Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

kama ina wanachama 14M+ ilikuwaje 2015 CCM ikapata kura 8M na upinzani ukapata 6M?
Ndio maana tunasema Lisu hana lolote ni debe tupu,,
Mpinzani pekee aliekuwa na uwezo wa kuitoa ccm ni Lowasa sababu alikuwa anavuka hadi mistari ya vyama vingine ndio maana alipata hizi kura.

Lisu hana mtaji wa kura zozote nje ya chadema.

Lisu ni debe tupu
 
Wanachokifanya chadema ni kujidifend ili ata wakishindwa waseme wameibiwa ila ki ukweli hakuna chama kwa Sasa Tanznaia ambacho kinaweza kuipiku ccm
CCM imeshapotea hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu ataipigia CCM kura zaidi ya nyinyi wachache wanufaika wa mfumo kandamizi mfumo uonevu unyanyasaji mliofaidi trilion 1.5 mgao 10% ununuzi wa Ndege na tenda za ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge
 
Moja kwa moja hojani,

Kwa mjibu wa website ya CCM, na Kwa mjibu wa kauli ya mwenezi wa CCM ndugu Hamphuley Polepole, CCM inawanachama wa kudumu M.14+
Na kikawaida, ili uwe mwanachama wa Chama chochote, maana yake uwe umefikia umri wa miaka 18+

Na kwa idaadi ya waliojiandikisha kupiga Kura nchi nzima ni M.29+

Kama ndio hivyo, maana yake CCM, Kati ya wapiga Kura M.29+ CCm inamtaji wa nusu ya wapigakura wote ikiwa wote watakuwa wamejandikisha na kuipigia Kura CCM siku ya uchaguzi

Sasa basi, Ni Kwa namna Ipi Chadema wataishinda CCM?

Let go...

Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?

Je, ni kwa sababu ya mwitikio wa watu kwenye Kampeni za mgombea wa Chama chao?

Je, ni kwa sababu ya kuhesabu uwingi wa washabiki na wachangiaji kupitia Mitandao ya kijamii?

Je, ni kwa sababu mgombea wa Chama hicho anajua sana sheria?

Je, ni kwa sababu mgombea wake anafahamiana na kujulikana na viongozi wa mataifa mengi duniani

Ni kwa sababu zipi haswa hawa Chadema kujiaminisha kuwa watashinda uchaguzi huu?

Kama ni Kwa sababu ya watu wengi kujaa katika mikutano yake, mbona hata haifikii uwingi wa watu wa mgombea na mpinzani wake Kutokea CCM?

Mbona Mikutano yake na jinsi watu inavyo jaa, ni kama Tu Ile mikutano anayoifanya waziri mkuu Majaliwa?

Mitaani watu wengi ukiwahoji, wanasema kwamba, Mgombea uriais kupitia Chadema, atashindana, lakini kushinda atashinda wa CCM

Nimalizie kwa kuuliza, je, ni kwa kigezo kipi kinachowapa wanachadema waseme Chama Chao kitamwangusha Magufuli?
Majibu yako ni rahisi saana:

1. Sio wanachama woote wa CCM watampigia CCM JIWE. Mie pamoja na dugu zangu sita (jumla) ni wanachama wa CCM lakini hatuwezi kupoteza kura yetu kumpigia kura mtu aliyesababisha Baba yangu asimamishwe kazi kwa kukataa kutii amri za mwenyekiti wa CCM Mkoa aliyetaka kuwatengenezea kesi ya uwongo vijana wawili ambao inasemekana ni wanachama wa Chadema. Vile vile wadogo zangu wawili wamebomolewa nyumba zao kimara..(sakata la barabara). Hapo sijaweweka wale wengine walioumizwa kama akina Membe n,k. Hivi unategemea mtu Kama January makamba,Nape au Mzee kinana, au JK watampigia kura JIWE? pevuka kidogo

2. Nyomi la mikutano ya CCM kafanye utafiti kama wanakuja kwa wito au ni kubebwa kwa kupewa buku tano.Ndugu zangu wengi wamekula saana hizi buku tano na kura wamesema ni siri yao
 
Ndio maana tunasema Lisu hana lolote ni debe tupu,,
Mpinzani pekee aliekuwa na uwezo wa kuitoa ccm ni Lowasa sababu alikuwa anavuka hadi mistari ya vyama vingine ndio maana alipata hizi kura.

Lisu hana mtaji wa kura zozote nje ya chadema.

Lisu ni debe tupu
Wewe ndiyo debe tupu hujielewi mwaka 2015 watanzania hawakuwa hawa wa sasa ambao wametaabika kwa mateso kibao kubambikiwa kesi kupigwa risasi uonevu unyanyasaji mwingi na mambo mengi ya hovyo yasiyo na tija kwa Taifa, Usifananishe ya lowasa na sasa kwani sasa watanzania wameamka hawataki ujinga wa CCM kabsa
 
Zipi? Hebu ziweke hapa
NECCCM Tumeccm nao sasa eti wanapiga kampeni na cha ajabu eti chombo binafsi cha CCM eti wakamhoji Lisu ni maajabu yaliyopa Tanzania pekee hakuna ujinga huu sehemu zingine Duniani
 
Ccm itashinda sabab mashabiki wengi wa Cdm hawajajiandkisha kwenye daftar la wapga kura
Hizi fikra za kizamani sana achana Nazi,nw hivi vitambulisho vinatumika ktk maeneo mbalimbali ya kijamii so watu waliona no muhimu kuwa navyo zaidi ya kupigia kura 2/, acha kujidanganya
 
Mkuu, ukiambiwa ukweli utachukia?

Kwa ulichoandika hapa, kinakuonyesha kabisa wewe ni mjinga haswaa, Umeshindwa nini KUELEWA kile CCM kinachowafanya waseme watashinda,

Kwanza, kinawanachama na wapiga Kura 14.M+, idadi ya waliojiandikisha ni 29M+

Kati ya hao, CCM inawatu kinindoni zaidi ya 14.m,ikiwa watu hao wataipigia Kura

Je, Chadema unatumia kigezo gani kusema inashinda?

Uspaniki Mzee, mambo mengine hayahitaji hasira aisee
Kwenye Uchaguzi wowote wapiga kura siyo wanachama wa Vyama vya Siasa bali ni Raia wa nchi husika ndo maana mpiga kura yeyote haruhusiwi kwenda Kituo cha Kupigia Kura na sare au utambulisho wowote wa Chama chake. Kama damu ingekuwa inaonekana, maCCM nguli yenye damu ya kijani yangezuiwa kupiga kura!
 
Moja kwa moja hojani,

Kwa mjibu wa website ya CCM, na Kwa mjibu wa kauli ya mwenezi wa CCM ndugu Hamphuley Polepole, CCM inawanachama wa kudumu M.14+
Na kikawaida, ili uwe mwanachama wa Chama chochote, maana yake uwe umefikia umri wa miaka 18+

Na kwa idaadi ya waliojiandikisha kupiga Kura nchi nzima ni M.29+

Kama ndio hivyo, maana yake CCM, Kati ya wapiga Kura M.29+ CCm inamtaji wa nusu ya wapigakura wote ikiwa wote watakuwa wamejandikisha na kuipigia Kura CCM siku ya uchaguzi

Sasa basi, Ni Kwa namna Ipi Chadema wataishinda CCM?

Let go...

Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?

Je, ni kwa sababu ya mwitikio wa watu kwenye Kampeni za mgombea wa Chama chao?

Je, ni kwa sababu ya kuhesabu uwingi wa washabiki na wachangiaji kupitia Mitandao ya kijamii?

Je, ni kwa sababu mgombea wa Chama hicho anajua sana sheria?

Je, ni kwa sababu mgombea wake anafahamiana na kujulikana na viongozi wa mataifa mengi duniani

Ni kwa sababu zipi haswa hawa Chadema kujiaminisha kuwa watashinda uchaguzi huu?

Kama ni Kwa sababu ya watu wengi kujaa katika mikutano yake, mbona hata haifikii uwingi wa watu wa mgombea na mpinzani wake Kutokea CCM?

Mbona Mikutano yake na jinsi watu inavyo jaa, ni kama Tu Ile mikutano anayoifanya waziri mkuu Majaliwa?

Mitaani watu wengi ukiwahoji, wanasema kwamba, Mgombea uriais kupitia Chadema, atashindana, lakini kushinda atashinda wa CCM

Nimalizie kwa kuuliza, je, ni kwa kigezo kipi kinachowapa wanachadema waseme Chama Chao kitamwangusha Magufuli?
Unapoingia kwenye pambano huingii kushindwa bali kushinda, ukiona mpinzani yeyote anasema atashindwa bila kuingia uwanjani huyo hastahili, naamini si tu chadema kila chama kilichosimamisha mgombea kina imani ya kushinda, hata kama hakitoshinda.
 
Majibu yako ni rahisi saana:

1. Sio wanachama woote wa CCM watampigia CCM JIWE. Mie pamoja na dugu zangu sita (jumla) ni wanachama wa CCM lakini hatuwezi kupoteza kura yetu kumpigia kura mtu aliyesababisha Baba yangu asimamishwe kazi kwa kukataa kutii amri za mwenyekiti wa CCM Mkoa aliyetaka kuwatengenezea kesi ya uwongo vijana wawili ambao inasemekana ni wanachama wa Chadema. Vile vile wadogo zangu wawili wamebomolewa nyumba zao kimara..(sakata la barabara). Hapo sijaweweka wale wengine walioumizwa kama akina Membe n,k. Hivi unategemea mtu Kama January makamba,Nape au Mzee kinana, au JK watampigia kura JIWE? pevuka kidogo

2. Nyomi la mikutano ya CCM kafanye utafiti kama wanakuja kwa wito au ni kubebwa kwa kupewa buku tano.Ndugu zangu wengi wamekula saana hizi buku tano na kura wamesema ni siri yao
CCM bila fuso kusomba watu bila wasanii wa bongo fleva hauna mkutano hapo, CCM ni ile ile ukoo wa panya
 
Ukweli lazima usemwe, CHADEMA wana asilimia chache sana za kuibuka na ushindi kwenye kinyang'anyiro hiki.

Wakati wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura CCM ilikuwa ipo kwenye mkakati mkali was kuhakikisha wanachama wake wanajiandikisha au wanarekebisha taarifa zao kwenye daftari hilo

CDM wao walikuwa wanafurahia kususia zoezi hilo wakidhani kwamba wanaikomoa serikali, kitu cha kusikitisha ni kwamba, hata viongozi wao walikuwa wanawaunga mkono wasiende kujiandikisha, na wakati mwingine walikuwa wanatupia picha mitandaoni kwa furaha kabisa kuonesha uchache wa watu kwenye vituo.

Baya zaidi wengi wa wafuasi wa CHADEMA sio wapiga kura, we angalia tu kwenye mikutano yao wapiga kura utawajua na wahuni utawajua, wengi hawana hata vitambulisho vya mpiga kura, sasa huo ushindi unatokea wapi.

Hebu acheni kujifariji jamani, mambo sio mazuri kwa upande wenu, ndio maana TL ameanzisha mtindo wa kuhutubia huku anatoa vitisho kwa tume, mara uchaguzi huu unaangaliwa na mataifa mbalimbali, cha kumwambia ni kwamba hakuna wa kumuibia kura ila ajiandae kiakili tu kwamba keshashindwa, CCM inaweza kuwa kwenye migogoro weeeee, lakini wanapofika wakati wa uchaguzi ndio wanaondoa tofauti zao wanaungana kuwa kitu kimoja chenye nguvu kubwa.
Hata hao ccm sio wote watapigia kura kwa magufuli sie tunaoenda vijijini huko kwenye mishe mishe zetu huwa tunafanya research kidogo hasa tukimkuta mtu kada was ccm ,majibu wanayotoa ni kwamba miaka mitano ya magufuli kafanya watu kuwa maskini zaidi eg wakulima na wafanyabiashara
 
Kigezo kikuu cha CCM kushindwa ni uonevu unyanyasaji uovu waliowatendea watanzania wengi ikiwemo wafanyabiashara wakubwa kuporwa pesa mali zao kubambikiwa kesi, watanzania waliopo nje kuzuiwa kuleta pesa nyingi kwa ndugu zao kwa visingizio vya uhujumu uchumi na mambo mengi ya hovyo ambayo hayapo Nchi za jirani na kwingine Duniani
 
Hata hao ccm sio wote watapigia kura kwa magufuli sie tunaoenda vijijini huko kwenye mishe mishe zetu huwa tunafanya research kidogo hasa tukimkuta mtu kada was ccm ,majibu wanayotoa ni kwamba miaka mitano ya magufuli kafanya watu kuwa maskini zaidi eg wakulima na wafanyabiashara
Uchumi wa kenya umekuwa kwa sababu wanaruhusu pesa kutoka nje kuingia kenya kwa wingi bila masharti ya wivu kama utawala huu wa wivu uliopo Tanzania sasa, kuzuia pesa kuja imewafanya watanzania wengi kuwekeza Uganda kenya Rwanda ambapo wanatuma pesa pasipo usumbufu wa kijinga jinga kama Tanzania
 
Hata hao ccm sio wote watapigia kura kwa magufuli sie tunaoenda vijijini huko kwenye mishe mishe zetu huwa tunafanya research kidogo hasa tukimkuta mtu kada was ccm ,majibu wanayotoa ni kwamba miaka mitano ya magufuli kafanya watu kuwa maskini zaidi eg wakulima na wafanyabiashara
wanaccm wengi moyoni ni wapinzani ingawa huvaa nguo za CCM usoni ili kulinda mali zao binafsi wasije kubambikiwa kesi na kuporwa mali zao
 
Wafanyabiashara ambao ndiyo hutoa ajila nyingi wamedhoofishwa mno na utawala huu mpaka kupelekea kuathiri ajila kwa kiwango cha kutisha sana
 
Back
Top Bottom