Emmanuel Tutuba ateuliwa na Rais Samia kuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT)

Emmanuel Tutuba ateuliwa na Rais Samia kuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT)

Luoga alikuwa pale kimakosa,sidhani kama anajua hata balance sheet ni.nini,
Sheria ya benki kuu imesema Ili uteuliwe kuwa Gavana wa benki kikuu unatakiwa uwe na degree ya economics, finance, banking,au Law
Gavana wa benki kuu anasaidiwa na deputy governors SI chini ya watatu Kuna anayehusika na utawala, financial stability nk
 
Nini mandate ya BOT?,hiki chombo kitakua muhimu kama kitaendeshwa bila ya urasimu wa serikali, serikali ijiondoe kabisa katika uendeshaji WA BOT, wakiwa huru wapewe jukumu kubwa la kulinda sarafu yetu ili thamani yake against major world currencies iwe kubwa
Ujinga gani huu. Unafikiri BOT wakiachwa bila kudhibitiwa na serikali ndio watasaidia uchumi wa nchi kama yetu?
Sisi sio uingereza bhana. Hata hapo south afrika bank kuu iko huru na hisa ni makaburu ila inasaidia nini kukwamua uchumi kutoka mikononi kwa makaburu?
Awamu ya kwanza hadi ya tatu BOAT walikua kama kisiwa serikali haingilii. Bila shaka kama hamjui ni wizi mtupu ulikua unafanyika. Yule mbunge wa butiama kofia tarabushi mwenye firm ya sheria kapiga kupindukia pale benki kuu. Jpm alivyokuja kumbana akasusa ubunge akakimbilia kuishi miami marekani na wanae kula matunda ya ufisadi.
Kuna yule daudi balali mkapa alimleta toka marekani. Pale BOAT wahindi matajiri wakiongozwa na andy chandy ndio wakawa wanapanga mambo. And then mtakumbuka ile kashfa kubwa ya epa.
Mlaumuni jk kwa mengine lakini alikataa eti uhuru wa benki kuu kwa nchi kama yetu na kuanza kudhibiti mambo pale.
 
naona Rais Hassan ameanza kuheshimu wenye uzoefu na weledi kuliko taaluma za vyeti peke yake, ni jambo jema sana, uprofesa bila skills na experience kiutendaji ni bure tu wengi angle ya leadership na management ni weupe sana, hata standing order ya serikali wanaenda kuiona na kuanza kuisoma baada ya hzi teuzi
 
Hongera sana tutuba hua hana mambo mengi sana atafanya vizuri huko benki kuu
 
PhDs tunatambuana kwa teuzi.
 
Hivi Gavana wa BoT na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nani mkubwa wa cheo?
Nilitarajia hili swali kuulizwa. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ni PST na PMG (mwenya hazina na mlipaji mkuu). Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ndiye anaidhinisha malipo yoote ya Serikali na kumuamuru Gavana atoe hela. BOT, TRA ni Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na bosi wao ni Katibu Mkuu. Hivyo KM ni mkubwa kuliko Gavana (plz msiniulize kuhusu fulusi).
 
Back
Top Bottom