Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

Moja kwa moja hojani,

Kwa mjibu wa website ya CCM, na Kwa mjibu wa kauli ya mwenezi wa CCM ndugu Hamphuley Polepole, CCM inawanachama wa kudumu M.14+
Na kikawaida, ili uwe mwanachama wa Chama chochote, maana yake uwe umefikia umri wa miaka 18+

Na kwa idaadi ya waliojiandikisha kupiga Kura nchi nzima ni M.29+

Kama ndio hivyo, maana yake CCM, Kati ya wapiga Kura M.29+ CCm inamtaji wa nusu ya wapigakura wote ikiwa wote watakuwa wamejandikisha

Sasa basi, Ni Kwa namna Ipi Chadema wataishinda CCM?

Let go...

Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?

Je, ni kwa sababu ya mwitikio wa watu kwenye Kampeni za mgombea wa Chama chao?

Je, ni kwa sababu ya kuhesabu uwingi wa washabiki na wachangiaji kupitia Mitandao ya kijamii?

Je, ni kwa sababu mgombea wa Chama hicho anajua sana sheria?

Je, ni kwa sababu mgombea wake anafahamiana na kujulikana na viongozi wa mataifa mengi duniani

Ni kwa sababu zipi haswa hawa Chadema kujiaminisha kuwa watashinda uchaguzi huu?

Kama ni Kwa sababu ya watu wengi kujaa katika mikutano yake, mbona hata haifikii uwingi wa watu wa mgombea na mpinzani wake Kutokea CCM?

Mbona Mikutano yake na jinsi watu inavyo jaa, ni kama Tu Ile mikutano anayoifanya waziri mkuu Majaliwa?

Mitaani watu wengi ukiwahoji, wanasema kwamba, Mgombea uriais kupitia Chadema, atashindana, lakini kushinda atashinda wa CCM

Nimalizie kwa kuuliza, je, ni kwa kigezo kipi kinachowapa wanachadema waseme Chama Chao kitamwangusha Magufuli?
Kuwa mwanachama haina maana utapigia kura ccm
 
Bado sana mkuu, bado hatujapata upinzani wa watu wenye akili timam ambao tunaweza sema tujaribu kuwapa nchi.
Hao wenye akili wakoje na wapo wapi?
Pema usijapo pema ukipema si pema tena
Ukweli ccm ukweli mnaujua ndiyo maana mmepoaaaa!!
 
Wanakwambia"watu wamelala barabarani ili Lissu asimame aongee wamsikie, kweli Lissu ni Rais", yani kwa watu kulala barabarani basi ndo kigezo cha Lissu kushinda urais.Chadema ndo matahira kweRi kweRi.
Matusi mnayaweza siyo hoja
Na hii ni dalili ya kushindwa
 
Hao wenye akili wakoje na wapo wapi?
Pema usijapo pema ukipema si pema tena
Ukweli ccm ukweli mnaujua ndiyo maana mmepoaaaa!!
Nikukumbushe kidogo, kinachomfanya mtu awe kiongozi ni Kura na sio swala la kuchangamka au kupoa.
 
Moja kwa moja hojani,

Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?...
Hayo ni maswali ya kijinga ya mtu mjinga lazima wa CCM ya wajinga kwa sababu angekuwa na akili hata kidogo tu angeuliza: Je ni kigezo gani kinawapa wanachama wa CCM na viongozi wao kudai kuwa watashinda kati ya Vyama 14 vinavyoshindana.

licha ya kuboronga miaka 5 waliyopewa? Ukijibu swali hili sasa jaribu kujibu maswali yako kwa kuweka CCM badala ya CHADEMA na Lissu badala ya Magufuli.
 
Wanakwambia"watu wamelala barabarani ili Lissu asimame aongee wamsikie, kweli Lissu ni Rais", yani kwa watu kulala barabarani basi ndo kigezo cha Lissu kushinda urais.Chadema ndo matahira kweRi kweRi.
[emoji3][emoji3][emoji3]Umenikumbusha siku EL alipidekiwa barabara
 
Hayo ni maswali ya kijinga ya mtu mjinga lazima wa CCM ya wajinga kwa sababu angekuwa na akili hata kidogo tu angeuliza:
Mkuu, ukiambiwa ukweli utachukia?

Kwa ulichoandika hapa, kinakuonyesha kabisa wewe ni mjinga haswaa, Umeshindwa nini KUELEWA kile CCM kinachowafanya waseme watashinda,

Kwanza, kinawanachama na wapiga Kura 14.M+, idadi ya waliojiandikisha ni 29M+

Kati ya hao, CCM inawatu kinindoni zaidi ya 14.m,ikiwa watu hao wataipigia Kura

Je, Chadema unatumia kigezo gani kusema inashinda?

Uspaniki Mzee, mambo mengine hayahitaji hasira aisee
 
Ukweli lazima usemwe, CHADEMA wana asilimia chache sana za kuibuka na ushindi kwenye kinyang'anyiro hiki...
Mkuu umemaliza yote!

Kuna jamaa mmoja yuko humu anatumia ID ya tindo, yeye huwa anahoja sana ila siku ile selikali imetangaza siku za watu kwenda kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura yeye alikuwa anakejeli na kupinga kwamba huo ni ujinga kwenda kupoteza muda huko.

Kuna siku Mbowe alisema chadema nendeni kuboresha taarifa zenu, huyu jamaa akamkejeli Mbowe kwamba wataenda wajinga ila wenye akili hawana huo muda. Cha ajabu sana leo nae anashangilia Lisu atashinda.
 
Umenena yaliyonyooka msitari.

CHADEMA ilikuwa na nafasi kubwa kushinda 2015.
√ Mgombea wao Lowassa, alikuwa na bado ana nguvu kubwa kisiasa kuliko Lissu, maradufu;..
Sasa ni 2020 siyo 2015 watu wana machungu ya unyanyasaji uonevu kuwabambikia kesi kupigwa risasi, ufisadi wa trilion 1.5 kisha CAG akatolewa kafara , watu wameamka wanajua haki zao
 
Huu ni mwaka 2020 na sio mwaka 1995. Vijijini wanamjua Lissu vizuri mno na huko ndipo ambapo lissu atapata ushindi wa tsunami kabisa. Maana ccm hamjawapelekea milioni 50 wanakijiji, uchaguzi wa serikali za mitaa CCM waliuharibu, majimbo mengine watu wamelazimisha kupita bila kupingwa, barabara mbovu,pia watu wanakunywa maji kama matope na wakulima wamedhurumiwa malipo yao, sukari bei imepanda.

Na huko vijijini vyuma vimekaza mno. Ndugu zao waliopo mjini wanaowategemea na wao pia pesa hawana na vyuma vimewabana. Hata wewe pia najua kura yako utampa Lissu.

Mwaka huu Lissu ushindi atakaopata utavunja rekodi.
Unafikiri wanakijiji wana huo ujinga wenu wakungojea hela mifukoni?

Tatizo lako upo tu kwa shemeji yako hapo kwa mtogole! Zunguka zunguka nchi hii ni kubwa
 
Chadema hakina uwezo wa kushinda. Kama huo ni ukweli kwanini maccm wahofie kuwepo kwa Tume HURU badala ya hii Tume FAKE!? Kwanini wahofie kura kuhesabiwa hadharani ili tupate mshindi halali na kuionyesha dunia kwamba Tanzania uchaguzi wetu ni HURU na wa HAKI!? [emoji15]

View attachment 1583971
Yani wewe ndio unataka kura zihesabiwe hadharani!? Kwa sheria ipi?
 
Sababu zipo nyingi sina ila mimi nakupa dalili chache tu :-

1. Mkurugenzi wa uchaguzi umemsikia leo akimfanyia kampeni Magufuli? Hii ni moja ya dalili kama kuna kila dalili cdm kushinda uchaguzi huu, mkurugenzi amefanya jambo ambalo kwa akili za kawaida halikutakiwa kutokea,wasomi wanasema mkurugenzi wa uchaguzi amepanic au anaweweseka...
Morali na hamasa waliyonayo mashabiki na wafuasi wa TL ni tofauti Sana na Ile ya washabiki wa CCM. Wafuasi wa CCM wanaonesha kabisa mioyo yao haipo pale, Ila njaa na mabavu ndio yamewafanya wawepo hapo. Molari ya Wafuasi wa TL haijawahi onekana katika chaguzi zilizotangulia. Vijana Wana Power na Confidence Kubwa Sana.
 
Wanachokifanya chadema ni kujidifend ili ata wakishindwa waseme wameibiwa ila ki ukweli hakuna chama kwa Sasa Tanznaia ambacho kinaweza kuipiku ccm
 
Moja kwa moja hojani,

Kwa mjibu wa website ya CCM, na Kwa mjibu wa kauli ya mwenezi wa CCM ndugu Hamphuley Polepole, CCM inawanachama wa kudumu M.14+
Na kikawaida, ili uwe mwanachama wa Chama chochote, maana yake uwe umefikia umri wa miaka 18+

Na kwa idaadi ya waliojiandikisha kupiga Kura nchi nzima ni M.29+

Kama ndio hivyo, maana yake CCM, Kati ya wapiga Kura M.29+ CCm inamtaji wa nusu ya wapigakura wote ikiwa wote watakuwa wamejandikisha na kuipigia Kura CCM siku ya uchaguzi

Sasa basi, Ni Kwa namna Ipi Chadema wataishinda CCM?

Let go...

Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?

Je, ni kwa sababu ya mwitikio wa watu kwenye Kampeni za mgombea wa Chama chao?

Je, ni kwa sababu ya kuhesabu uwingi wa washabiki na wachangiaji kupitia Mitandao ya kijamii?

Je, ni kwa sababu mgombea wa Chama hicho anajua sana sheria?

Je, ni kwa sababu mgombea wake anafahamiana na kujulikana na viongozi wa mataifa mengi duniani

Ni kwa sababu zipi haswa hawa Chadema kujiaminisha kuwa watashinda uchaguzi huu?

Kama ni Kwa sababu ya watu wengi kujaa katika mikutano yake, mbona hata haifikii uwingi wa watu wa mgombea na mpinzani wake Kutokea CCM?

Mbona Mikutano yake na jinsi watu inavyo jaa, ni kama Tu Ile mikutano anayoifanya waziri mkuu Majaliwa?

Mitaani watu wengi ukiwahoji, wanasema kwamba, Mgombea uriais kupitia Chadema, atashindana, lakini kushinda atashinda wa CCM

Nimalizie kwa kuuliza, je, ni kwa kigezo kipi kinachowapa wanachadema waseme Chama Chao kitamwangusha Magufuli?
kama ina wanachama 14M+ ilikuwaje 2015 CCM ikapata kura 8M na upinzani ukapata 6M?
 
Back
Top Bottom