"Eimeeenn!" ni neno ni la lugha gani?

"Eimeeenn!" ni neno ni la lugha gani?

Halafu wale wachungaji wanaowaweke watu mikono vichwani wananikera mno. Mchungaji mmoja alikuwa anamwombea demu wangu huku amemwekea mkono kichwani, Sasa demu akawa mgumu wa kuanguka mchunguaji akaamua kumtegea mguu Kwa mbele na kukishika kichwa Cha demu Kwa nguvu Kisha akamsukuma chuni. Demu alianguka mpaka mapaja yakaonekana.

Nilikasirika mpaka nikasonya kanisani.
Sasa nini kilichokuudhi zaidi hapa? Mapaja ya demu wako kuonekama au demu wako kuangushwa?
 
Na wanaojua kiingereza ndiyo wanawashika balaa. Unakuta mtu alizamiaga South au Ulaya zamani sasa kiingereza kipo kipo. Anaamua kurudi bongo na kufungua kanisa. Basi anahubiri kwa kiingereza na anakuwa na mtafsiri.
Hatari mno.
 
Haya makanisa yanayoota kama uyoga yanayojiita ya kiroho yana vituko achilia mbali hiyo miujiza feki. Eimeen ni neno la lugha gani? Siyo neno halisi katika lugha mama za biblia.
Mmh nadhani ni jamaica
 
Hatari mno.
Wapo wengi tu Arusha wana viredio vyao. Wizi mtupu. Nasema siku zote huyu Yesu wanayemhubiri kama siku moja angeamua kukagua makanisa yote hawa manabii na mitume na walimu wangekuwa wa kwanza kutorokea dirishani. Asalimia 99 ni majizi tu. Motivational speakers deceiving people in the name of religion!
 
Wewe mtanzania wa wapi hujui Amina? Hiyo amein ni mbwembwe za wale wanaongea kwa sauti za kukwaruza kwenye nyumba za ibada
 
Walokole wana mambo sana!

Kuna haya makanisa ya mitume na manabii... Haya huwaga siyaelewi aiseee! Mtu hasomi biblia, anasomewa na mtu mwingine ikifika muda wa kuombea akipuliza tu maiki watu wote wanaanguka! Huu si uchawi huu? Na kila mtu ana maji au mafuta yake anayoyauza kwa kisingizio cha kuleta mafanikio kwa watumiaji
Ukiwa na afya timamu ya akili huwezi kuanguka huko makanisani. Nimepita makanisa mengi mno nikasema acha nione. Akijaribu kunisukuma na mimi namsukuma aanguke yeye😆😆
 
Wewe mtanzania wa wapi hujui Amina? Hiyo amein ni mbwembwe za wale wanaongea kwa sauti za kukwaruza kwenye nyumba za ibada
Sina shida na Ameen au Eimeen yao. Nimeuliza ni lugha gani? That was my basic question. Hata AMINA ni lugha gani? Siyo Kiebrania wala Kigiriki wala Kiaramayo wala Kilatini.
 
Unachanganyikiwa na neno dogo sana ewe farisayo, mtoza ushuru na mtu wa mataifa. Eimeeen ni neno sawa na kusema amina, hiyo amina itamke kwa kiingereza ita sound vile
 
Wewe mtanzania wa wapi hujui Amina? Hiyo amein ni mbwembwe za wale wanaongea kwa sauti za kukwaruza kwenye nyumba za ibada
Sauti za kukwaruza wanajitakia wenyewe kwa upumbavu wa kukemea pepo kwa jina la Yesu mara hamsini. Jina la Yesu wa kweli linatajwa mara moja tu mambo yanakamilika. Huyo Yesu wao wa KWA JINA LA YESU mara kumi ishorini thelathini ni YESU WA UONGO. Matapeli tu hao. Soma Biblia hakuna mahali mitume wa Yesu walikuwa wanafanya miujiza kwa kulitaja jina la Yesu kipumbavu kama hawa wahubiri wa leo. Soma kitabu cha MATENDO YA MITUME ujionee mwenyewe Petro alipomponya kiwete pale kwenye MLANGO MZURI wa hekalu na Mtume Paulo alipomfufua kijana aliyekufa kwa kuanguka kutoka ghorofani na simulizi zingine. Kwa sasa ni matapeli tu wamejipatia mahali pa kujificha ambapo haguswi mtu. So sad!
 
Unachanganyikiwa na neno dogo sana ewe farisayo, mtoza ushuru na mtu wa mataifa. Eimeeen ni neno sawa na kusema amina, hiyo amina itamke kwa kiingereza ita sound vile
Basi tutafute neno la Kiswahili. Maana neno hilo la Kiebrania linamaanisha NA IWE HIVYO na kuna mahali hata kwenye sacraments fulani za walatoliki neno hilo halitumiki kwenye sacrament ya upatanisho maana haina HUMAN SANCTION
 
Unachanganyikiwa na neno dogo sana ewe farisayo, mtoza ushuru na mtu wa mataifa. Eimeeen ni neno sawa na kusema amina, hiyo amina itamke kwa kiingereza ita sound vile
Amen kwa matamshi ya kiingereza ni eimeen? Are you serious?
 
Unachanganyikiwa na neno dogo sana ewe farisayo, mtoza ushuru na mtu wa mataifa. Eimeeen ni neno sawa na kusema amina, hiyo amina itamke kwa kiingereza ita sound vile
FARISAYO, MTOZA USHURU
, MTU WA MATAIFA. Yaani hawa wote ni mtu mmoja?? Nimecheka kwa sauti kubwa. Jifunze biblia na historia ya ukristo na kanisa vizuri. Maana sasa hata sijui wewe umejiweka wapi hapo. According to the bible you are a GENTILE.
 
mbona povu sana ewe sadukayo?
 
Back
Top Bottom