Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi

Ooh, ni huzuni, ni majonzi, ni maombolezo. Mwenzetu ametutoka akiwa bado kijana. Alikuwa mwema sana, tena mkarimu. Hakupenda ugomvi, fitina wala chuki. Hakuwa mchoyo wala bahili. Wote waliokuwa wakimuomba awakopeshe pesa, walipewa mikopo tena bila masharti. Na wale walioshindwa kurudisha mikopo aliwasamehe bure tu. Akisikia jirani anaumwa, haraka sana alikuwa anaenda kumuona na kumpa pole.

Akiombwa kuchangia sherehe, ujenzi au gharama za misiba, hakusita kutoa mchango. Alikuwa anamiliki nyumba nzuri ya kisasa na magari ya kifahari lakini hakujivuna wala kuwa na kiburi. Unyenyekevu ilikuwa sehemu ya tabia yake. Akialikwa arusini alikuwa anakaa viti vya nyuma. Alikuwa msomi mwenye shahada ya uzamivu. Hata hivyo hakupenda kujikweza wala kuonekana mtu mkubwa. Akisikia ndugu wamefarakana alikuwa wa kwanza kwenda kuwapatanisha. Akisikia mtu amekatishwa tamaa na jambo fulani anamtia moyo kwa maneno mazuri ya faraja. Kinywa chake kilikuwa hakitoi matusi wala maneno ya kashfa au dharau. Alikuwa anampenda sana mke wake. Hakuwahi kumpiga kofi wala ngumi tangu walipooana. Hakika alikuwa mtu mwema sana. Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi.

Hakukosea aliyesema ‘duniani sisi wanadamu ni wasafiri na wapitaji.’ Magonjwa, ajali, vita nk vinatuondoa duniani hata kabla ya wakati wetu kufika. Hakuna anayeweza kukwepa kifo. Kuna takwimu fulani zinasema kwamba takriban watu 150,000 wanaaga dunia kila siku kwa sababu ya magonjwa tu! Kwa sababu hiyo, misiba imekuwa ikishuhudiwa kila siku pia. Na kila mara wakati wa maziko/mazishi huwa tunawasikia viongozi wa dini au wafiwa wakimuomba Mungu aiweke mahali pema peponi, roho ya mpendwa wao aliyeiaga dunia.

Hapa JF, ‘members’ wanajulikana pia kama ‘Great Thinkers.’ Great Thinker, sio mwepesi wa kuamini au kukubali jambo fulani, bila kulitafakari au kulichunguza kwa makini jambo hilo. Na mimi ni miongoni mwao; nimejaribu kuchunguza Maandiko matakatifu kuhusu sala au maombi hayo tunayomuomba Mungu kwamba awaweke mahali pema peponi wenzetu waliotutoka. Je, Mungu anasikia maombi hayo na kufanya kama tunavyomuomba? Kwa utafiti wangu mdogo, nimegundua Mungu hafanyi kama tunavyomuomba. Mtu akifa, sekunde ile ile roho yake ama inaingia mahali pema peponi au inaingia kuzimu kwenye mateso. Maombi yetu hayawezi kamwe kubadili mahali roho ya mtu inapowekwa. Nimehakikisha hilo kwa kusoma Luka 16:19-31. Kwa sababu hiyo tufanye bidii kuishi maisha mema/matakatifu(Waebrania 12:14) ili siku tukiondoka duniani tuwe na uhakika kwamba Mungu atatuweka mahali pema peponi na kutupatia pumziko na raha ya milele.
Mkuu umeomboleza kama Mnyakyusa!
Nasikia wanyakyusa wanalia kisawasawa, hata wasipojua nani kafa!
 
Uwepo wa Mungu hauthibitishwi na watu ni kutokana na nguvu ya Roho mtakatifu ndo humfunulia mtu nuru ya kuona uwepo wa Mungu. Unamjua Roho Mtakatifu?
Umeambiwa kuthibitisha uongo mmoja, umeshindwa, unazusha uongo mwingine kabla hujathibitisha wa kwanza.

Roho Mtakatifu ni nini? Unaweza kuthibitisha huyo Roho Mtakatifu yupo kwli na si hadithi za uongo za watu tu?
 
Hakika huko kwenye giza totoro, hivi unawezaje kumthibitisha kwamba kiranga ni binadamu sio roboti.
Usikalili kwamba kila habar ya uwepo wa Mungu ni uongo utakuja kuumia.
 
Unajuaje aliyewaumba ni Mungu?

Yani hapo ni sawasawa na kusema Toyota imeumbwa na Mjerumani, kwa sababu Toyota ni lazima iwe na muumbaji.

Sasa unajuaje muumbaji ni Mjerumani na si Mchina au Mjapani?
Biblia imesema wazi.
 
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu mwenye enzi yupo kweli na kwamba habari za kuwepo kwake si za kutungwa na watu tu?
Hata wewe Kiranga (Shetani) ni matokeo ya uwepo wa Mungu.
Unajuaje Biblia inachosema ni kweli na si uongo ulioandikwa na watu tu?
Kiranga kwa kilugha chetu ni Shetani kwa hiyo sishangai sana kupinga uwepo wa Mungu.
 
Hujathibitisha kwamba Mungu yupo, wala Shetani.

Thibitisha, bila uthibitisho, tutajuaje hizo habari zako si hadithi za watu tu?
 
Ooh, ni huzuni, ni majonzi, ni maombolezo. Mwenzetu ametutoka akiwa bado kijana. Alikuwa mwema sana, tena mkarimu. Hakupenda ugomvi, fitina wala chuki. Hakuwa mchoyo wala bahili. Wote waliokuwa wakimuomba awakopeshe pesa, walipewa mikopo tena bila masharti. Na wale walioshindwa kurudisha mikopo aliwasamehe bure tu. Akisikia jirani anaumwa, haraka sana alikuwa anaenda kumuona na kumpa pole.

Akiombwa kuchangia sherehe, ujenzi au gharama za misiba, hakusita kutoa mchango. Alikuwa anamiliki nyumba nzuri ya kisasa na magari ya kifahari lakini hakujivuna wala kuwa na kiburi. Unyenyekevu ilikuwa sehemu ya tabia yake. Akialikwa arusini alikuwa anakaa viti vya nyuma. Alikuwa msomi mwenye shahada ya uzamivu. Hata hivyo hakupenda kujikweza wala kuonekana mtu mkubwa. Akisikia ndugu wamefarakana alikuwa wa kwanza kwenda kuwapatanisha. Akisikia mtu amekatishwa tamaa na jambo fulani anamtia moyo kwa maneno mazuri ya faraja. Kinywa chake kilikuwa hakitoi matusi wala maneno ya kashfa au dharau. Alikuwa anampenda sana mke wake. Hakuwahi kumpiga kofi wala ngumi tangu walipooana. Hakika alikuwa mtu mwema sana. Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi.

Hakukosea aliyesema ‘duniani sisi wanadamu ni wasafiri na wapitaji.’ Magonjwa, ajali, vita nk vinatuondoa duniani hata kabla ya wakati wetu kufika. Hakuna anayeweza kukwepa kifo. Kuna takwimu fulani zinasema kwamba takriban watu 150,000 wanaaga dunia kila siku kwa sababu ya magonjwa tu! Kwa sababu hiyo, misiba imekuwa ikishuhudiwa kila siku pia. Na kila mara wakati wa maziko/mazishi huwa tunawasikia viongozi wa dini au wafiwa wakimuomba Mungu aiweke mahali pema peponi, roho ya mpendwa wao aliyeiaga dunia.

Hapa JF, ‘members’ wanajulikana pia kama ‘Great Thinkers.’ Great Thinker, sio mwepesi wa kuamini au kukubali jambo fulani, bila kulitafakari au kulichunguza kwa makini jambo hilo. Na mimi ni miongoni mwao; nimejaribu kuchunguza Maandiko matakatifu kuhusu sala au maombi hayo tunayomuomba Mungu kwamba awaweke mahali pema peponi wenzetu waliotutoka. Je, Mungu anasikia maombi hayo na kufanya kama tunavyomuomba? Kwa utafiti wangu mdogo, nimegundua Mungu hafanyi kama tunavyomuomba. Mtu akifa, sekunde ile ile roho yake ama inaingia mahali pema peponi au inaingia kuzimu kwenye mateso. Maombi yetu hayawezi kamwe kubadili mahali roho ya mtu inapowekwa. Nimehakikisha hilo kwa kusoma Luka 16:19-31. Kwa sababu hiyo tufanye bidii kuishi maisha mema/matakatifu(Waebrania 12:14) ili siku tukiondoka duniani tuwe na uhakika kwamba Mungu atatuweka mahali pema peponi na kutupatia pumziko na raha ya milele.
asante mtumishi
 
Unajuaje Biblia inachosema ni kweli na si uongo ulioandikwa na watu tu?
Biblia inaeleza jinsi Yesu alivyokuwa akikemea pepo/majini, yanatii na kutoka. Leo hii kwa Jina la Yesu tunakemea pepo na pepo wanatoka. Hujasikia watu waliokuwa viziwi au bubu kwa sababu ya pepo? Pepo walipokemewa na kutoka, waliokuwa viziwi walianza kusikia na waliokuwa mabubu kwa sababu ya pepo walianza kuongea. Biblia ingekuwa sio ya kweli hayo yasingefanyika leo.
 
Hata wafanya maigizo wanaweza kusema wanatoa pepo.

Thibitisha Mungu yupo.

Biblia imejaa contradiction na hivyo haiwezi kuwa kitabu cha Mungu.
 
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu mwenye enzi yupo kweli na kwamba habari za kuwepo kwake si za kutungwa na watu tu?

Ila wee jamaa unafurahisha sana 😄 upande huu ndio huwa unawasumbua maana hawajulikani Mungu yupi wanamwabudu. Lakini kwa waislamu unaonekana empty kabisa. Pole sana kiranga.
 
Ooh, ni huzuni, ni majonzi, ni maombolezo. Mwenzetu ametutoka akiwa bado kijana. Alikuwa mwema sana, tena mkarimu. Hakupenda ugomvi, fitina wala chuki. Hakuwa mchoyo wala bahili. Wote waliokuwa wakimuomba awakopeshe pesa, walipewa mikopo tena bila masharti. Na wale walioshindwa kurudisha mikopo aliwasamehe bure tu. Akisikia jirani anaumwa, haraka sana alikuwa anaenda kumuona na kumpa pole.

Akiombwa kuchangia sherehe, ujenzi au gharama za misiba, hakusita kutoa mchango. Alikuwa anamiliki nyumba nzuri ya kisasa na magari ya kifahari lakini hakujivuna wala kuwa na kiburi. Unyenyekevu ilikuwa sehemu ya tabia yake. Akialikwa arusini alikuwa anakaa viti vya nyuma. Alikuwa msomi mwenye shahada ya uzamivu. Hata hivyo hakupenda kujikweza wala kuonekana mtu mkubwa. Akisikia ndugu wamefarakana alikuwa wa kwanza kwenda kuwapatanisha. Akisikia mtu amekatishwa tamaa na jambo fulani anamtia moyo kwa maneno mazuri ya faraja. Kinywa chake kilikuwa hakitoi matusi wala maneno ya kashfa au dharau. Alikuwa anampenda sana mke wake. Hakuwahi kumpiga kofi wala ngumi tangu walipooana. Hakika alikuwa mtu mwema sana. Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi.

Hakukosea aliyesema ‘duniani sisi wanadamu ni wasafiri na wapitaji.’ Magonjwa, ajali, vita nk vinatuondoa duniani hata kabla ya wakati wetu kufika. Hakuna anayeweza kukwepa kifo. Kuna takwimu fulani zinasema kwamba takriban watu 150,000 wanaaga dunia kila siku kwa sababu ya magonjwa tu! Kwa sababu hiyo, misiba imekuwa ikishuhudiwa kila siku pia. Na kila mara wakati wa maziko/mazishi huwa tunawasikia viongozi wa dini au wafiwa wakimuomba Mungu aiweke mahali pema peponi, roho ya mpendwa wao aliyeiaga dunia.

Hapa JF, ‘members’ wanajulikana pia kama ‘Great Thinkers.’ Great Thinker, sio mwepesi wa kuamini au kukubali jambo fulani, bila kulitafakari au kulichunguza kwa makini jambo hilo. Na mimi ni miongoni mwao; nimejaribu kuchunguza Maandiko matakatifu kuhusu sala au maombi hayo tunayomuomba Mungu kwamba awaweke mahali pema peponi wenzetu waliotutoka. Je, Mungu anasikia maombi hayo na kufanya kama tunavyomuomba? Kwa utafiti wangu mdogo, nimegundua Mungu hafanyi kama tunavyomuomba. Mtu akifa, sekunde ile ile roho yake ama inaingia mahali pema peponi au inaingia kuzimu kwenye mateso. Maombi yetu hayawezi kamwe kubadili mahali roho ya mtu inapowekwa. Nimehakikisha hilo kwa kusoma Luka 16:19-31. Kwa sababu hiyo tufanye bidii kuishi maisha mema/matakatifu(Waebrania 12:14) ili siku tukiondoka duniani tuwe na uhakika kwamba Mungu atatuweka mahali pema peponi na kutupatia pumziko na raha ya milele.
Ni MTU asiyejulikana?
 
Ila wee jamaa unafurahisha sana [emoji1] upande huu ndio huwa unawasumbua maana hawajulikani Mungu yupi wanamwabudu. Lakini kwa waislamu unaonekana empty kabisa. Pole sana kiranga.
Thibitisha Mungu yupo.
 
Hata wafanya maigizo wanaweza kusema wanatoa pepo.

Thibitisha Mungu yupo.

Biblia imejaa contradiction na hivyo haiwezi kuwa kitabu cha Mungu.
"Hakiwezi kuwa kitabu Cha Mungu" unataka kutuambia kuwa Mungu yupo Ila Biblia si kitabu chake kwa sababu kina mkanganyiko?
 
Back
Top Bottom