Emmanuel Tutuba ateuliwa na Rais Samia kuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:-

1) Amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Bw. Tutuba anachukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza kipindi chake.

2) Aidha, amemteua Dkt. Natu El- Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Undeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).

Dkt. Mwamba anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel M. Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu.

Teuzi hizi zinaanza mara moja.

View attachment 2472348
Bado Kassim Majaliwa subirini ngojeni baraza la mawaziri livunjwe naye atemwe ila Samia anatupeleka pabaya japo mnashangilia kila teuzi zikifanyika. Hivi hao mgambo wapo tuu wakiangalia haya??
Ulitaka uteuliwe wewe?
 
Hivi Gavana wa BoT na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nani mkubwa wa cheo?

Gavana wa benk kuu cheo kikubwa sana, gavana ana report kwa Rais apitii wizarani.

Katibu mkuu haingii kwa gavana kivyovyote

Ni sawa na ulinganishe katibu mkuu wa wizara ya ulinzi. Na mkuu wa majeshi CDF nani yupo juu

Ama ulinganishe katibu mkuu wizara wa mambo ya ndani na IGP nani yupo juu ?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Keki ya kula watu milioni 60 sio mchezo kuigawanya kwake.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Si unaona, wengine watabahatika kuila na wengine wataikuta kwenye ubwabwa na kunao watakaokosa kabisa hata kwenye ubwabwa. Watu wawe na shukrani hata kwa kuwaona wengine wakiila.
 
Bado Kassim Majaliwa subirini ngojeni baraza la mawaziri livunjwe naye atemwe ila Samia anatupeleka pabaya japo mnashangilia kila teuzi zikifanyika. Hivi hao mgambo wapo tuu wakiangalia haya??
Una matatizo ya akili wewe,kwani huyo Kasim atakuwa PM wa kwanza Kupigwa chini?

Pabaya kiaje? Kisa Kupigwa chini kwa Royalists wa Mwendazake? Endeleeni kuugulia.

Bado Kadogosa wa TRC
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:-

1) Amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Bw. Tutuba anachukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza kipindi chake.

2) Aidha, amemteua Dkt. Natu El- Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Undeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).

Dkt. Mwamba anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel M. Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu.

Teuzi hizi zinaanza mara moja.

View attachment 2472348
Yule jambazi wa maduka ya pesa za kugeni kule Arusha yametimia? Mungu ni mwema.
 
Sisi wengine kazi yetu kila siku ni kupongeza tu wale walioteuliwa! 😇
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:-

1) Amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Bw. Tutuba anachukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza kipindi chake.

2) Aidha, amemteua Dkt. Natu El- Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Undeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).

Dkt. Mwamba anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel M. Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu.

Teuzi hizi zinaanza mara moja.

View attachment 2472348
Bora professor wa makinikia kaondoka zake, ujinga mtupu teuzi za Magu
 
Nini mandate ya BOT?,hiki chombo kitakua muhimu kama kitaendeshwa bila ya urasimu wa serikali, serikali ijiondoe kabisa katika uendeshaji WA BOT, wakiwa huru wapewe jukumu kubwa la kulinda sarafu yetu ili thamani yake against major world currencies iwe kubwa
Ujinga gani huu. Unafikiri BOT wakiachwa bila kudhibitiwa na serikali ndio watasaidia uchumi wa nchi kama yetu?
Sisi sio uingereza bhana. Hata hapo south afrika bank kuu iko huru na hisa ni makaburu ila inasaidia nini kukwamua uchumi kutoka mikononi kwa makaburu?
Awamu ya kwanza hadi ya tatu BOAT walikua kama kisiwa serikali haingilii. Bila shaka kama hamjui ni wizi mtupu ulikua unafanyika. Yule mbunge wa butiama kofia tarabushi mwenye firm ya sheria kapiga kupindukia pale benki kuu. Jpm alivyokuja kumbana akasusa ubunge akakimbilia kuishi miami marekani na wanae kula matunda ya ufisadi.
Mnakumbuka daudi balali awamu ya tatu mkapa alimleta toka marekana ndio tukaona madudu ya kutisha. Kina ande chande yule mhindi ndio wakawa wanapanga mambo benki kuu.
Mlaumuni jk kwa mengine lakini alikataa eti uhuru wa benki kuu kwa nchi kama yetu na kuanza kudhibiti mambo pale.
 
Back
Top Bottom