Eng Hersi: Kuna namna timu fulani ilijipa utawala wa nchi, Nitawanyoosha

MwananchiOG

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
1,970
Reaction score
4,037
Akiwa kwenye mahojiano yanayorushwa kupitia EATV katika kipindi cha Salama na Rais wa Yanga Engineer Hersi, Amesema kuna club ilikuwa imejipa utawala na kujiona wao ni vichwa. Sasa alikuwa kwenye mpango na bado yupo katika mipango ya kuwaonyesha kwamba Yanga ndiyo club kubwa zaidi "Nitawanyoosha" alisema kiongozi huyo wa Yanga ambaye kwa miaka mitatu mfululizo ameirejesha Yanga kwenye utawala wake na kuifikisha katika orodha ya vilabu 10 bora barani Afrika.

Hii inaonyesha Rais wa Yanga amepania na bado yupo kwenye mkakati wa kuifanya Yanga kuwa club ya mfano Afrika Mashariki na Afrika kiujumla.

Huenda miaka kadhaa ijayo tukashuhudia yale ya Al Ahly kumuacha na kumpoteza kabisa katika ramani za soka mpinzani na mtani wake Zamalek fc
 
Kitendo cha Eng Hersi kuwepo uwanjani kila mechi kinaakisi ni kwa kiwango gani anaipenda Yanga na ana mipango mikubwa na Yanga maana huna cha kumwambia ni mchezaji gani Yanga hajitumi au ni kivuruge, kila kitu anaona mwenyewe.

Ni hakika Hersi atamnyoosha Karai na simba yake mpaka makolo maji waseme mma!!

Hii Yanga ya Eng Hersi inakera mno, kuifunga ni lazima utumie marefa au kalumanzila!!
 
Na atawanyoosha kweli huyu jamaa

Simba pale hakuna aliye serious hayupo yaani hata kama isingekuwa ni yanga azam angewannyoosha sana Simba, nadhani sio kwamba Yanga ni wazuri sana ila kwa sababu simba ni wabovu sana hawana nafuu yaani Simba Kuna wahuni wengi sana

Yanga walivyohitaju kuwa serious walifukuza wapigaji, wazee wote na wajanjajanja wa ten percent ndo akaingia kichwa hersi saidi kama Barbara angebaki Simba ingekuwa inaogopesha sana
 
Akiwa kwenye mahojiano yanayorushwa kupitia EATV katika kipindi cha Salama na Rais wa Yanga Engineer Hersi, Amesema kuna club ilikuwa imejipa utawala na kujiona wao ni vichwa. Sasa alikuwa kwenye mpango na bado yupo katika mipango ya kuwaonyesha kwamba Yanga ndiyo club kubwa zaidi "Nitawanyoosha" alisema kiongozi huyo wa Yanga ambaye kwa miaka mitatu mfululizo ameirejesha Yanga kwenye utawala wake na kuifikisha katika orodha ya vilabu 10 bora barani Afrika.

Hii inaonyesha Rais wa Yanga amepania na bado yupo kwenye mkakati wa kuifanya Yanga kuwa club ya mfano Afrika Mashariki na Afrika kiujumla.

Huenda miaka kadhaa ijayo tukashuhudia yale ya Al Ahly kumuacha na kumpoteza kabisa katika ramani za soka mpinzani na mtani wake Zamalek fc
Asimamie utopolo wake aache taarabu za kisomali
 
Aache kauli za kipumbavu. Hana mamlaka ya kuinyoosha simba. Ni suala la muda tu simba itarudi kwenye ubora wake na mtaanza malalamiko yenu ya kumlalamikia Karia na tff yake na sijui ataficha wapi sura yake huyo msomali.
 
Tunaomba Rais aongezewe ulinzi.
 
Aache kauli za kipumbavu. Hana mamlaka ya kuinyoosha simba. Ni suala la muda tu simba itarudi kwenye ubora wake na mtaanza malalamiko yenu ya kumlalamikia Karia na tff yake na sijui ataficha wapi sura yake huyo msomali.
Namba huwa hazisemi uongo Yanga 7- 2 Simba ni mnyoosho wa maana. Kwani mbumbumbu mnataka mnyooshweje? Kumi bila? Hata Mamelodi walinyooshwa refa akaokoa jahazi.

Eng Hersi kuinyoosha Simba na Karai TFF sio kwa hiari yenu bali kwa nguvu, na mjue kero ya mabango ya ushindi na chopa vitaendelea!!

Mchezaji mmoja tu kama Aziz Ki ni zaidi ya safu nzima ya kushambulia ya my wetu, je ni mchezaji gani Simba ana uwezo kama Aucho? Kwanini msinyooshwe tu!!
 
Aache kauli za kipumbavu. Hana mamlaka ya kuinyoosha simba. Ni suala la muda tu simba itarudi kwenye ubora wake na mtaanza malalamiko yenu ya kumlalamikia Karia na tff yake na sijui ataficha wapi sura yake huyo msomali.
2021 - kauli ilikuwa hiyohiyo
2022- kauli ilikuwa hiyohiyo
2023- kauli ilikuwa hiyohiyo
2024- kaulimbiu ni hiyohiyo! Huo muda labda mpaka 2072 😄
 
Kwa uhuni wa viongozi waliopo Simba kina Mangungu na Try Again wake Hersi atawanyoosha kweli. Pal hakuna uongozi, kuna uozo tu. Timu haiwaumi wala njia mpya hawana. Labda wawekwe pembeni, vinginevyo ni mnyoosho hadi huko miaka ya mbele kabisa..
 
Simba walikosea sana kutengeneza mazingira ya Babra kuondoka, sasa inawagharimu
Nashangaa Sana wanaomsifia Babra kwani hakuwa na cha ajabu zaidi ya kulinda maslahi ya mi na kutumia Simba kujitangaza binafsi.
Simba imeanza kuyumba baada ya kifo cha Hanspope mtu aliyeweza kupambana na figisu za yanga na Tff. Pia akitaka mchezaji alikuwa hasubiri mo atoe pesa.
 
Aache kauli za kipumbavu. Hana mamlaka ya kuinyoosha simba. Ni suala la muda tu simba itarudi kwenye ubora wake na mtaanza malalamiko yenu ya kumlalamikia Karia na tff yake na sijui ataficha wapi sura yake huyo msomali.
Kwa viongozi hawa ni kujidanganya tu.
Tuna watu wasio na mapenzi na simba wao wanaangali maisha yao zaidi
 
Back
Top Bottom