Elon Musk azikosoa vikali ndege vita za F-35 na mradi mzima wa utengenezaji wa ndege hizo

huyu mwamba kapiga ndege wawili kwa jiwe mmoja hapa anapiga siasa na anatengeneza mazingira achukue tender na huenda akaja na bonge la suprise.
 
Mkuu nakumbuka tulikesha humu kumuelewesha jamaa lakini ni kama alikaza fuvu.
 
Elon Musk alitumia mfano wa Wachina walipoonyesha drones ukasema ooh manned fighters hamna kitu sasa ni mwendo wa drones tu.

Leo Wachina haohao walikuwa wanatest stealth jet mpya hata haijazinduliwa na inaendeshwa na rubani.

Xi Jinping

Kwahiyo vipi sasa wewe na Elon Musk mnasemaje. Wachina nao ni wapumbavu ila nyinyi ndio wajanja si ndio?
 
Wachina hawakuwahi kusema hivyo yalikuwa ni maoni yake Musk, ukweli ni kwamba drones zimekuja kuleta challenge kwenye warfare

Project ya China ya 6th generation ipo kwa miaka kadhaa na jana video zilisambaa kwenye mitandao zikionyesha first flight kwa hiyo hawajawahi kusema drones zitareplace fighter jets

Suala la kuendeshwa na rubani au haindeshwi na rubani hatuna jibu kamili kwani hata PLA haijatoa official announcement kuhusu. Cha muhimu fighter Jet successfully made its first flight

Na yako matoleo mawili moja la Chengdu yenye engines 3 na lingine ni Shenyang yenye engines 2

Lets wait for an official announcement
 
Elon Musk alitumia demonstration ya drones za Wachina kusema manned fighter jets ni upuuzi na ukamuunga mkono, mkasema vile vidrone ndio future of air warfare.

Jana Wachina haohao wameonyesha fighters mbili ambazo sio drones. Nakuuliza swali Wachina nao ni wajinga na wanazidiwa maarifa ya kijeshi na Elon Musk?
 
Wachina sio wajinga, ule ulikuwa tu ni mtazamo wa Elon Musk alitumia tu drones za Wachina
 
Wachina sio wajinga, ule ulikuwa tu ni mtazamo wa Elon Musk alitumia tu drones za Wachina
Ndio tunarudi palepale kwenye hoja yangu. Elon Musk sio military genius kwamba mtazamo wake ndio uwe mwelekeo sahihi, aliotolea mfano wenyewe wameishaonyesha ndege 3 za majaribio na zina marubani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…