayemkosoa sana.

Kwa mfano aliyomkosoa Nyerere kuhusu muungano yana mashiko kabisa na tena aliweka na ushahidi wa kutetea hoja au tuhuma zake. Shida lugha isiyo ya staha.
Mimi na wenzangu humu JF au vijiweni tunaweza kutumia lugha hiyo bila shida ila siyo yeye kwa wadhifa wake na mahali pale. yeye ni muomba kura na alikuwa anaitwa Mheshimiwa Tundu Lisssu mbunge ...
 
Back
Top Bottom