Eminem ndiye rapper bora kuwahi kutokea, kikwazo ni rangi

Hapo Kwa kanye, 50 zote chai
 
1. Christopher Wallace a.k.a Biggie smalls , notorious, B.I.G or Biggie.
2. Makavelli
3. Hov, Hova, Jigga, Shawn Carter, Jay Z
4. Eminem
5. Nas
 
Niliiona hiyo ilikuw kwenye big Sunday live ya wasafi FM

Nikki alitulizwa na hata hivyo cado alifanya kwa heshima sio kwa ule uwezo wake rasmi hiyo yote coz anamuheshimu sana Mbishi.
So na wewe upo serious unataka kumfananisha unju na hao watoto kisa hile show
 
Wanaosema kwamba vifo vya Pac na Big ni vikubwa kuliko muziki wao nawatangaza kama AIBU YA KWENYE HIPHOP. Hao jamaa walifanya maajabu yao katika umri mdogo... watu kama hao hutokea mara chache sana. Kwa mfano Bob Marley naye alifariki akiwa bado mbichi kabisa ila aliyoyafanya yanaishi hadi leo. Kwa pamoja tuelekee You Tube tukaangalie LIVE shows za hao miamba wawili halafu tuje tujadili ni marapa wangapi wenye energies walizokuwa nazo.
 
Wengi awajawasikiliza hao watu serious ndomaana unakuta mtu anajisemea tu
 
Dunia inabadilika sana na ladha ya muziki inabadilika miongoni mwetu pia
Kizazi cha sasa sio rahisi kujua ukubwa wa kazi za akina Tupac Big Rakim nk

Eminem ni mtundu sana kwenye kurap na anafanya vizuri sana sokoni lakini yupo soft na ni aina ya wanamuziki wanaobenwa sana na maendeleo ya teknolojia kuzipa nyimbo zao upekee

Magwiji wa mambo ya hip hop kwenye vyanzo vyao vya kuaminika nadhani wote Em hayupo kwenye top 5 wachache wamemuweka kwenye top ten

Kwangu mimi Nas ndio GOAT wa ukweli aliyebakia anaishi

Kwa bahati mbaya sana miziki ya siku hizi kwa kiasi kikubwa inapimwa tu mainstreams kama mauzo na streaming
Ndio maana hata sasa kuna kizazi kinaanza kutuaminisha Lil Nas X ndie atakua Raper bora kabisa kuwahi kutokea sababu ya kazi zake zinavyopokelewa kwa ukubwa
 
Nas.....
Namkubali, ila nyimbo zake nyingi ni harakati za mtu mweusi( kama sio za watu wa hali ya chini)....
Eminem yupi ambaye yuko soft mkuu?

Eminem yupi anayebebwa na maendeleo ya Teknology? ( Album bora kwangu ni The Eminem Show, je ilibebwa na maendeleo ya Technology?)

Eminem yupi huyo ambaye anakimbiza kwa streams tu, Eminem ashakuwa star kipindi ambacho DVD hazipo bongo ( na kama zipo ni kwa uchache)....
Unafahamu mauzo ya albums zake ( hard copy), mpaka useme ni streams tu ?
Eminem anajua acheni masihara Nyie......
 
Narudia tena ni kweli Eminem anafanya vizuri sana SOKONI ntakupa sababu

Watu tunakataa ubaguzi wa rangi lakini kwanamna ya maisha yetu upo na utarndelea kuwepo hata kama tutajifanya hatuuzungumzi

Mauzo ambayo ndio rekodi za Eminem zinabebwa pia na uzungu wake
Ikumbukwe kuwa Rap ni muziki wa watu weusi na haupendwi na wazungu walio wengi.... ulikua unawatukana wazungu

Eminem alipofanya vizuri akapata audience mbili ya weusi na wazungu wenzake ambao walimsapoti kwa kuona wazungu pia wanaweza kufanya rap inayolingiwa na weusi....... kushindana na Eminem kimauzo utakwama
Manguli kama Nas hakuna mzungu anataka kuwasikiliza
Nas katoa King disease album haijashika kabisa soko lakini Lil Nas X nakimbiza hatari na show zake zote ticket sold out sababu anaimba na kukubalika na mashabiki wa rangi zote

Lakini binafsi nafikiri ingependeza ubora wa Rap utengenishwe kwa vizazi vyake pia, kulinganisha wanaharakati akina Rakim na hawa commercial akina Dreak Em nk inakua sio sawa

Eminem ni mzuri sana lakini kamwe katu abadan hawezi kuwa GOAT
 
Unakubaliana na mimi kuwa Nas, anaimba mziki wa aina moja ( harakati zaidi).....
Kuanzia illmatic mpaka hii ya juzi Kings disease....?
 
Mi kwa Mtazamo wangu Em ni Mkali sana kla Rangi yake ni Kikwazo...Rakim,KRS one na watu kama Eric Sermon ni wazuri sana Eminem anawazidi ubunifu speed na Rythims...!
 

Vutu vyote ulivyoviweka hapo Tupac alishaviimba tena kwa ubora wa hali ya juu,umeshawahi kweli kusikiliza nyimbo za Tupac au unaongea kishabiki tu?
 

Jamaa anaonyesha hajawahi kwasikiliza kina Tupac na B.I.G maana kuwafananisha na Eminem ni matusi makubwa sana kwao Eminem hajawapita kwenye sehemu yoyote ile wala kuwafikia.
 

Thread iishie hapa.
 

You are spitting facts.
 
Kwangu mm sijaona wa kumlinganisha na Tupac mpaka sasa hivi, hapa nasikiliza kitu Life goes on

Halafu nyimbo kama life goes on,how long will they mourn me,troublesome etc sio popular huku TZ lakini ni moja kati ya nyimbo kali za Tupac,hawa watu hawamjui bhana Tupac ndiyo maana wanamlinganisha eti na Eminem.
 
Hapana angalia show zake live
 
Halafu nyimbo kama life goes on,how long will they mourn me,troublesome etc sio popular huku TZ lakini ni moja kati ya nyimbo kali za Tupac,hawa watu hawamjui bhana Tupac ndiyo maana wanamlinganisha eti na Eminem.
Kwanini sio popular.....?
 
Hapana angalia show zake live
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…