Marcostilone
JF-Expert Member
- Jun 25, 2023
- 7,018
- 17,932
Binti kwenye ubora wako, mijadala kama hii wewe kuwa msomaji tu, maana imevuka upeo wako wa kufikiri.Oyaa huyo jamaa utajisumbua tuu
Ni hanaga hoja kabisa.. Tena siku hizi ndo amelijua hilo
Binti kwenye ubora wako, mijadala kama hii wewe kuwa msomaji tu, maana imevuka upeo wako wa kufikiri.Oyaa huyo jamaa utajisumbua tuu
Ni hanaga hoja kabisa.. Tena siku hizi ndo amelijua hilo
Boya niniBinti kwenye ubora wako, mijadala kama hii wewe kuwa msomaji tu, maana imevuka upeo wako wa kufikiri.
Tulia binti, jenga hoja kwa utulivu ueleweke.Boya nini
Wewe uko chini sana mentally,
Elon nimemfatilia sana,
Wewe umekaa kunakiri vitu sivyo na uelewa navyo unakuja kubishana na wataalam?
Bora umesha jua where you belong.
Anawapiga watu kamba ili stocks zipande apige ela. Ana ahadi nyingi ambazo hazijatekelezeka. Alianza na Mars na alisema kufikia nadhani 2025 binadamua atakuwa ashaweka makazi now naona kaachana napo. Mpaka sasa rocket yake ambayo inapaswa kuwa ndiyo inasaforisha watu na mizigo hazijawa tayari kila test linaibuka tatizo.Hivi karibuni, Elon Musk alitangaza mpango wa kujenga mji kwenye Mwezi; alisema kuwa mpango huo unaweza kutekelezwa ndani ya muda usiozidi muongo mmoja na kwamba mji huo utakuwa na uwezo wa kukua na kuendelea kwa kujitegemea.
Elon Musk alisema kuwa badala ya kujikita katika ujenzi wa mji kwenye sayari ya Mirihi (Mars), kampuni ya SpaceX sasa inaelekeza nguvu zake katika kujenga mji kwenye Mwezi.
============================
Recently, Elon Musk announced that SpaceX has shifted its focus toward building a self-growing city on the Moon, saying the ambitious project could potentially be achieved in less than a decade.
Musk said that, rather than focusing primarily on building a city on Mars, SpaceX is now prioritizing the Moon because it is much closer and can be reached more frequently. He argued that missions to the Moon can be launched far more often than missions to Mars, making lunar development faster to advance.
However, Musk has not completely abandoned his long-term plans for Mars. He said SpaceX still intends to begin work toward building a city on Mars within about five to seven years, but the Moon has become the company’s immediate priority.
The announcement represents a significant change from Musk’s previous position, in which he had described Mars as the main destination for establishing a permanent human settlement beyond Earth.
View attachment 3653168
Halafu boya ni huyo baba ako unayemuanzishia uzi kila siku, half witted bastard!Boya nini
Wewe uko chini sana mentally,
Elon nimemfatilia sana,
Wewe umekaa kunakiri vitu sivyo na uelewa navyo unakuja kubishana na wataalam?
Bora umesha jua where you belong.
Atanufaika nini akijenga kwenu?Wataalamu wetu wa uchumi hapa tz mnashindwa kumshawishi uyo jamaa kuja kuje uku kwetu badala kwenda kupoteza pesa uko kusipojulikana?
Utatoa mapovu na kuichachafya bipolar mpaka uchoke.. Issue ni kuwa ulikua na moto sasa umeenda unako belong (dumbness) ... Huna maarifa, huna influence, huna kitu... Yaani unakesha jf bure ni heri urudi kijijini ukaendelee kumsaidia mashamba ng'ombe weweHalafu boya ni huyo baba ako unayemuanzishia uzi kila siku, half witted bastard!
Sawa binti.Utatoa mapovu na kuichachafya bipolar mpaka uchoke.. Issue ni kuwa ulikua na moto sasa umeenda unako belong (dumbness) ... Huna maarifa, huna influence, huna kitu... Yaani unakesha jf bure ni heri urudi kijijini ukaendelee kumsaidia mashamba ng'ombe wewe
Nilitegemea labda ungeniambia gharama za kujenga mji mwezini ni kiasi hiki, na anaweza kuzimudu hivi.Ndio anaweza kwa sababu ana rasilimali ana teknolojia ana mtaji na ana taasisi zilizothibitishwa ambazo zinaweza kufanya mradi huo ufanikiwe..
NASA shirika ambalo lina wataalamu na wanasayansi wakubwa zaidi duniani kwenye masuala ya anga wamemuamini na kuingia nae mkataba wa dola bilioni 2.9 kutengeneza chombo kiitwacho Starship HLS ambacho kitaweza kupeleka wanasayansi wa NASA mwezini kupitia program wanayoita Artemis..
Kama wanasayansi wa NASA wameridhika na uwezo wa SpaceX kwa kushirikiana na kutengeneza chombo cha kwenda mwezini hilo si suala dogo ni uthibitisho kwamba SpaceX wanaweza...
SpaceX wana Starship, hakuna nchi duniani wala kampuni wanamiliki Starship kama waliyonayo SpaceX, ina nguvu na inabeba waru na tani hadi 150 za mzigo na kuupeleka kwenye orbit ya dunia.. ndio rocket kubwa zaidi na yenye nguvu zaidi kuwahi kutengenezwa kwenye historia ya mwanadamu..
Starship hio inakwenda angani na kurudi..
Hivyo ikitokea wanajenga mji, hizo Starships ndizo zitakuwa zinapeleka vifaa huko mwezini..
SpaceX wana miradi mingine kama starlink Internet na hurusha satellites za nchi nyingine au satellite za kijeshi na kulipwa ambapo wanaingiza pesa ambazo zitawasaidia kuendesha mradi huo wa kwenda mwezini , ina maana hawategemei tu fedha kutoka serikalini.. ina maana wana cash flow.. hii inasaidia wazidi kufanya R&D pasipo kufilisika..
Kingine historia inaonyesha Musk ameshafanya mambo ambayo wengi waliona hayawezekani, mfano katikati ya miaka ya 2000s watu walidai haiwezekani kupeleka rocket angani na ikarudi imesimama wima na ikatua.. Musk alipambana na likawezekana hilo..
Pia kwenye magari ya EV, mwanzoni watu walisema gari za umeme zisingeweza kupambana sokoni na gari zinazotumia mafuta, ni kama watu hawakuamini uwezo wa gari za umeme, tazama leo baada ya Tesla kuleta mapinduzi kwenye EVs kila mmoja sasa anazungumzia gari za umeme... gari za umeme sasa imekuwa kawaida kutumika kila siku...
Hivyo track record inaonyesha Musk alisha zungumza ideas baadhi na kubezwa na akazifanya zikafanikiwa hivyo nina uhakika hata hili la mwezini atafanikiwa tu.. maana tayari ana taasisi yenye wanasayansi na wataalamu wanaoshirikiana...
Hufahamu kwamba Musk ndiye alikuwa risk taker? Mwaka 2008 kampuni ilitaka hadi kufilisika..Kwanza unajua kuwa waanzilishi wa Tesla, Martin Eberhard na Marc Tarpenning, wamewahi kumfungulia kesi mahakamani kwa kutaka kujimilikisha sifa asizostahili? Unalijua hili?
Nitajie mhandisi yeyote mkubwa wa roketi au magari aliyewahi kufanya kazi chini ya Musk ambaye amewahi kukubali kuwa Musk ndio anayegundua hizo teknolojia.
Nikisema unaandika kishabiki unatakiwa uelewe, haya maelezo yote hapa haujajibu kile nilichotaka kufahamu, unazunguka zunguka tu.Hufahamu kwamba Musk ndiye alikuwa risk taker? Mwaka 2008 kampuni ilitaka hadi kufilisika..
Unaelewa kwamba engineer anapoajiriwa mshahara wake analipwa kama kawaida, kampuni iingize faida ama hasara yeye mshahara wake upo pale pale.. na hata kampuni ikifilisika Engineer anaweza kuhamia kampuni nyingine..
Kingine Musk ndiye chief engineer na designer naielewa rocket, hilo hata wahandisi anafanya nao kazi wamethibitisha... uaifikiri ni mtu wa kukaa ofisini na kuhesabu fedha.. jamaa yupo vizuri kwenye rocket science...
Musk anafanya pia maamuzi ya kiufundi... kuna kipindi walitaka kutengeneza Starship kwa carbon fiber Musk akawakataza na kuwaambia watumie chuma cha pua...
Bmw, Ford, General motors n.k kabla ya Tesla kuwa serious na EVs kampuni nyingi za magari waliona gari za umeme hazina faida , kabla ya spaceX kutengeneza rocket zinazorudi duniani zikiwa wima, engineers na watu wengine walisema haitawezekana...
Kumbuka hiko kipindi engineers walikuwepo, wataalamu walikuwepo, alikosekana tu kiongozi mwenye maono ambae anngewekeza kwao na kuwaambia washirikiane kutengeneza gari ya umeme ya kiwango na rocket itakayoweza kutua ikiwa wima...
Bila maono ya Musk, ku take risk hao engineers wangekuwa kampuni zingine wakifanya kazi za kawaida.. Musk ndiye mbeba maono...
Nijifunze swali lako mhandisi mkuu wa injini za rocket kwenye SpaceX, Tom Mueller alisema Musk ana uelewa wa ndani sana kuhusu rockets na jinsi zinavyofanya kazi, Musk huwa anashirikiana na engineers wengine wakifanya mahesabu magumu ya sayansi ya rockets...
Sio engineer mmoja tu aliyeshtushwa na uwezo wa Musk...
Musk anasoma vitabu sana, na ana passion na interest na anachokifanya.. ndio maana imetokea akawa na uelewa mkubwa wa masuala ya rockets...
Huu ukweli hataki kuukubali, lakini ndio uhalisia wake, jamaa ni muumini tu wa Musk, anatoa hoja za kishabiki sana kuliko uhalisia wa jambo lenyewe.Bandiko lako linaonesha wewe ni muumini wa Musk zaidi ya mtu anayeangakia data, yani uneanza kwa imani kabla hujajua changamoto zikoje.
Dah umenisikitisha sana kumfananisha genius na mawinga wa kkoo akina barakaMusk nae ni Tapeli km mawinga was kariakoo, mxxxiiieeew.
Wewe ndiye ulipaswa kuuliza hayo maswali, maana hata swali lako lilikuwa general sana...Nilitegemea labda ungeniambia gharama za kujenga mji mwezini ni kiasi hiki, na anaweza kuzimudu hivi.
Nilitegema ungeniambia changamoto za kujenga mji mwezini ni hizi, na atazimudu hivi.
Nilitegemea utaniambia gharama hizi za kujenga huo mji mwezini atazirudisha hivi.
Nilitegemea unioneshe necessity ya huo mji, kwa nini unahitajika. Kwamba hii si a white elephant vanity project tu ambayo inajitengenezea tatizo na kulitatua bila ya hilo tati,o kuwapo kiukweli.
Sasa hivi, ukiondoa hoja ya kwamba watu wanahitaji kuwa na sehemu nyingine ya kuishi ili kitu kibaya kikitokea duniani, kikasababisha "extinction level event" ya kuua watu wote duniani, maisha yaendelee huko nje ya dunia, ukiiondoa dhana hiyo, hakuna point ya kujenga mji mwezini. Labda kujenga base ya scientific research, kitu ambacho hakihitaji mji wa watu wa kawaida kuishi.
Idea ya kujenga mji wa watu kuishi mwezini haina mashiko kwa sababu hapa duniani sehemu za kuishi hazijaisha, pia kwa sababu ni gharama sana.
Unapotaja dola bilioni 2.9 katika hesabu za kujenga nyumba mwezini inaonesha hujaelewa gharama zinazohusika hapa, hujaelewa suala la Return on Investment, hujajua gharama za kumsafirisha mtu mmoja tu kutoka duniani mpaka mwezini, achilia mbali kum support huko, kuweka mifumo ya hewa, chakula, kazi, ecosystems zote.
Hujajua changamoto za kisaikolojia, za kukabili radiation. Changamoto za meteorites, changamoto za kukosa hewa. Changamoto za vumbi la glass mwezini. Changamoto za joto na baridi kali. Changamoto za gravity na biology yetu. Changamoto za supply chain.
Unapofananisha suala la magari ya umeme na kujenga mji mwezini nakucheka kwa kuwa huelwi somo la awali kabisa la kulinganisha vigu. Ukitaka kulinganisha vitu, chagua vitu vinavyofanana. Magari ya umeme ya hapa duniani na kujenga mji mwezini ni changamoto mbili tofauti kabisa.
Kama Elon Musk ana uwezo huo, hujauelezea kwa detail hapa.
Umeuelezea kama muumini wa dini anayeamini mambo bila uhakiki.
Bandiko lako linaonesha wewe ni muumini wa Musk zaidi ya mtu anayeangakia data, yani uneanza kwa imani kabla hujajua changamoto zikoje.
Ndiyo maana umeshindwa hata kuzitaja changamoto umeenda moja kwa moja kuonesha una imani na Elon Musk.
Una imani na Elon Musk kwenye kukabiki changamoto gani?
Wewe ndiye ulipaswa kuuliza hayo maswali, maana hata swali lako lilikuwa general sana...
Dola bilioni 2.9 wanayotoa NASA kwa SpaceX ni kwa ajili ya kutengeneza Starship HLS.. sio kujenga majengo mwezini...
Kuhusu suala la mionzi, vumbi la mwezi na baridi kali mwezini, wanasayansi wamegundua mwezini kuna mapango ya kivolkano ambayo yapo ndani ya ardhi, si juu ya ardhi, hivyo watajenga hio miji huko kwenye mapango kuepuka baridi, mionzi na vumbi huko mwezini..
Mwezini huko watajenga gas station , kwa kutumia barafu iliyopo mwezini watazalisha oxygen na hydrogen ambapo hydrogen itatumika kama fuel kwenye rocket, kwa mwezi kuwa kama gas station ya vifaa vinavyokwenda anga za mbali ama sayari zingine itapunguza gharama za fuel za rockets.. hio tayari ni biashara itakayorudisha pesa ambazo zimewekezwa (ROI)..
Mwezini pia kutafanyika uchimbaji wa nishati safi , watachimba helium 3 ambapo mwezini kuna tani zaidi ya milioni.. duniani helium 3 kwa mwaka mzima inapatikana kilo 10 hadi 20 duniani kote kwa ujumla.. helium 3 ina thamani kubwa.. kwa kuanzisha uchimbaji huo wa helium 3 huko mwezini lazima fedha waliowekewa zitarudi na faida juu(ROI).
Maana gram moja pekee ya helium 3 ni dola karibu 19,000... je huo ni mradi wa hasara? Usiseme tu zaidi ya kutengeneza makaazi mengine ya binadamu huko mwezini hakuna faida nyingine ya maana...
Vingine ulivyouliza hapo naona havina mashiko..
Wabongo huwa mnataka matokeo ya haraka na shortcuts.. huu utamaduni wa kupenda vitu rahisi rahisi ndio maana kuamini mtu anaweza akafanya mambo magumu huwa hatuamini..Anawapiga watu kamba ili stocks zipande apige ela. Ana ahadi nyingi ambazo hazijatekelezeka. Alianza na Mars na alisema kufikia nadhani 2025 binadamua atakuwa ashaweka makazi now naona kaachana napo. Mpaka sasa rocket yake ambayo inapaswa kuwa ndiyo inasaforisha watu na mizigo hazijawa tayari kila test linaibuka tatizo.
Starlink inafanya poa na soace X haitengenezi faida maana mteja mkubwa wa soace X ni Starlink kama ambavyo mteja mkubwa wa cyber truck alikuwa space x.