Eng. Hersi ajiuzulu nafasi yake ya urais kwa kututusi sisi wanayanga!

Eng. Hersi ajiuzulu nafasi yake ya urais kwa kututusi sisi wanayanga!

Kama GSM mwenyewe ametulia na anakula mabaga,mapiza,mayonaizi ,makoronya,matambi,ma eggs chop,makababu na machapati chapati na amewekeza Bs ametulia tuli iweje wewe mla mihogo unalalamika?
Tengua kauli yako King Kong III inamaana nikila mihogo siruhusiwi kuchangia hoja yoyote ile juu ya klabu yangu?
 
Mmeshauza timu hamna chenu, Yani mmepewa mihogo mkaachia timu.
 
Naona umekuja kutimiza ibada.😃😃
Cc adriz
Tumedhalilishwa sana sisi mashabiki wa yanga. Mihogo ilivo mizuri na ina afya tele, wanga wakutosha na bado tuonekane hatufai kisa tunashindia mihogo 🥺 inauma sana tena sana.
 
Mantiki kwamba aliyewekeza Bs halalamiki ,iweje wewe haujawekeza hata senti 5 ya nyerere na mla mihogo ulalamike?
Kabla ya gsm yanga ilikuepo na hata akiondoka yanga itakuepo. Yanga mi mashabiki wake ndio maana tunajivunia klabu yetu na ndio fahari ya Tanzania. Hersi kama amekosea lazima ajiuzulu nafasi yake kwa maana watu wanawekeza kwasababu ya mashabiki. Kwanini wasingeenda kuwekeza kmc au toto africans?
 
Kitendo cha raisi wa klabu yetu pendwa ya Young Africans au yanga kutuita sisi mashabiki wake wala mihogo, ni kutudhalilisha, kutufedhehesha, kutudharau na kutuona hatuna maana. Inauma sana kwa kweli leo hii sisi ni wakuitwa wala mihogo ambao hatufai kuchangia chochote kisa tumekula mihogo. Na je vipi kuhusu wanachuo wanaoshindia mihogo kwa wingi wao nao hawana nafasi pale yanga kisa mihogo. Mihogo kama chakula kizuri cha wanga kimedhalilishwa na Eng.Hersi raisi wa yanga kuwa muungwana ujiuzulu nafasi yako tutafte raisi mwingine ambaye atakuwa ni muungwana asiye na kashfa na sio kutudhalilisha sisi mashabiki wake.
Hakuna tusi hapo.
 
Kabla ya gsm yanga ilikuepo na hata akiondoka yanga itakuepo. Yanga mi mashabiki wake ndio maana tunajivunia klabu yetu na ndio fahari ya Tanzania. Hersi kama amekosea lazima ajiuzulu nafasi yake kwa maana watu wanawekeza kwasababu ya mashabiki. Kwanini wasingeenda kuweka kmc au toto africans?

GSM ndio mwenye uchungu ,mbona enzi za papa zahera tulikuwa tunatembeza bakuli? Eng yupo sahihi kutoa hiyo kauli kwa mashabiki maandazi(feki fans -shabiki wa makolo) wanaojifanya ni yanga....Mimi ni yanga lakini sijaona tatizo kwa kauli ya eng.
 
Kwa kifupi kinachowakuta mashabiki wa Yanga SC naweza kusema mmevuna mlichopanda.

Huyo Hersi mlimchagua kwasababu ya pesa zake, naamini hiyo ndio sababu kubwa..

Nae akajua hawa wachovu wamenichagua kwa kishindo sababu ya pesa zangu, sasa leo amewaita wala mihogo msikasirike, kiukweli mihogo ndio chakula chenu kikuu hata kabla Hersi hajaja.

Ningewashauri tu, kwanza muoneshe heshima kwa mihogo iliyotajwa, lakini pia, mumshukuru bosi wenu kwa kujua chakula chenu kikuu ni kipi, kumbuka mihogo ndio iliwalea kabla Hersi hajaja Yanga.
Ulitaka achaguliwe masikini? mpira ni pesa
 
GSM ndio mwenye uchungu ,mbona enzi za papa zahera tulikuwa tunatembeza bakuli? Eng yupo sahihi kutoa hiyo kauli kwa mashabiki maandazi(feki fans -shabiki wa makolo) wanaojifanya ni yanga....Mimi ni yanga lakini sijaona tatizo kwa kauli ya eng.
Tatizo lipo kwenye kauli kwamba wala mihogo hatupaswi kushauri chochote katika yanga. Na GSM kuwekeza ni kwasababu ya mashabiki wa yanga hivo anajua kuna profits anazozipata hakuna mtu ambaye anawekeza bila kutarajia faida. Hersi ametukosea ajiuzulu nafasi yake waje wengine ambao watatambua umuhimu wa mashabiki katika klabu.
 
Mashabiki ni vinyonga ,deal na wafuasi tu.(Royal fans)....Mashabiki hawataki kuambiwa ukweli ,mashabiki wanataka timu ifunge tu.
 
Huu ni ushabiki Maandazi, kama kweli mngekua mmeguswa mngekemea siku ileile mlipopata matokeo chanya.

Hersi alikosea na alifaa kukemewa mapema lakini siku ile ilionekana utani wa kawaida mpaka mliposhindwa pata matokeo ndio ikaonekana tusi.
 
Tafadhali sana tengua kauli yako na utuombe radhi sisi mashabiki wa yanga. Kwahyo sisi mashabiki wa yanga tunakula chakula cha nguruwe.
Sio mbakula chakula ya nguruwe. Ninyi ni nguruwe kasoro mkia hahahaa
 
Tunakataa hatuli mihogo wakati tupo busy na mihogo nani anakula Pizza au burger kama sio mihogo hii hii tena inapakiwa rangi eti Chips dume...
 
Kitendo cha raisi wa klabu yetu pendwa ya Young Africans au yanga kutuita sisi mashabiki wake wala mihogo, ni kutudhalilisha, kutufedhehesha, kutudharau na kutuona hatuna maana. Inauma sana kwa kweli leo hii sisi ni wakuitwa wala mihogo ambao hatufai kuchangia chochote kisa tumekula mihogo. Na je vipi kuhusu wanachuo wanaoshindia mihogo kwa wingi wao nao hawana nafasi pale yanga kisa mihogo. Mihogo kama chakula kizuri cha wanga kimedhalilishwa na Eng.Hersi raisi wa yanga kuwa muungwana ujiuzulu nafasi yako tutafte raisi mwingine ambaye atakuwa ni muungwana asiye na kashfa na sio kutudhalilisha sisi mashabiki wake.
Kwani mihogo ina shida gani, mbona ni chakula kizuri tu! Au angewaita wala chipsi
 
Back
Top Bottom