jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,540
- 25,834
Wanajamvi,
Kama kwenye Taifa kuna mtu au kikundi cha watu ambao wako juu ya Sheria na Katiba, basi Taifa hilo siyo huru. Bali litakuwa linaongozwa na kundi hilo.
Ngoja kitu kimoja tulivyokuwa wajinga kama Taifa. Na ujinga siyo tusi, maana unafutika, ila ni adui mkubwa wa maendeleo tokea uhuru. Mwalimu alisema maadui wakuu ni “ujinga na maradhi”, mara baada ya kupata uhuru. Lakini kama ilivyo kwa umasikini, tatizo hili nalo bado liko.
Kwamfano, wengi wanatetea haya yanayoendelea nchini, lakini hawajiulizi maswali ya msingi kabisa. Maana “The devil is always in details”. Yani hili sakata la hawa wabunge, ni kwasababu tu ya wale waliokuwa wakiitwa “mabeberu” wakati huo huo kura zinaibiwa! Ndo ushangae ujinga uliopo. Kama uchaguzi unaiba, kelele za nini sasa kama siyo sawa na kula na kipofu kisha ukamkamata mkono?
Sasahivi, hao mabeberu, ndiyo wahisani. Na hili hao wahisani waendelee kutoa misaada, hizo kamati za ndani ya bunge, huwa zinatakiwa kuongozwa na wapinzani. Yani beberu huyo huyo ambaye apingwa kila siku, ndiyo huyo huyo anayetaka kuwepo na uhakikishwaji wa matumizi bora ya pesa zetu? Sasa ili hizo kamati ziwe na “wapinzani”, ambao huwa ni kama “watchers”, ama wanaohakikisha hakuna kona kona, ndiyo hili sakata la hao COVID-19 waliofutwa na CHADEMA.
Yale makashfa ya EPA, RICHMOND, MEREMETA, KIGODA, BUZWAGI na nyingine nyingi, ndizo zilizosababisha hao wahisani wahitaji hizo kamati ili tuweze kujisimamia dhidi ya mafisadi wanaodai eti ni wazalendo na wanaohoji ni wasaliti na propaganda nyingine za kijinga kabisa ambazo zimechota wengi akili. Very sad. Lakini in the end, time always is the factor!
Kwa mfano, Kuna watu kama kina Pascal Mayalla ,wanatumia neno “sovereignty”, kila wanapoitetea serikali pale inapokuja kwa wahisani ama mabeberu, kuulizia kuhusu utawala wa kidemokrasia. Lakini pengine hawafahamu maana halisi ya “sovereignty”
“Sovereignty, in political theory, the ultimate overseer, or authority, in the decision-making process of the state and in the maintenance of order. ... Derived from the Latin superanus through the French souveraineté, the term was originally understood to mean the equivalent of supreme power.”
**noun
supreme power or authority...
"how can we hope to wrest sovereignty away from the oligarchy and back to the people?"
So obviously, sovereignty of any free nation, lays with the people! Period!
If people have no say, no sovereignty, no freedom. Simple!
Tunaposema... “Taifa hili ni huru”, na kwamba lina “sovereignty”, yani haki ya kujitawala na kujiamulia mambo yake yenyewe, halafu wananchi wasiwe huru kwenye kuwapata hao viongozi wanaosimamia “sovereignty” yao, basi neno “sovereignty” halina tena maana yoyote ile haswa kama unadai kufuata utawala wa kidemokrasia.
Ndiyo maana mataifa makubwa huwa yanaenda kuwasaidia wananchi kwenye mataifa ambayo yako hivyo na wananchi hawana “sovereignty” yao. Haya yanapotokea, hata UN wanahalalisha. Ni suala la utambuzi kwa kiasi kikubwa. Kwahiyo mfano hawa tunaowaita mabeberu, wanapokuwa wanafanya maamuzi, huwa wanazungumzia hilo la wananchi kuwa ndiyo source of power. That is possible only with a free and fair elections. That becomes possible with a new constitution from the people by the people.
Lakini pamoja na yote, bado mengi yatakayolipata taifa, ni ya kujitakia tu!
Mambo mawili wamekosea.
1. Kama walijuwa watashinda ije mvua lije jua, wasingehangaika na propaganda za mabeberu na kuwatukana nk.
2. Kama walikuwa na uwezo wa kujipatia wabunge wote, basi walikuwa na nafasi ya kuwaachia wapinzani majimbo.
Hapo wa kulaumiwa ni nani?
Mimi ninavyohisi, usalama wa Taifa ulimsikiliza boss mkuu kwasababu anataka amalizie miradi yake mikubwa kwa Taifa, na anataka sapoti ya bunge kuweza kufanya anayoyataka. Matokeo yake, wakampatia majimbo yote bila kuuliza maswali. Ndiyo shida ya katiba yetu ya sasa na madaraka aliyonayo rais, ambapo hata iweje huwezi kuhoji. Anachotaka rais, anapatiwa by any means necessary.
Kama alifurahishwa na ule Uchaguzi wa serikali za mitaa, na alikuwa akifurahia wale wabunge wa CCM kupita bila kupingwa baada ya kina Mahera kuwaondoa wale wagombea wa upinzani. Sasa hapo ni nani aliye chini yake, au taasisi yoyote iliyopo chini yake itakayoacha kufuata hayo hayo ya kumfurahisha mkuu hata kama Taifa ndilo linaingia gharama? Ukitaka kujuwa demokrasia ya kweli, shangaa Trump anapodai kuwa FBI wamehusika kuhakikisha hapati ushindi! Hayo ni maajabu makubwa sana ukilinganisha na sisi! Hakuna “balance and checks”.
Watu wa nje wanatushangaa sana. Na wengine tunawashangaa sana wale wanaoona ni sawa tu na kwamba maisha yaendelee!
Sasa mfano kauli kama zile kuwaambia wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwa “haiwezekani wapinzani washinde na wakati yeye ndiye anayewalipa”! Kama tungekuwa taifa la maana na uhuru wa taasisi zetu uzingatie maslahi ya Taifa, basi hata hao usalama wa Taifa wangemshauri mkuu ili mambo yasiende kombo “kwa maslahi ya Taifa”