Kinamchompandisha utajiri ni hisa za kampuni zake. SpaceX ina tests mbili zijazo na so far wanafanya vizuri kwenye test zilizopita. Wanataka kuwa na reusable rockets hivo wana support kubwa ya NASA, wanunuaji wa hisa wakiona kampuni ina support kubwa ya NASA na ni leading kwenye teknolojia wanamwaga sana pesa kwenye kampuni hivo mwenye asilimia za hisa anazidi kuwa na pesa nyingi.
Tesla imeuza magari karibia laki 5 kama ilivopanga, hii imewapa imani wawekezaji kuwa kampuni ina mipango inatekelezeka hivo wanaongeza fedha na hawauzi hisa zao. Tesla imeuza magari machache lakini ndio kiongozi kwenye magari ya umeme ambayo ndio yatakuja tumika mbeleni. Kwanza ina mpango wa kujaza vituo vya kuchaji kila nchi ya Ulaya, China na US. Kwa nini mtu asiwekeze huku? Wachache watawekeza Coca cola wakati haina invention yoyote ya maisha.
Ana mpango wa kufanya utalii na kuchimba madini kwenye sayari ya Mars. Tiyari hao NASA wanajua madini yapo na shughuli zake atapinzana na kampuni flani ya Jeff Bezos. Hili soko ushindani hakuna, pesa za nje nje.
Neuralink yake inataka kufanya mageuzi kwenye artificial intelligence na ina mwanzo mzuri ingawa haina breaking news na ina staff ndogo tu.
The Boring Company wanataka wagundue teknolojia ya nishati mbadala wa lithium kwenye kuhifadhi charge. Ulimwengu ujao utatumia umeme na betri zinabidi zitengenezwe kwa gharama ndogo, ziwe bora, zidumu, performance kubwa. Yani maana yake wanataka kugundua mbadala wa Lithium, ambayo ni mbadala wa mafuta. Sasa kwa nini wasiwe na hela wakifanikiwa. Wawekezaji wataweka hela tu
Kwa vile yeye ndio anaanzisha makampuni yote haya anakuwa na hisa zake nyingi mfano pale Tesla ana 20%. Kama Jeff Bezos ana 10% kwenye Amazon, Tesla mwenye makampuni kibao akiunganisha thamani zote anakuwa na hela nyingi.