Elizabeth, kabla ya kifo chako uliwahi kuwaomba msamaha watu weusi?

Elizabeth, kabla ya kifo chako uliwahi kuwaomba msamaha watu weusi?

hapa hatumsemi marehemu ila kuna msemo unasem UKINYA UNUKE usitegemee kupewa sifa wakati umefanya mabaya..m
Mimi ni Pan-Africanist ila hata kuonyesha mabaya wakati tayari ni marehemu ni useless.

How long will Africans continue being inferior?

Hata hapa bongo kuna watu kipindi JPM yupo hai walifyata mikia mfano:Nape ila JPM alipokufa wakaanza kuropoka wakiyaita mabaya.

Hizi hoja zenu ni useless na zipo chini ya kivuli cha uoga.Kwa nini hukuyasema haya kipindi yupo hai?

Every wise African knows how the mabeberu were and are discriminative, exploitative and brutal to Africans.

All in all dark skin has got its negativity as well as white skin!
 
Mimi ni Pan-Africanist ila hata kuonyesha mabaya wakati tayari ni marehemu ni useless.

How long will Africans continue being inferior?

Hata hapa bongo kuna watu kipindi JPM yupo hai walifyata mikia mfano:Nape ila JPM alipokufa wakaanza kuropoka wakiyaita mabaya.

Hizi hoja zenu ni useless na zipo chini ya kivuli cha uoga.Kwa nini hukuyasema haya kipindi yupo hai?

Every wise African knows how the mabeberu were and are discriminative, exploitative and brutal to Africans.

All in all dark skin has got its negativity as well as white skin!
not useless gee... bado wapo ai na wao wanajukum km marekan anavyolip kwa aliyofanya iloshima
 
not useless gee... bado wapo ai na wao wanajukum km marekan anavyolip kwa aliyofanya ilosoma
White people's aids have contributed nothing to ustawi wa nchi za kiafrika.

Mfano rahisi:Tangu nchi nyingi za kiafrika zianze kupewa mikopo ndiyo exploitation ya rasilimali za taifa za Afrika zinaibiwa.

Swali:Tatizo ni nini?
Jibu:Tatizo ni waafrika wenyewe(wanapokuwa viongozi) pamoja na wazungu.
 
White people's aids have contributed nothing to ustawi wa nchi za kiafrika.

Mfano rahisi:Tangu nchi nyingi za kiafrika zianze kupewa mikopo ndiyo exploitation ya rasilimali za taifa za Afrika zinaibiwa.

Swali:Tatizo ni nini?
Jibu:Tatizo ni waafrika wenyewe(wanapokuwa viongozi) pamoja na wazungu.
tukiwalaumu viongozi wetu kutufikisha hapa tulipo . sio lesson et tusiwalaumu white peoples....

viongozi wanatufelisha ila white peoples walitufelisha
 
Japo kwa cheo QUEEN ELIZABETH wewe ulikuwa malkia kwa maana kiongozi hakosei.

ila kwa upande wengine tukitoa cheo chako wewe Elizabeth Alexandra Mary Windsor ulikuwa ni binadamu kama binadamu wengine.

na japo kosa haukulifanya wewe walifanya watu wengine ila ungetudanganya basi hata kwa neno samahani tu.

Maana mtoto anapokesea nje na kwao watu aanza kuuliza yule ni mtoto wa nani na sio yule ni nani

Habari zenu wapendwa pia poleni na msiba wa kiongozi wenu. ila bado tunawakumbusha tunawadai na tutaendelea kuwadai


ili lipo wazi kabisa japo kuwa hadhani masikio yenu hayataki kusikia aya maneno (Ukweli ambao hatumatiki kuisikia).

Ukisiliza nyimbo ya Bob Marley " Buffalo soldiers" basi kuna vitu vingi sana utajifunza .

kuna mstari unasema

"If you know your history
Then you would know where you coming from "

kwa maana ya uo mstari kinyume chake kama haujui unatoka wapi basi pia hauwezi kujua historia yako.


Kauli ya kiongozi wa kambi ya upinzani Africa kusini Bwana Julius Malema naomba usitafsiriwe kama chuki au hajielewi ni kauli safi kabisa.

ila kama unatumia hisia kwenye tukio linalotakiwa kutumia akili hauwezi kumuelewa Julius malema.

"We do not mourn the death of Elizabeth, because to us her death is a reminder of a very tragic period in this country and Africa's history.... If there is really life and justice after death, may Elizabeth and her ancestors get what they deserve."

Hii kauli unaweza kusema imebeba chuki kwa watu weupe ila hiyo kauli haijatoka kwa mtu ambae ajielewi. nadhani julius malema alikuwa anajua anasema nini na pia anaijua historia ya afrika juu ya waingereza.

Turudi kwenye historia karne ya 17.

Mwaka 1619 meli ya kwanza ilifika katika katika Amerika ( Virginia) na ilikuwa na waafrika ambao walikamatwa na maalamia wa kiingereza kutoka pwani ya Mexico . waafrika ao walikuwa wametoka kwenye meli ya watumwa iliyokuwa inamilikiwa na Wareno.

Meli hiyo ilikuwa imebeba waafrika 350 kama watumwa sio abiria . ambao walitokea Angola na wengi wao walikuwa wamekufa njiani kutokea ndani ndani na hata wengine walikufa ndani ya meli wakiwa safarini miili yao ilitupwa baharini.

walikufa kutokana na mazingira magumu na waliobaki hai walienda kuuzwa huko Amerika na ulaya ya Magharibi. Waafrika ao walitumika kama wafanyakazi wa ndani wengine walipelekwa mashambani.

hizi safari za watumwa zilianza karne ya 16 hadi 19 . na zilikuwa safari za kulazimishwa hakukuwa na muafrika hata moja aliyetaka kwenda ulaya na amerika kufanyishwa kazi bila malipo na kuwekwa mazingira kama mnyama.

Ambapo biashara hiyo alichukua takribani watu Million 12 wakiwemo Wanaume , wanawake na watoto


Lakini mnamo karne ya 17 .

Ndani ya ulaya inazaliwa sera ya Mapinduzi ya kilimo ( Agriculture revolution ). ni bidhaa ghali zaidi inajulikana ni sukari.

na sukari kwa karne hiyo ndo ilikuwa bidhaa yenye thamani zaidi ulaya .

Muingereza anagundua ardhi nzuri yenye kutoa miwa mizuri ni ile ya pale caribbean. lakini binadamu wenye rangi nyeupe inakuwa ngumu kuishi mda mrefu kutokana na mazingira.

Wanachukuliwa watu weusi wanaenda kulimishwa miwa ndani ya caribbean ambapo msanii maarufu wa kike duniani Rihanna alipozaliwa.

mtu mweusi ( mtumwa) . anaenda kulimishwa sehemu ambayo kiufupi yeye hana maslahi napo anayeenda kufaidika ni muingereza.

Sina mahana mbaya na wala musitoe tafsiri mbaya . mnufaika namba moja wa kilimo cha caribbean ilikuwa ni Familia ya Kifalme ya pale nchini uingereza.

Kwa kipindi hiko life expectancy ya binadamu walikuwa wanaishi hapo ilikuwa ni miaka 18 tu sasa vuta picha leo hii Tanzania life expectancy yetu ni miaka 66. 08 ( 2022) kwa report ya World bank

hayo tufanye hayapo ni ya miaka mingi sana yamepita

Twende 1915- 1918

Zaidi ya Wamarekani weusi 380,000 walihudumu katika Jeshi wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Wanajeshi Waafrika milioni mbili waliuawa

katika vita ya pili ya dunia pia 1939-1945

bahati mbaya Waafrika wamekuwa hawatajwi sana katika historia rasmi za vita ya pili ya dunia .

ingawa wengi walilipwa, wengi wamesahaulika kabisa.

wanajeshi 15,000 wa Kiafrika walipoteza maisha yao wakipigania Uingereza.

15, 000 ndio waliokufa . je unaweza kujiuliza ni wangapi walirudi na ulemavu

Na je vita hiyo inawahusu nini waafrika wakati vita ilikuwa ni ya watu weupe kwa weupe.

Wanajeshi wao walipigana vita wanawatunza na kuwapa mahitaji mazuri .

ila wazee wetu ambao walipigana vita kwa faida zao wapo na wengine washakufa hakuna walichofaidika nacho zaidi ya kulalamika tu na kutupa historia ambazo kiufupi hatuna faida nazo yoyote.

Sasa ni mda wa uingereza kuiomba samahani afrika kwa yote waliyoyafanya au musituombe samahani tuendelee kuwapa lawama na musituone wabaya mukae kimya.

Kama hipo video inayomuonesha kiongozi wa ulaya akiiomba samahani Afrika naomba munitumie

na kama haipo basi Samahani iusike mara moja sio samahani ya maneno na vitendo vionekane.

Leo hii julius Malema kauli yake imetoka baada ya kujijua yeye ni nani ila wanaompinga julius Malema ni wale ambao hawajui historia yao.

Sio weusi tu, hata waarabu n.k, refer kilichotokea iraq
 
Laiti huu mjadala ungeletwa wakati huyo malkia wao yu hai,ningetoa mchango wa kimawazo nikiwa kama Pan-Africanist.

Ameshakufa,kumuongelea kwa kumuhukumu ni kama kutaka kukausha bahari,haileti mabadiliko.

Laiti angelikuwa hai...ningeshusha NONDO.
Au co
 
Wewe ndiyo PIMBI..
Mimi ni pimbi but at least naijali asili yangu na najitambua.

Wewe unaejiona mjanja kujipendekeza kwa hao ngozi nyeupe jua wao wanakuona nyani tu,kwa maneno mengine wakipita sehemu wakakukuta wewe na ngozi yako ya mkaa pembeni yako pana mbwa na paka mmejificha mvua chini ya mti watasaidia hao wanyama wakuache hapo zikikukaa vizuri kichwani.
 
Dunia haiko fair.
Binafsi nadhani ni mihemko kumwaga chuki mtandaoni dhidi ya bidada Eliza.

Waafrica tumenyanyasana sana baada ya utawala wa hawa watu kiasi sioni tofauti yoyote.

Hebu tuombane misamaha sisi kwa sisi halafu baada ya hapo tudai misamaha kutoka ughaibuni.


Aibu zetu.
 
Back
Top Bottom