Moja kwa moja hojani,
Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?
Je, ni kwa sababu ya mwitikio wa watu kwenye Kampeni za mgombea wa Chama chao?
Je, ni kwa sababu ya kuhesabu uwingi wa washabiki na wachangiaji kupitia Mitandao ya kijamii?
Je, ni kwa sababu mgombea wa Chama hicho anajua sana sheria?
Je, ni kwa sababu mgombea wake anafahamiana na kujulikana na viongozi wa mataifa mengi duniani
Ni kwa sababu zipi haswa hawa Chadema kujiaminisha kuwa watashinda uchaguzi huu?
Kama ni Kwa sababu ya watu wengi kujaa katika mikutano yake, mbona hata haifikii uwingi wa watu wa mgombea na mpinzani wake Kutokea CCM?
Mbona Mikutano yake na jinsi watu inavyo jaa, ni kama Tu Ile mikutano anayoifanya waziri mkuu Majaliwa?
Mitaani watu wengi ukiwahoji, wanasema kwamba, Mgombea uriais kupitia Chadema, atashindana, lakini kushinda atashinda wa CCM
Nimalizie kwa kuuliza, je, ni kwa kigezo kipi kinachowapa wanachadema waseme Chama Chao kitamwangusha Magufuli?