Edwin Mtei aliposikitishwa na Tundu Lissu kumtusi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Ok.. Nyerere ana makosa lakini si kwa ukali na lugha ile aliyotumia Lisu katika kumkosoa!

Yani kwa akili ya Lisu, alimuweka Nyerere kwenye kapu moja na kina Msukuma,

Kwangu mimi Lisu ni msomi anaetumia usomi wake kudanganya wapumbavu.
 
Mtu yeyote anayemlaumu Nyerere kwa kuchakachua kura Znz au baadhi ya maamuzi yake aseme hapa angekua yeye angefanyaje.

Znz imekua ally kwa ajili ya usalama. Tungekua na usalama huo huo kama ingekua inaongozwa na mtu wa cham tofauti na chake? Wewe ungekua ndiyo kiongozi ungefanyaje?

Nataka mjue kua chochote ambacho aliamua huo uamuzi ulikua ni best option kati ya options zote zilizopo. Vijiji vya ujamaa, vita n.k hizo zote zilikua ni best options kuliko zote zilizokuepo.
 
Kukosoa na kutukana vitu viwili tofauti kabisa mkuu.
 
[emoji2315]
 
Kukosoa na kutukana vitu viwili tofauti kabisa mkuu.
OK. Sawa.

Kukosoa kunaishia wapi na kutukana kunaanzia wapi?

Tundu Lissu katoa maneno gani ambayo ni ya kutukana, na si ya kukosoa.

Mimi sikumbuki vizuri maneno halisi.

Tuyachambue maneno halisi. Tukiongozwa na fact.

Kwa mfano. Mtu akisema "Nyerere hayawani" kwangu hii si fact. Ni kashfa.

Ila mtu akisema "Nyerere muuaji, alimrubuni Kassim Hanga arudi kutoka Guinea, kisha akamrubuni Kassim Hanga aende Zanzibar huku akijua kule Hanga anaenda kuuawa na Karume", hapo kuna a factual basis ya kumuita Nyerere muuaji.

Sasa maneno halisi aliyosema Tundu Lissu, ukiacha habari za watu wengine za uchambuzi wa maneno aliyosema Tundu Lissu, ni yapi?

Tuyachambue maneno aliyosema Tundu Lissu, tuangalie kama yana fact au hayana fact au ni kashfa au ni matusi.
 
Ok.. Nyerere ana makosa lakini si kwa ukali na lugha ile aliyotumia Lisu katika kumkosoa!

Yani kwa akili ya Lisu, alimuweka Nyerere kwenye kapu moja na kina Msukuma,

Kwangu mimi Lisu ni msomi anaetumia usomi wake kudanganya wapumbavu.
Wanasiasa karibu wote wanatumia exaggeration katika sanaa yao.

Hiki ni kitu cha kuwa makini nacho sana.

Hata wewe.

Kwa nini unasema Tundu Lissu alimuweka Nyerere kundi moja na Msukuma? Alisema Nyerere ni sawa na Msukuma?
 
Mzee Mtei, mtu mzima mwenye heshima yake ilibidi ajitenge na maneno ya Lissu kama ifuatavyo.....

Tundu Lissu.. "yule Nyerere aliishi maisha ya ulaghai,udanganyifu na vitisho kama vile majambazi/matapeli Papaa Musofe na Alex Massawe!?"

Hayo ni maneno kayatamka Tundu Lissu, mpaka leo hakuomba radhi kuwa mdomo ulikuwa kwenye overspeed.
Leo naye ati anataka urais.
 
Kwamba Karume alimwambia Nyerere ampeleke Hanga huko Znz? Au Nyerere alioda Karume amuue Hanga na yeye ndiye atakayemfikisha Hanga kwa Karume?
 
Wanasiasa karibu wote wanatumia exaggeration katika sanaa yao.

Hiki ni kitu cha kuwa makini nacho sana.

Hata wewe.

Kwa nini unasema Tundu Lissu alimuweka Nyerere kundi moja na Msukuma? Alisema Nyerere ni sawa na Msukuma?
Ungesikiliza kwanza hizo crip ndio ujue akili za Lisu zikoje
 
Nyerere hakudanganya na kuendeleza utawala wake kwa vitisho?

Twende na facts.
 
Reactions: Pep
Kwamba Karume alimwambia Nyerere ampeleke Hanga huko Znz? Au Nyerere alioda Karume amuue Hanga na yeye ndiye atakayemfikisha Hanga kwa Karume?
Huo ni mfano wa kuonesha kwamba kikitu kikiwa fact,mtu kusema fact si kashfa.

Karume alimuomba Nyerere ampeleke Hanga Zanzibar, Nyerere akamrubuni Hanga atoke Guinea alipokuwa kajificha arudi Tanzania. Hanga alipofika Tanzania Nyerere akamrubuni Hanga aende Zanzibar. Akijua Hanga anaenda kuuawa na Karume huko.

Hanga akaenda Zanzibar, akauawa.
 
Nyerere hakudanganya na kuendeleza utawala wake kwa vitisho?

Twende na facts.
I challenge you ,huyo mtaalam wa matusi Tundu Lissu aseme hivyo tena kwa Magufuli leo.
Kama ataiona Tanzania itakuwa mjaaliwa.

Fact ni kwamba alimlinganisha Mwalimu na matapeli!
Hilo la kwamba Mwalimu aliendesha utwala wake kwa vitisho anzisha mada kuhusiana na hilo ambalo ni tofauti na mada hii.
 
Hilo bandiko lipo humu humu JF ana mzee mtei aliandika mwenye maana ni member humu
 
Binafsi sijawahi kumwelewa kiviile mzee wetu Nyerere,Kuna maamuzi mengi ya kiboya aliyafanya na kuficha ukweli, hakuwa muwazi na alikuwa mbinafsi sana, aliona yeye ndo Yuko sahihi tu na watanzania wote no maboya. Ni Kama kagame anavyoiongoza Rwanda
Nyie madogo kuweni na heshima kidogo japo hata kwa Baba Wa taifa, hizo schoolboy politics zitawaletea shida,
 
Nyerere katapeli watu ana degree ya pili , wakati ana degree ya kwanza.

Unaelewa hilo?
 
Reactions: Pep
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…