Aisee nashindwa hata nianzeje kumwelekeza. Ilibidi nicheke kuona jamaa anasema Elon ana deal na spice (Mawazo yakaja ya mdalasini, giligilani etc) wakati mshua anadili na roketi, magari ya umeme etc.Hahahah usimcheke bana muelekeze
Elon Musk ni level ingine. Alisoma shahada ya Economics na Physics, na alipoenda kufanya PhD, alijongo baada ya siku 2 tu chuoni, akaenda kufungua biashara.
Kampuni yake (SpaceX) ni kampuni ya kwanza private duniani kumpeleka mwanadamu kwenye space. Ameondoa monopoly ya Urusi waliokuwa nayo kwa miaka 9 baada ya program ya space shuttle kufika ukingoni. Nakumbuka test ya kwanza ya roketi yake alipeleka gari yake ya Tesla angani na mpaka sasa ipo anga za juu.
Yapo mengi kuhusu Elon na SpaceX ambayo waweza kuyaona youtube.