SoC04 Elimu ya shule ya msingi bure, tuition ya kulipia ya lazima kwa wanafunzi wote!

SoC04 Elimu ya shule ya msingi bure, tuition ya kulipia ya lazima kwa wanafunzi wote!

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Sep 9, 2022
Posts
5
Reaction score
3
Katika sekta ya elimu naipongeza serikali kwa uamuzi wa kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote waliofikisha umri wa kuanza shule.

Nawapongeza pia walimu katika utendaji kazi wao wa kutoa elimu kwa watoto wetu wote.

Katika hili kuna changamoto kidogo ya matokeo katika mitihani ya shule mpaka kitaifa kwa kiukweli shule nyingi za uma asilimia kubwa zimekuwa zikiburuzwa na shule nyingi za private zimeonekana kuwa na matokeo mazuri. Hii ni kivipi?

Ukiangalia shule nyingi za privae ukiacha mzazi kulipa ada kubwa lakini wamekuwa na utaratibu wa walimu kuwa karibu na wanafunzi kwa kuwafuatilia kila hatua katika masomo yao na hii ni kutokana na uchache wa idadi ya wanafunzi....tukirudi kwenye shule za umma wanafunzi wamekuwa ni wenzi lakini pia hakuna ule ufuatiliaji (ukaribu)baina ya mwanafunzi na mwalimu.

Mzazi analipa pesa nyingi katika shule binafsi hivyo moja kwa moja anasikia uchungu kwenye elimu ya mtoto wake hali inayopelekea pia kuwa na uwiano baina ya mwalimu ,mzazi mwanafunzi. Lakini shule za umma hali ni tofauti kwa asilimia nykubwa ya wazazi, hawana ukaribu na mtoto wala mwalimu na hii ni ukifuatilia hata vikao vingi vya wazazi shuleni wengi huwa hawauzurii, hii inamfanya mtoto kutokuwa na mkazo katika masomo yake hasa ukizingatia shule nyingi bado zimeelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi ambapo kutokana hii changamoto likaanzishwa suala la tuisheni mashuleni.

Kiukweli suala la tuisheni ni jema kwani sio kila mtoto anaweza kudaka material kwa muda ambao anakuwa darasani kiujumla, lakini suala hili ningependa liboreshwe kwani sio wote wanaosoma tuisheni na labda ni kwa mapuuza yetu sisi wazazi...Hii pia inapelekea kuonekana kama ni mchongo kwani imani yangu inasema kuna kauzembe kwa mwalimu kutofundisha ipasavyo darasani akitegemea mwanafunzi asielewe ili aje amfundishe baadae kwenye tuishen yake ambayo mzazi huwa analipia...

Ningependa kuishauri serikari,ifanye maboresho suala la tuisheni katika shule za msingi liwe la lazima ambapo mzazi atatakiwa achangia kiasi kadhaa kwa mwaka mzima hii inaweza kuiinua sekta ya elimu katika shule za umma kwa asilimia fulani.


Nawasilisha.
 
Upvote 2
Mzazi analipa pesa nyingi katika shule binafsi hivyo moja kwa moja anasikia uchungu kwenye elimu ya mtoto wake hali inayopelekea pia kuwa na uwiano baina ya mwalimu ,mzazi mwanafunzi. Lakini shule za umma hali ni tofauti kwa asilimia nykubwa ya wazazi, hawana ukaribu na mtoto wala mwalimu na hii ni ukifuatilia hata vikao vingi vya wazazi shuleni wengi huwa hawauzurii,
Pesa muda mwingine inaongeza thamani ya kitu. Ukiiondoa kabisa unaondoa na umakini. Nadhani ndicho kilichotokea kwenye elimu bure.

Ningependa kuishauri serikari,ifanye maboresho suala la tuisheni katika shule za msingi liwe la lazima ambapo mzazi atatakiwa achangia kiasi kadhaa kwa mwaka mzima hii inaweza kuiinua sekta ya elimu katika shule za umma kwa asilimia fulani.
Mmmmmmh! Kwa nini isibakie hiyari mtu anayeona faida yake ndiyo alipie
 
Pesa muda mwingine inaongeza thamani ya kitu. Ukiiondoa wkabisa unaondoa na umakini. Nadhani ndicho q kwenye elimu bure.


Mmmmmmh! Kwa nini isibakie hiyari mtu anayeona faida yake ndiyo alipie
Watu wengi wanalichukulia kwa wepesi hili suala hasa huku kwetu kitaa, hawajali kabisa....ni bora pesa ya tuisheni itolewe mtoto akitoka kwenye masomo yake ya darasani moja kwa moja anaingia tuisheni.
 
Back
Top Bottom