EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Majizo na kampuni yake wanatafuta ugali sasa channel ilishakamata halafu mtu mmoja anahoji mikopo wakati hiyo serikali ndo ina TRA, INA BRELA, TCRA, INATAWALA hapo kama Gerald Hando ajitokeze aombe msamaha hadharani na akae nje ya kituo mwezi 1 atakuwa amejirekebisha
Alitakiwa asome maudhui ya radio na TV yao
 
Kwa hiyo hii comment yako ndio Ina ishara za usomi?
 
TANGAZO la MD wa E-FM la kumchukulia hatua Gerald Hando limetolewa kiwa Chalinze Msoga hii ina maana gani wadau tuchambue kinagaubaga
 
Yaani wote tuungane na msimamo wa serikali kwa lazima hata kama tuna mawazo tofauti?
 
Kuna Kosa gani amefanya?
 
Mali ni ya Majizo ila uamuzi wa Majizo ni wa kwake binafsi na hataki matatizo na Mamlaka na wewe tafuta chombo chako cha mawasiliano fanya kama Hando life ni tight mno kwa sasa why uingie matatizo na Mamlaka tena kupitia kwa mtu ambaye hajui umetafutaje hizo Mali kwa jasho kubwa?
 
Wamesema wanazingatia sheria lakini kwenye andiko hilo hawajatuambia huyo Hando amevunja sheria ipi? Haya mambo ya kuiogopa serikali hata mahala ambapo hujavunja sheria ni mambo ya kipumbavu yaliyoanza enzi za Marehemu. Marehemu ametuharibia nchi.
 
Muhimu ujumbe ulishafika, hii serikali inasifa zote za kidikteta, haina tofauti yoyote na ile iliyopita.

Majizzo anaposema wasikilizaji wa EFM wamemlalamikia kwa ile kauli ya Hando ni kama anatuona watanzania wote wajinga, bora angetafuta excuse nyingine..hii aliyoitoa amejitungia tu.
 
Amekiuka maadili ya taaluma, ashughulikiwe vilivyo, suala la umiliki halihusiani.

Ni wakati muafaka kuondoa watu wa hovyo katika tasnia
Maadili gani ya umma aliyokiuka Hando?

Suala la public kujadiliwa public kuna ubaya gani? kwani hiyo mikopo inamuhusu nani mpaka isijadiliwe na umma? na ni nani wanaolipa hiyo mikopo kama sio watz? sasa kwanini walipaji wasiruhusiwe kuijadili hiyo mikopo inayowahusu?

Listen, haya mambo ya kijinga ya kusifia muda wote hufanywa na wapumbavu pekee, lakini werevu watakaa kimya kwa muda fulani, ila iko siku wataongea ukweli, hicho ndicho Hando alichofanya, na kitafanywa na mwingine tena next time, hili sio taifa la wapumbavu kama mnavyotaka liwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…