CCM
Moja kwa moja hojani,
Kwa mjibu wa website ya CCM, na Kwa mjibu wa kauli ya mwenezi wa CCM ndugu Hamphuley Polepole, CCM inawanachama wa kudumu M.14+
Na kikawaida, ili uwe mwanachama wa Chama chochote, maana yake uwe umefikia umri wa miaka 18+
Na kwa idaadi ya waliojiandikisha kupiga Kura nchi nzima ni M.29+
Kama ndio hivyo, maana yake CCM, Kati ya wapiga Kura M.29+ CCm inamtaji wa nusu ya wapigakura wote ikiwa wote watakuwa wamejandikisha na kuipigia Kura CCM siku ya uchaguzi
Sasa basi, Ni Kwa namna Ipi Chadema wataishinda CCM?
Let go...
Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?
Je, ni kwa sababu ya mwitikio wa watu kwenye Kampeni za mgombea wa Chama chao?
Je, ni kwa sababu ya kuhesabu uwingi wa washabiki na wachangiaji kupitia Mitandao ya kijamii?
Je, ni kwa sababu mgombea wa Chama hicho anajua sana sheria?
Je, ni kwa sababu mgombea wake anafahamiana na kujulikana na viongozi wa mataifa mengi duniani
Ni kwa sababu zipi haswa hawa Chadema kujiaminisha kuwa watashinda uchaguzi huu?
Kama ni Kwa sababu ya watu wengi kujaa katika mikutano yake, mbona hata haifikii uwingi wa watu wa mgombea na mpinzani wake Kutokea CCM?
Mbona Mikutano yake na jinsi watu inavyo jaa, ni kama Tu Ile mikutano anayoifanya waziri mkuu Majaliwa?
Mitaani watu wengi ukiwahoji, wanasema kwamba, Mgombea uriais kupitia Chadema, atashindana, lakini kushinda atashinda wa CCM
Nimalizie kwa kuuliza, je, ni kwa kigezo kipi kinachowapa wanachadema waseme Chama Chao kitamwangusha Magufuli?

CCM wanaweza wakashinda lakini kwa wizi na dhulma.
Japo pia dhulma na wanaitengeza Mungu atawaangamiza kama Korona mana Mungu ameamua alipiganie taifa lake linalodhuliwa kutokana na upole,ujinga,umaskini unaotumiwa kama fimbo ya kuwaswaga watu wake huku waliodhulumu wakineemeka na dhulma zao hivyo kuwafanya watu wengi kutamani kujiunga na dhulma.
CCM kina kadi nyingi hewa mana wazee wengi ndio wanachama wa CCM . Wazee wengi wa umri wa Mkapa ndio wanachama wa CCM wasioyumba hata wakiona dhulma kubwa wanaisifia. Hao wengi wameshatangulia mbele za haki na wengine ni wagonjwa na uhakika wa kupiga kura hawana.
Lakini pia CCM kipindi hiki imepata wanachama wengi feki kama Alivyo Bashiru Ally , Mtatiro ,Ana Ngwira, Kafulila, Katambi, Nasari, na wengine wengi. Hao wangejua kuwa Lisu atarudi wasingejiunga na CCM . Hao adui yao alikua ni yule mlevi na Fisadi Mbowe aloyemleta Fisadi Lowasa.
CCM itapoteza kura nyingi sana kutoka kwa WanaCCM waliochoka siasa za kutishana ,kuuana ,kufitiniana, kukomoana, kudhulumiana, kuchafuana , kujipendekeza, kudhalilishana na kudharauliana .
Kura kwa Lisu , nyingi zitatoka kwa wale wanaojiita CCM lakini wapenda haki na usawa.
Kura nyingi kwa Lisu na Chadema zitatoka kwa watanzania wasiopenda kuona nchi hii inaingia kwenye ukabila wa wazi na kuona serikali ikiweka dini zote mfukoni kwake na kuwafanya watu wenye madaraka kuwa miungu ya kuabudiwa kwa sifa na shukrani huku wakipewa enzi na kutawala milele.
Kura nyingi zitatoka kwa wanaCCM wasiotaka kuona nchi hii inatawaliwa na mtu mmoja maisha yaani kuwa na Rais wa maisha eti kwa sababu amenunua ndege kwa kodi za wananchi.
Kura nyingi kwa Lisu zitatoka kwa Watanzania na wanachama wa CCM wasiopenda kuona ndugu zao na marafiki zao wanapigwa risasi na kupotea bila sababu ya msingi.
Kura nyingi kwa Lisu zitatoka Zanzibar kwa wanaCCM na Wana ACT .
Kura nyingi kwa Lisu zitatoka kwenye vijiji vilivyotengwa na kunyimwa mil.50 isipokuwa Chato pekee . Kura nyingi zitatoka kwa watanzania waliokos mgao wa Noah za makinikia.
Ni vita kati ya matajiri waliokwapua mali za umma na kujiuzia kila kitu mpaka nyumba za umma na sasa wanafanya kila hila kunakia madarakani huku wakitoa rushwa kwa tume na makada wengine wa CCM ndani ya vyombo vya dola.
Ushindi wa Chadema unaweza ukawa sio ndoto bali ni kweli.
Dhulma iondoke ili CCM ishinde au ishindwe kwa haki.