Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Poor management nayo ilichangia,nakumbuka kuna mrembo alikuwa reception mid 90s alikuwa mpigaji mzuri sana wa dola na kupangisha vyumba akishirikiana na walinzi.

imagine mshahara wake ulikuwa elfu themanini lakini alikuwa anarudi home na kama laki nne kwa siku baadaye mkinga wa Peacock akamchukua.

pale napo akapiga sana na hivi mkinga alikuwa mshamba anamwambia usichukue malipo kwa dolaaa ndiyo akapata mwanya mwingine wa kupiga.RIP Dada Uncle wangu alikupenda sana.
Fafanua anko alimpendaje huyu dada
 
Nipo hapa mitaa posta mpya najaribu kuvuta siku ipite kutafuta riziki, maana kuna usemi wa wahenga unasema riziki ya mbwa ipo miguuni kwake.

Sasa ndugu zangu nimegeuza macho naona hili jengo naambiwa ilikuwa hotel moja kali sana miaka ya 80 kwa jina Embassy Hotel Dar es salaam, Lakini hapa kuna uzio wa mabati na nikicheki kupitia madirishani naona makorokoro kama viti, meza makochi nk.

Hili eneo ni very potential, wakongwe tujuzeni kuna nini kuhusu hii Hotel iliyotamba mno miaka hiyo leo kugeuka na kuwa kiota cha bundi?

Ni hayo tu kwa asubuhi hii.
Kuna tetesi kuwa ilikuwa mojawapo ya "straw company" ya kitengo chetu pendwa.
 
Hivyo vyote ni kumbukumbu ya ubaya wa ujamaa? Serikali haiwezi kumiliki biashara. Watafaidika wachache wanaoziendesha.
 
Serikali ibaki kutoa huduma tu biashara haiwezi.
 
Umeshaambiwa ilinunuliwa na wamiliki wa wet n wild
Tungempata huyo mmiliki wa sasa na kwa nini hapaendelezi, alinunua mwaka gani kwa kiasi gani cha pesa - ingetusaidia sana kupata pa kuanzia.
 
Nasubiri nione Ngorongoro mountain lodge itaangukia wapi?.
Kuna wakati ilitekwa pia, baada ya media kuhoji sana ilidaiwa kuridishwa lakini hakuna ushahidi.
 
Tungempata huyo mmiliki wa sasa na kwa nini hapaendelezi, alinunua mwaka gani kwa kiasi gani cha pesa - ingetusaidia sana kupata pa kuanzia.
Ukitaka kupata undani wa Embassy Hotel ingia kwa gia ya kutaka kuwekeza hapo, anzia TIC.
 
Silver sand hotel nayo imebaki magofu ya wavuta bangi.
Ilaaniwe serikali ya CCM.
Ni kati ya mali za umma zilizoangukia mikononi mwa mafisadi. Maamuzi ya kuziendeleza yalikwama siku nyingi kwa sababu wahusika wakuu kwenye huo mgogoro ni wakubwa tu wenye maslahi yao ambao waliishastaafu.

Siyo hiyo tu, Kuna nyingine mbili zilizokuwa Icône ya Jiji .... Twiga Hotel na Motel Agip zote zimebakia kuwa magofu ya Serikali....Skyway Continental zote zimebaki majina tu.
 
Kuna wakati ilitekwa pia, baada ya media kuhoji sana ilidaiwa kuridishwa lakini hakuna ushahidi.
Bado ipo mikononi mwa serikali ila ni dhoofu, but kiukweli ile hoteli is one of the best hotel iliyopo eneo lile ndiyo mwana mapaka wana dondosha udenda.

Yule jirani yake pale anaroom mpaka 10mil per night ila kwa ustadi hii yetu bado ipo matawi.
 
Ile hotel ya Ngorongoro ilijengwa kwa mbinde enzi za Nyerere, kulikuwa na upinzani mkubwa wa wanamazingira wakati huo kuwa uwepo wa hoteli ya kitalii mbugani utakuja kuathiri bioanuai ya viumbe. Ukilinganisha nguvu iliyotumika kuitetea mpaka ikajengwa na ufanisi na mapato yatokanayo na mradi ni viwili tofauti....
 
Hivyo vyote ni kumbukumbu ya ubaya wa ujamaa? Serikali haiwezi kumiliki biashara. Watafaidika wachache wanaoziendesha.
Mkuu hiyo hotel haikufa enzi za umiliki wa serikali enzi za ujamaa.
Tatizo limeanza baada ya kukataa ujamaa na serikali kujitoa umiliki kwa kuuza hisa zake.
Tatizo ubinafishaji unao ushabikia.
Sijui kama umesoma maoni ya watu shida ni nini hadi ikafungwa.
 
Back
Top Bottom