Ni kweli unachokisema kiongozi. Iko hivi anaposema muajiriwa anamaanisha yupo kwenye payroll ya Yanga kitu ambacho siyo kweli yeye hayupo kwenye roster ya wanaolipwa mishahara kila mwezi au mkataba. Kwenye governance inakuwaga hivi bosi. Mfano CRDB ina wafanyakazi na wasiowafanyakazi ila wanawasimamia wafanyakazi. Hii tunaiitw bodi ya wakurugenzi. Kwenye bodi kuna waajiriwa wa CRDB (wana mikataba) na wengine siyo waajiriwa wa bank (hawana mikataba na hawapo kwenye payroll). Kinachotokea huwa ni wahusika ambao siyo waajiriwa hulipwa kama posho (remuneration-director fee etc) kwa muda fulani inaweza kuwa kila baada ya miezi sita etc, na wanapohudhuria vikao wanalipwa. So alichokisema Eng. Hersi ni kipo hivyo, siyo kabisa mwajiliwa ila ni mtendaji anayelipwa posho au fee inategemea wao yanga wataitaje. Aina hii ya governance husaidia kuwasimamia waajiriwa na lengo la kina Hersi ni kuhakikisha wanasimamia maslahi ya wanachama na ndiyo maana haiwezekana wawe waajiriwa watashindwa kusimamia hao waajiriwa wa yanga na hii iko kisheria zaidi bosi. Hata CRDB bodi ya wakurugenzi kazi yake ni kuisimamia management na ndiyo maana siyo waajiriwa. Nadhani nimeeleweka