Elimu ni ufunguo wa Maisha, Diamond anamsomesha mtoto wake Braeburn International school, chekechea ada milioni 20

Na huu ndio ukweli usiopingika wa maisha: Usiwasomeshe watoto wako kuwa matajiri, wafundishe kumjua Mungu,Yeye atawapa utajiri. Kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Kwa njia hiyo pia watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.
Hayo ni mawazo ya kimasikini

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Kila mtu hujikuna anapojipata
 
Na huu ndio ukweli usiopingika wa maisha: Usiwasomeshe watoto wako kuwa matajiri, wafundishe kumjua Mungu,Yeye atawapa utajiri. Kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Kwa njia hiyo pia watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.
Mawazo ya kimasikini haya yanayohubiriwa na wachungaji wanaokusanya sadaka zenu kununulia V8 huku nyie waumini mpo hoi.

Maarifa ni muhimu na Mungu nae ni Muhimu
 
Mil 20 kwa Mwaka si pesa ndefu kwa huyo Jamaa, ila kwa Mimi kapuku.. aisee huo ni mkopo wa miaka 8 nakatwa kila mwezi mpk hela ya watu irudi..🀣

Diamond mbali sana

MC GARAB tu anaipata hiyo hela mwezi mmoja tu.

Mpuuzi kama Mwijaku anaipata hiyo hela ndani ya miezi mitatu tu.

Hiyo hela ni ndogo sana ukiwa unafanya kazi na watu wengi ama taasisi nyingi tofauti

Shida wengi tumejifunga na ajira zetu tunategemea mshahara wa mwajiri mmoja
 
Mkuu huko tuendako watoto wa hawa viongozi wa sasa ndo wanaenda kuwa viongozi wa hili taifa na kwa taarifa yako ni kuwa sio upinzani wala CCM ni kwamba vigogo wote wanasomesha watoto hizi shule kali. Kama huamini fuatilia UVCCM ya sasa viongozi wake ni kina nani... tayari wa kishua Jokate ni boss UWT. Mbowe nae anamrithisha chama mwanae aitwae James ambaye kasoma Nje. Acha hizo fikra zilizopitwa na wakati
 
Sio kwamba Fikra zimepitwa na wakati... hilo la vigogo kusomesha shule kali watoto wao nalijua pia.

Hunielewi na huwezi kunielewa na hautanielewa. Nchi kuongozwa na kiongozi wa aina fulani kunataka protokali mzee ambazo katu hutakaa ukazijua wewe mwananchi wa kawaida.

Tuombeane uhai uone kama nchi itakujwa kuongozwa na waliosoma IST na Braeburn... unafkiri sisi ni mazwazwa sana? πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Wataishia hukohuko ilipopataja, kuwa Rais kuna nidhamu zake bwamdogo. Huwezi katu kuyajua hayo mpaka uwe kwenye game
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…