Eeh Mungu, sijui kipi kinachofuata, natumaini ni chenye unafuu kidogo zaidi ya ugumu huu

FORBIDDEN HISTORY

Senior Member
Joined
Jul 28, 2024
Posts
125
Reaction score
224
Nini maana ya maisha?, Nini sababu ya uwepo huu?, Ni ipi siri ya safari hii?

Nini maana yangu? Nini sababu ya uwepo wangu? Ni ipi siri ya uundaji wangu?

Ni ujinga wangu au ni hatma ya safari yangu?
Ni mapungufu yangu au ni ubabe wao?
Ni dhambi zangu au ni laana yangu?

Je hii safari yangu hadi kifo ni "challenge" ilioandaliwa tayari?

Je mimi ni "NPC" (non-playable character) nilioundwa kwa madhumuni fulani na siwezi toka katika system.

Ni kwamba sijakuwa kiroho zaidi?
Ni kwamba sina bidii zaidi?
Ni kwamba sina bahati zaidi?
Ni kwamba sina akili zaidi?

AU TU,

Ni kwamba basi, SISTAHILI.

Je NEEMA anastahili kila mtu?
Je REHEMA anastahili ya kila mtu?
Je FADHILI anastahilii kila mtu?
Je HURUMA anastahili kila mtu?
Je BARAKA anastahili kila mtu?

AU BASI TU,

Maisha na ulimwengu mzima ni fumbo ambalo linahitaji passwords na labda wachache walifanikiwa kujua.

AU BASI TU,

Sina bidii kwa Mungu mkuu.

JIONI NJEMA.
 
20240723_155504.jpg
 
Whatever happening to you, you're in positive side, sababu hujui kabla ya kuja duniani ulikuwa wapi na hujui baada ya hapa utaenda wapi?, ulikuja bila kitu, utaondoka bila kitu.
Kwahiyo hapa duniani wewe ishi tu the way maisha yanakupeleka😆, usicomplicate. Heaven, hell sijui nini hizo zote bla bla tu na kuongeza ugumu wa maisha
 
Mambo magumu sana sana kwa tulio wengi,huku tukiona wengine wakiwa na maisha na hali nzuri za kufuru za maisha. Inauma na kuumiza sana.
Ni siku 3 leo silali nakosa usingiz.Si kwamba nataka maisha ya anasa la hasha! Naomba tu niondolewe kwenye mashida haya ya mashida shida.Mbaya zaidi nakosa msaada.
Mungu ni mwema,Mungu awape afya na hitaji lenu note wenye bahati.
 
Nilitaka nianze Kwa kuandika kibongo bongo asilimia kubwa ya maisha ya wabongo ni bongo nyoso.Bahati nzuri au mbaya au isivyo bahati kabisa hili tatizo ni la kidunia.

Maisha ya mwanadamu tafsiri yake ni mtambuka.Jibu lako sahihi katika maisha Kwa mwingine linawezekana lisiwe sahihi.La umuhimu ila sio sana maisha ni vile unavyoishi usiwaze sana na kujiumiza Kwa maswali ambayo yatakumiza kichwa afu baadaye israel mtoa roho anasepa na pumzi uliyopewa bure

Ila kiukweli maisha kitaa yamekuwa magumu mpaka inafikia hatua watu wanaona Bora kufa kuliko kuendelea kuishi.Usife moyo kesho Yako huijui amini ipo ili uendelee kukomaa pia Kuna watu wanapitia magumu kuliko wewe lakini Bado wanapambania
 
Umeona eeh
Uzima na afya njema ndo utajiri tosha.
 
Ahsante mkuu, ahsante sana.
 
Kiongozi pole kwa ambayo yanakusibu maana siri ya maisha hakuna aijuaye

Utofauti wa maisha usifanye ukakata tamaa maana wapo waliokuwa Kama wewe lakini wakaweza kuvuka katika hali hizo

Amini katika njia yako na uzidi kujijenga
Usisahau kunywa maji
Ahsante mkuu, ahsante sana.
 
Back
Top Bottom