Edwin Mtei aliposikitishwa na Tundu Lissu kumtusi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Edwin Mtei aliposikitishwa na Tundu Lissu kumtusi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Nyerere kafanya mazuri mengi, na ana makosa mengi tu.

Na alilalamika watu wanaangalia makosa yake, wanaacha kuangalia mazuri.

Hapo napingana naye, watu wanatakiwa waaangalie makosa ya viongozi. Bila kuangalia makosa ya viongozi hawawezi kuyarekebisha.

Mazuri hayahitaji kurekebishwa sana, hivyo hayatakiwi kupewa kipaumbele katika kuangaliwa.

Nyerere ninamuheshimu kwa mengi mazuri aliyofanya.

Lakini, nikisikia kuna mwanasiasa anamkosoa Nyerere, nashukuru kwamba kuna mtu ana uthubutu wa kumkosoa Nyerere.

Mtei hakueleza Tundu Lisssu alisema nini.

Sitaunga mkono kumtusi Nyerere. Nyerere alikuwa ni kati ya viongozi waliojiheshimu na kuheshimu watu sana, sana tu. Angeweza kuwa dikteta mkubwa lakini hakuamua kufanya hivyo.

Ukitaka kuelewa umuhimu wa Nyerere, na alivyojiheshimu, linganisha kauki za Nyerere na za Magufuli halafu uone tofauti. Kama rais Mwinyi alisema yeye ni kichuguu na Mwalimu Nyerere ni mlima Kilimanjaro, basi Magufuli ni punje moja ya mchanga!

Lakini, Nyerere katika siasa, alifanya makosa mengi tu. Hata yeye mwenyewe alikubali hilo.

Sasa kama Nyerere mwenyewe alikubali kwamba alifanya makosa (mfano alikubali utaifushaji wa mashamba makubwa ulikuwa na mapungufu makubwa, serikali iliyachukuwa bika ya kuwa na uwezo wa kuyaendesha).

Mtu kama huyo ambaye mwenyewe kakubali makosa, kwa nini wengine wasimseme makosa yake?
Awamu ya kwanza pana makosa tulifanya kwani sisi si malaika serikali zote hizi zinaongozwa na watu mabaya au makosa yetu yarekebisheni ila cha ajabu hata mema au mazuri tuliyoyafanya mnayahoji? Nukuu ya mwalimu Nyerere.
 
Mema gani? Nani kasema mema?

Kuna mambo Nyerere aliyaona mema wakati watu wengine waliona si mema.

Sasa kwa nini asihojiwe, ikiwa hata jambo kuwa jema au si jema ni mjadala, kwa nini asihojiwe?

Alitaka asihojiwe? Kiongozi kutaka asihojiwe si ndiyo udikteta wenyewe huo?
 
Nimejaribu kutoa moja ya nukuu zake kuhusu jambo hili
 
Nimejaribu kutoa moja ya nukuu zake kuhusu jambo hili
Hiyo ni kauli ya kisiasa isiyo na facts.

Nyerere mwenyewe, kwa kauli yake, alisema kwamba, kuna mambo alikosea, akataja kutaifisha mashamba makubwa wakati serikali haijaweza kujenga ubunifu wa kuyaendesha kwa tija, kuwa ni jambo alilokosea.

Sasa kama yeye mwenyewe anajua kakosea mambo, kwa nini wengine wasimhoji?
 
Mtiririko wa wachangiaji unaonyesha kuwa vijana wa sasa matumizi yao ya akili yapo chini sana na wabishi sana, kwa muktadha huo wameukumbatia ujinga kuwa sehemu ya maisha ingawa wamekaa kwenye majengo yanayoitwa shule!
 
Mkuu kuna majambazi hapa wanalazimisha mtu awe perfect 100%. Kuwa rais wa kwanza kwenye nchi masikini ambayo haina misingi yoyote ni kazi ngumu.
Imagine mtu alikuwa na complete power na hakufanya wizi wala kutengeneza circle yake, hawaoni alichofanya Kenyatta Sr. Rais kaleta umoja, kaondoa uwezekano wa matabaka, ukabila na udini, mwishoni kaona uwezo wake umefika kikomo kaondoka mwenyewe huku wakimuomba abaki, kawapa uhuru kwa njia ya amani kabisa. Mtu kama Nyerere ni underrated kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla.
Sasa kuna watu walitaka afanye kila kitu as if yeye ni Mungu. Sasa kaondoka, benki na viwanda alivyoacha vingine vishauzwa na kufirisika. Katiba aliyoacha bado inatumika, hivi kuna rais anagusa lifestyle ya nchi kama Mwalimu? Kama alikosea mbona hawawezi kukosoa makosa yake miaka yote tangu aondoke.

Mtu asiyeweza kusema asante, huwa anakufa lofa. TL yeye amefanya nini cha ajabu cha kupenda kumdharau Nyerere kila wakati akipewa nafasi?
Naona huruma. Kambona alifikiria itakuwa rahisi kwake kudharau mambo ya msingi na kujiunga ma wazungu. Alirudi kachoka, hana mvuto, halafu na mastery kama yuko kwenye kipindi cha Jahazi cha Marehemu Kibonde.
 
Hiyo ni kauli ya kisiasa isiyo na facts.

Nyerere mwenyewe, kwa kauli yake, alisema kwamba, kuna mambo alikosea, akataja kutaifisha mashamba makubwa wakati serikali haijaweza kujenga ubunifu wa kuyaendesha kwa tija, kuwa ni jambo alilokosea.

Sasa kama yeye mwenyewe anajua kakosea mambo, kwa nini wengine wasimhoji?

Nyerere hakuwahi kujutia kutekeleza kwa vitendo azimio la Arusha. Infact alikufa akiamini ipo siku Tanzania itarudi kule kule inakojaribu kukukimbia.
Shida yetu ni kukosa staha tunapozungumza hoja zetu, na kufikiria sisi ni super humans. And yet, we all have different flaws which make us imperfect
 
Nyerere katapeli watu ana degree ya pili , wakati ana degree ya kwanza.

Unaelewa hilo?
Substantiate!
Na jaribu kuelewa hii quote toka Wikipedia, and THINK about it:

Edinburgh University: 1949–1952[edit]

The Old College in Edinburgh
In April 1949, Nyerere flew from Dar es Salaam to Southampton, England.[71] He then travelled, by train, from London to Edinburgh.[72] In the city, Nyerere took lodgings in a building for "colonial persons" in The Grange suburb.[73] Starting his studies at the University of Edinburgh, he began with a short course in chemistry and physics and also passed Higher English in the Scottish Universities Preliminary Examination.[74] In October 1949 he was accepted for entry to study for a Master of Artsdegree at the University of Edinburgh's Faculty of Arts; his was an Ordinary Degree of Master of Arts which, in contrast to common uses of the term "Master of Arts", was considered an undergraduate rather than postgraduate degree, the equivalent of a Bachelor of Arts in most English universities.[75]
 
Mtiririko wa wachangiaji unaonyesha kuwa vijana wa sasa matumizi yao ya akili yapo chini sana na wabishi sana, kwa muktadha huo wameukumbatia ujinga kuwa sehemu ya maisha ingawa wamekaa kwenye majengo yanayoitwa shule!
Mkuu ill informed young minds with ill conclusions, rapidly racing down hill!
Vijana wa leo ni kashfa kwa elimu waliyonayo.
 
Substantiate!
Na jaribu kuelewa hii quote toka Wikipedia, and THINK about it:

Edinburgh University: 1949–1952[edit]

The Old College in Edinburgh
In April 1949, Nyerere flew from Dar es Salaam to Southampton, England.[71] He then travelled, by train, from London to Edinburgh.[72] In the city, Nyerere took lodgings in a building for "colonial persons" in The Grange suburb.[73] Starting his studies at the University of Edinburgh, he began with a short course in chemistry and physics and also passed Higher English in the Scottish Universities Preliminary Examination.[74] In October 1949 he was accepted for entry to study for a Master of Artsdegree at the University of Edinburgh's Faculty of Arts; his was an Ordinary Degree of Master of Arts which, in contrast to common uses of the term "Master of Arts", was considered an undergraduate rather than postgraduate degree, the equivalent of a Bachelor of Arts in most English universities.[75]
Wewe uliyeiweka hiyo quote umeielewa?
 
Tundu Lissu na rekodi yake ya kisiasa, ati sasa naye anautaka Urais.
...............

APR
17

EDWIN MTEI ASIKITISHWA NA ALAANI KITENDO CHA TUNDU LISSU KUMTUKANA BABA WA TAIFA, MWL. NYERERE

Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.

Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.

Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke:

Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao.

Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.

Edwin Mtei,

Founder Chairman of CHADEMA.
Huyo msaliti Lissu hawezi pita hata kwenye kura za maoni za CDM wenye chama wameshasema anapoteza muda wake tu!!
 
Nyerere katapeli watu ana degree ya pili , wakati ana degree ya kwanza.

Unaelewa hilo?
Mkuu Idont believe you can be so low to spin facts unazozisoma kwa macho.
Nimekuletea quote ujisomee mwenyewe maana halisi ya somo la Master of Arts katika degree ya kwanza ya Mwalimu.
Ndiyo maana nikakushauri.
THINK!!!
 
Nyerere hakuwahi kujutia kutekeleza kwa vitendo azimio la Arusha. Infact alikufa akiamini ipo siku Tanzania itarudi kule kule inakojaribu kukukimbia.
Shida yetu ni kukosa staha tunapozungumza hoja zetu, na kufikiria sisi ni super humans. And yet, we all have different flaws which make us imperfect
Sijaongelea Azimio la Arusha.

Nimeandika Nyerere alisema kwamba zoezi la utaifishaji wa mashamba alifanya makosa kutaifisha kiholela kabla serikali haijawa na uwezo wa kuyaendesha.

Unaelewa kwamba huja address issue niliyoielezea, umekuja na issue tofauti?

Kwani haiwezekani Nyerere kutojutia Azimio la Arusha kama unavyosema, na hapo hapo akakubali kwamba kuna makosa yalifanyika katika utaifishaji wa mashamba?

Mnaosema habari za staha, Magufuli mwenye maneno ya kunya ana staha?

Hivi karibuni kasema ataamua kumkata mtu yeyote kutoka kwenye mbio za ubunge, kwa kuangalia atakavyoamka siku hiyo, hayo ninmaneno ya staha?

Amesema atawapiga wapinzani mpaka shangazi zao.

Hayo ni maneno ya staha?

Kama staha ni kigezo cha urais, Magufuli anastahili kuwa rais?
 
Mkuu ill informed young minds with ill conclusions, rapidly racing down hill!
Vijana wa leo ni kashfa kwa elimu waliyonayo.
Twende kwa facts, si kwa kashfa tu.

Nyerere kafanya mazuri mengi, lakini si mtume wala malaika.

Alipokosea, ni vizuri watu waseme.

Na wewe unapoita tusi na kukosa staha, mwingine ataona ni fair criticism.

Msitake kumfanya Nyerere ni some sacred cow.

Kwa mtu aliyejinadi kuwa muum8ni wa usawa wa binadamu, kumfanya Nyerere kuwa Malaika fulani si kumtendea haki yeye mwenyewe huyo Nyerere.

Na kunaonesha kuwa hamjamuelewa.
 
No body said Nyerere is a sacred cow.
Elewa we are arguing about Tundu Lissu KUMTUSI Mwalimu, is that hard to understand?
 
Mkuu Idont believe you can be so low to spin facts unazozisoma kwa macho.
Nimekuletea quote ujisomee mwenyewe maana halisi ya somo la Master of Arts katika degree ya kwanza ya Mwalimu.
Ndiyo maana nikakushauri.
THINK!!!

Umeongelea kuhusu ku spin facts.

Fine.

Let's talk facts. No spin.

Nyerere alikuwa na degree ya kwanza au ya pili?
 
No body said Nyerere is a sacred cow.
Elewa we are arguing about Tundu Lissu KUMTUSI Mwalimu, is that hard to understand?
Kamtusi wapi? Katumia tusi gani? Kwa nini hilo ni tusi na si neno sawa kumsema Nyerere?

Nyerere alipinga sheria za kikoloni zilizokandamiza Waafrika.

Akapata kuwa rais, hakuziondoa sheria hizi za kikoloni.

Akazitumia yeye mwenyewe kukandamiza watu.

Mpaka Chief Justice Nyalali alizisema hizi sheria 40 kandamizi.

Mpaka Nyerere anafariki hizi sheria zipo.

Mtu akimuita Nyerere Ndumilakuwili, tapeli, alipinga sheria kandamizi wakati hana utawala wa nchi, akapata utawala, akaziona sheria hizi kandamizi ni tamu, hakuziondoa, atakuwa kamtusi Nyerere?

Au kasema ukweli tu?

https://www.academia.edu/17581138/Judge_Nyalalis_Report_on_40_Repressive_Laws_in_Tanzania
 
Mkuu anzisha mada yako kwa kile wewe unachokiona kwa Mwalimu.
Usidandie mada.
And belive me you will be beaten hands down.

Mada hii ni unafiki wa mtu anaitwa Tundu Lissu kutaka urais wa Tanzania huku akijua bila Mwalimu angekuwa mpagazi au mfanyakazi wa ndani.Kile anachokitaka Lissu ni kuendesha nchi iliyo asisiwa katika misingi ambayo asingeweza kufika hapo alipo.
 
Back
Top Bottom