Jaribu na wewe kama ni rahisi..
Wewe usiite wenzako washabiki maandazi...
Narudia kusema tena hakuna tajiri mpuuzi na mjinga atakimbia kwenda kuwekeza mamilioni ya dola kama hisa kwa kusikiliza story za mtu..
Au hedge fund, ama bank ikanunue hisa kwq kukurupuka, watu walinunua hisa baada ya kuona matokeo, Tesla ilileta mapinduzi makubwa kwenye gari za umeme, SpaceX ilileta mapinduzi kwenye usafirishaji wa anga... hakuna ujanja ujanja na utapeli...
Banks, hedge funds ama mashirika hawanunui hisa kwa kukurupuka, wana timu za wataalamu wa fedha, wachambuzi wa data, na wanasayansi wanaochambua mizania ya kampuni, wanaelewa mauzo ya kampuni na faida n.k...
Wabongo bana, kirahisi tu, eti utajiri wake ni kwa sababu ya ku manipulate market.. ka manipulate na wewe...
Unafikiri aliamka asubuhi akaenda ku manipulate masoko ya hisa akawa bilionea?
Ukiona mtu amefikia hatua anazungumza na sekta ya fedha inatikisika inabidi umuheshimu, hakufika hapo kirahisi..