Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,294
- 10,970
- Thread starter
- #241
Kuna makumi ya mabilioni yetu tunayafuatilia taratibu kule Apollo Hospital India nyie jishaueni tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa wa kristo wote duniani kipindi cha kwaresma ni kipindi cha toba ambacho watu hukitumia kujirudi kwa muumba wao kwa kuomba na kusamehewa zambi zao.
Si sawa kwenye kipindi cha kwaresma kusema uongo waziwazi na kujilizaliza ili uonekane kwamba unaonewa na kuteseka sana kuliko binadamu wote hapa duniani!
Ndugu yetu huyu Tundu Lisu amekuwa mtu wa kusema uongo na kuzushia wengine mabaya ili waonekane ni wachafu mbele ya jamii, mfano kwa miaka nane alizunguka kote nchini na duniani akimtaja Lowasa kuwa ni fisadi namba moja duniani! Lakini baada ya Lowasa kuinunua chadema na kuwa mgombea urais , ni Lisu huyohuyo tena alizunguka nchi nzima akiwaambia watu kuwa Lowasa siyo fisadi na anafaa kuwa rais wa Tanzania!
Tabia mbaya hii Tundu Lisu aneendelea nayo hata baada ya kupigwa risasi zaidi ya 38, kwanza aliwaahidi wa Tanzania kwamba akipona tu atarudi nyumbani mpaka leo hajafanya hivyo maana yake alisema uongo. Pili ndani ya mwezi huu wa toba Tundu Lisu amelifurumshia uongo na uzushi bunge kwamba hajalipwa madai yake huku akijua si kweli!
Jana Spika Ndugai ameonyesha hadharani nyaraka zote zinazoonyesha Tundu Lisu amelipwa zaidi ya milioni 500 na bunge! ,tena amelipwa hela zingine za kutembelea wapiga kura wakati hajawahi kufanya hivyo! Hapo bado hujaweka mamilioni mengine aliyochangiwa na wana chadema.!
Tunakuambia tu Lisu huku kudeka na kulialia siyo kwa hali ya kawaida huenda una tatizo la malezi mahali na tunakuonya pia ipo siku wanyonge watataka kurudishiwa hela zao ulizolipwa bila kuzifanyia kazi.
Sent using Jamii Forums mobile app