EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Husda ya nini jombaa..!!
Hata mm sio ngumbaru shule ipo ya kutosha ya ndani na nje ya Tz na sasa ni mstaafu nanyonya pensheni tu.

Ndio maana nimesema wasomi wengi wao ni empty set sio wote.
Nawe ni msomi empty set nini?
Unaweza ukasoma sana,ndani na nje halafu usielinike! Ukaishia kukisanya vyeti tu,elimu hakuna!
 
Uhuru wake wa maoni afanye kwenye page yake binafsi ...sio kwenda kuongea vitu tofauti na misimamo ya Taasisi iliyokuajiri.....halafu ukifukuzwa kazi useme Uhuru wa kutoa maoni...
Ukifanya kazi media ambayo mmiliki wake ni Chadema ...maoni yako kupitia media hiyo lazima yaendane na misimamo rasmi ya hiyo media..

The same goes Kwa CCM, Cuf etc...

Hutaki Acha kazi ukaropoke popote kule
Ndugu kwani kosa la Hando ni lipi ?
 
Efm na tve ni biashara,na biashara haitakiwi kugombana na wanasiasa wenye mamlaka,hando Kama maoni yanamuwasha Sana alitakiwa ayatoe kweje kurasa zake au aanzishe media yake abwabwaje kutwa
Kwani kosa la Hando ni lipi ndugu ?
 
Hayo yote ya kuzuia maoni ya watu na watangazaji wote na wamiliki wa vyombo vya habari wamepewa agizo kudhibiti uhuru wa habari ...sababu kuu ya sa100 na kikweti kufanya hivyo ni hofu ya kifo cha JPM..Ndiyo maana sa100 na kikweti wamepiga marufuku hotuba zote za nyerere na magufuli kusikika redioni .....
Sa100 na mzee wa msoga ni maadui kamili wa uzalendo kwao uzalendo ni mafiiii[emoji90][emoji90] na hivi ndivyo ilivyo siku zote inapokuwa chini ya waisiharamu ikulu lazima wasujudie mabeberu ya magharibi
Hili la hotuba za Nyerere kuzuiwa sikulijua
 
Kwani kosa la Hando ni lipi ndugu ?
Nchi inakopa hovyohovyo....nchi haiwezi kopa bila rais kuridhia/agiza,kwa rais afuataye utaratibu hafanyi maamuzi peke yake Bali taasisi ya urais,kusema nchi inakopa hovyohovyo ni kusema serikali inafanya mambo/endesha nchi hovyohovyo...
 
Chezea asali wewe. Wenzako siku zote wanapigania ugali wao. Usije ukaona watu wanatoa povu humu ukadhani wana uchungu na Watanzania. Hata huyu mleta mada ipo siku atakushangaza.
Jamaa namuonaga bonge la kichwa!!!kumbe ...
 
Nchi inakopa hovyohovyo....nchi haiwezi kopa bila rais kuridhia/agiza,kwa rais afuataye utaratibu hafanyi maamuzi peke yake Bali taasisi ya urais,kusema nchi inakopa hovyohovyo ni kusema serikali inafanya mambo/endesha nchi hovyohovyo...
Kwa kuzingatia kipengele cha uhuru wa kutoa maoni kosa lake hapo ni lipi ?
 
Jamaa namuonaga bonge la kichwa!!!kumbe ...
Siyo mbele ya asali. 90% ya walimuchukia Mwendazake ni kutokana na kuwakatia mirija. Waliamua kujificha kwenye kichaka Cha demokrasia, lakini ni watu ambao hawajawwahi kujali kuhusu Hilo. After all ni lini nchi hii imewahi kuwa na demokrasia!
 
Kwa kuzingatia kipengele cha uhuru wa kutoa maoni kosa lake hapo ni lipi ?
Kama mwanahabari akitumia chombo Cha habari,ametoa taarifa Hasi dhidi ya serikali,taarifa zonazochochea chuki dhidi ya serikali na kuifanya serikali ionekane haijui inachofanya
 
Hando na wenzie wapelekwe shule wakasome na siyo kutegemea kufanya kazi kwa mazoea. Kwamba elimu ya Form IV na ujanja ujanja itakufanya uwe star news anchor siyo sawa.

Hamna namna Gerald anaweza kuongelea mambo ya mikopo, fedha na uwekezaji kama hana elimu ya kiwango cha Masters kwenye uchumi, fedha au biashara. Lazima uchomoe betri tu
Athari za mikopo kwa uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja haihitaji Masters kujua.
Msiwazibe wananchi midomo kwa kivuli cha elimu, kila mmoja ana haki ya kutoa maoni maana hiyo mikopo italipwa kwa kodi zetu.
 
Hewalaaaaa!!!
JamiiForums-627370351.jpg
 
Kama mwanahabari akitumia chombo Cha habari,ametoa taarifa Hasi dhidi ya serikali,taarifa zonazochochea chuki dhidi ya serikali na kuifanya serikali ionekane haijui inachofanya
Ki vipi Hando ame kitumia chombo cha habari ?.

Ni taarifa gani hasi alizo toa Hando ?.

Ni taarifa gani alizo toa Hando zinazo chochea chuki dhidi ya serikali ?.

Ni ki vipi alicho ongea Hando kina ifanya serikali ionekane haijui kitu ?.
 
Uhuru wake wa maoni afanye kwenye page yake binafsi ...sio kwenda kuongea vitu tofauti na misimamo ya Taasisi iliyokuajiri.....halafu ukifukuzwa kazi useme Uhuru wa kutoa maoni...
Ukifanya kazi media ambayo mmiliki wake ni Chadema ...maoni yako kupitia media hiyo lazima yaendane na misimamo rasmi ya hiyo media..

The same goes Kwa CCM, Cuf etc...

Hutaki Acha kazi ukaropoke popote kule
wajaribu kumfukuza awapeleke mahakaman wakaone kama hawajajuta wamfukuze sasa tuone au wanatishia kujamba.
 
Ki vipi Hando ame kitumia chombo cha habari ?.

Ni taarifa gani hasi alizo toa Hando ?.

Ni taarifa gani alizo toa Hando zinazo chochea chuki dhidi ya serikali ?.

Ni ki vipi alicho ongea Hando kina ifanya serikali ionekane haijui kitu ?.
Maswali yako yanaonesha hujui mjadala unahusu nini
 
Hajazuiwa kuandika chochote kwenye page yake wala kuchukua fomu kugombania nafasi yeyote kwenye chama chochote.... bado ana Uhuru mkubwa WA maoni na kushiriki siasa..

Asihusishe chombo ambacho muajiri wake hataki....mbona simple kabisa hii kueleweka?
Hakuna popote Hando aliposema anatoa yale maoni yake kama mfanyakazi wa EFM, alitoa maoni yake personally, na hii angeifanya popote iwe twitter au pengine..

Abovw all, kuna kampuni zinatengeneza robots, nendeni huko mkatengenezewe wafanyakazi muwa set vile mtakavyo, lakini kulazimisha mwanadamu mwenye upeo awe na tabia za robots ni ujinga.
 
Back
Top Bottom