Walitakiwa kudhibitiwa na polisi wana mbinu zao za kuwadhibiti watu kama hao na ndio maana wapo waliyokamatwa, sasa ukisema et kama wangeachwa nini kingetokea inakuwa kama vile kuuwa ndio kitu pekee ambacho polisi anaweza kufanya ili kudhibiti fujo kwa watu wasio na silaha ni kuwauwa tu kwamba kinyume na hivyo hakuna cha kufanya.
Ndio maana inakuja hoja ya kutumika nguvu kubwa na matokeo yake imesababisha madhara hadi kwa wasiohusika pia kwa sababu walichokuwa wanakifanya hakikuwa tena kudhibiti bali lilikuwa zoezi la mauwaji tu.