Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

kama ina wanachama 14M+ ilikuwaje 2015 CCM ikapata kura 8M na upinzani ukapata 6M?
Ndio maana tunasema Lisu hana lolote ni debe tupu,,
Mpinzani pekee aliekuwa na uwezo wa kuitoa ccm ni Lowasa sababu alikuwa anavuka hadi mistari ya vyama vingine ndio maana alipata hizi kura.

Lisu hana mtaji wa kura zozote nje ya chadema.

Lisu ni debe tupu
 
Wanachokifanya chadema ni kujidifend ili ata wakishindwa waseme wameibiwa ila ki ukweli hakuna chama kwa Sasa Tanznaia ambacho kinaweza kuipiku ccm
CCM imeshapotea hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu ataipigia CCM kura zaidi ya nyinyi wachache wanufaika wa mfumo kandamizi mfumo uonevu unyanyasaji mliofaidi trilion 1.5 mgao 10% ununuzi wa Ndege na tenda za ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge
 
Majibu yako ni rahisi saana:

1. Sio wanachama woote wa CCM watampigia CCM JIWE. Mie pamoja na dugu zangu sita (jumla) ni wanachama wa CCM lakini hatuwezi kupoteza kura yetu kumpigia kura mtu aliyesababisha Baba yangu asimamishwe kazi kwa kukataa kutii amri za mwenyekiti wa CCM Mkoa aliyetaka kuwatengenezea kesi ya uwongo vijana wawili ambao inasemekana ni wanachama wa Chadema. Vile vile wadogo zangu wawili wamebomolewa nyumba zao kimara..(sakata la barabara). Hapo sijaweweka wale wengine walioumizwa kama akina Membe n,k. Hivi unategemea mtu Kama January makamba,Nape au Mzee kinana, au JK watampigia kura JIWE? pevuka kidogo

2. Nyomi la mikutano ya CCM kafanye utafiti kama wanakuja kwa wito au ni kubebwa kwa kupewa buku tano.Ndugu zangu wengi wamekula saana hizi buku tano na kura wamesema ni siri yao
 
Wewe ndiyo debe tupu hujielewi mwaka 2015 watanzania hawakuwa hawa wa sasa ambao wametaabika kwa mateso kibao kubambikiwa kesi kupigwa risasi uonevu unyanyasaji mwingi na mambo mengi ya hovyo yasiyo na tija kwa Taifa, Usifananishe ya lowasa na sasa kwani sasa watanzania wameamka hawataki ujinga wa CCM kabsa
 
Zipi? Hebu ziweke hapa
NECCCM Tumeccm nao sasa eti wanapiga kampeni na cha ajabu eti chombo binafsi cha CCM eti wakamhoji Lisu ni maajabu yaliyopa Tanzania pekee hakuna ujinga huu sehemu zingine Duniani
 
Ccm itashinda sabab mashabiki wengi wa Cdm hawajajiandkisha kwenye daftar la wapga kura
Hizi fikra za kizamani sana achana Nazi,nw hivi vitambulisho vinatumika ktk maeneo mbalimbali ya kijamii so watu waliona no muhimu kuwa navyo zaidi ya kupigia kura 2/, acha kujidanganya
 
Kwenye Uchaguzi wowote wapiga kura siyo wanachama wa Vyama vya Siasa bali ni Raia wa nchi husika ndo maana mpiga kura yeyote haruhusiwi kwenda Kituo cha Kupigia Kura na sare au utambulisho wowote wa Chama chake. Kama damu ingekuwa inaonekana, maCCM nguli yenye damu ya kijani yangezuiwa kupiga kura!
 
Unapoingia kwenye pambano huingii kushindwa bali kushinda, ukiona mpinzani yeyote anasema atashindwa bila kuingia uwanjani huyo hastahili, naamini si tu chadema kila chama kilichosimamisha mgombea kina imani ya kushinda, hata kama hakitoshinda.
 
CCM bila fuso kusomba watu bila wasanii wa bongo fleva hauna mkutano hapo, CCM ni ile ile ukoo wa panya
 
Hata hao ccm sio wote watapigia kura kwa magufuli sie tunaoenda vijijini huko kwenye mishe mishe zetu huwa tunafanya research kidogo hasa tukimkuta mtu kada was ccm ,majibu wanayotoa ni kwamba miaka mitano ya magufuli kafanya watu kuwa maskini zaidi eg wakulima na wafanyabiashara
 
Kigezo kikuu cha CCM kushindwa ni uonevu unyanyasaji uovu waliowatendea watanzania wengi ikiwemo wafanyabiashara wakubwa kuporwa pesa mali zao kubambikiwa kesi, watanzania waliopo nje kuzuiwa kuleta pesa nyingi kwa ndugu zao kwa visingizio vya uhujumu uchumi na mambo mengi ya hovyo ambayo hayapo Nchi za jirani na kwingine Duniani
 
Uchumi wa kenya umekuwa kwa sababu wanaruhusu pesa kutoka nje kuingia kenya kwa wingi bila masharti ya wivu kama utawala huu wa wivu uliopo Tanzania sasa, kuzuia pesa kuja imewafanya watanzania wengi kuwekeza Uganda kenya Rwanda ambapo wanatuma pesa pasipo usumbufu wa kijinga jinga kama Tanzania
 
wanaccm wengi moyoni ni wapinzani ingawa huvaa nguo za CCM usoni ili kulinda mali zao binafsi wasije kubambikiwa kesi na kuporwa mali zao
 
Wafanyabiashara ambao ndiyo hutoa ajila nyingi wamedhoofishwa mno na utawala huu mpaka kupelekea kuathiri ajila kwa kiwango cha kutisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…