Eneo lililo wazi pembezoni mwa Barabara ya Morogoro linaweza kufanyiwa biashara na likazalisha pesa nyingi kwa serikali

uperiti

New Member
Joined
Mar 9, 2023
Posts
4
Reaction score
6
Je, Waziri wa fedha anahangaika kutafuta kodi wakati eneo hilo la pembezoni mwa barabara ya Morogoro lililo wazi linaweza kufanyiwa biashara na likazalisha pesa nyingi sana kwa serikali?

Kwani huyu Daktari wa uchumi hawezi kushauriana na Waziri wa Ujenzi wakawatumia wataalamu wa Mipango miji na Wasanifu majengo wa Chuo Kikuu Ardhi wakatengeneza/wakabuni biashara mbali mbali za kufanya kwenye maeneo hayo na serikali ikakusanya kodi?

Ushauri wangu ni kwamba watafutwe wataalamu wabuni namna ya kutumia maeneo hayo kwa kujenga structure ambazo siyo za kudumu kama kutumia makasha ya mizigo (containers), Mbao, mirunda n.k.

Wanaweza kutengeza bustani nzuri za kupumzikia zikiwemo sehemu za burudani mbalimbali. Yawekwe masoko madogo madogo kila kituo kama vile stop-over, suca, temboni n.k Naamini wakipewa wataalamu hii kazi serikali inaweza pata pesa nyingi sana.
 
Hizo ni road reserves, zitakuja kupanuliwa mabarabara zote hizo. Barabara zetu ni ndogo sana ukilinganisha na nchi zilizoendelea.
 
Back
Top Bottom