Wewe unaleta ubishi usio na maana! Marais wa Vilabu mbalimbali duniani Sio Waajiriwa wa Vilabu, na kwahiyo HAWAPO kwenye payroll! Kwa mfano leo hii Uto wakipigwa na mtikisiko wa kiuchumi, ikifika mwisho wa mwezi Mzee Mtime atakuwa na haki ya ku-demand mshahara wake, klabu itatoa wapi huo mshahara; yeye haimhusu; na Uto wakishindwa kulipa, hiyo ni bleach of contract na wanaweza kufikishwa mahakamani! Kinyume chake, Hersi hawezi ku-demand chochote kwa sababu mara nyingi hata hizo posho hulipwa ili kufanikisha kazi fulani, mathalani ya vikao, n.k! Kwahiyo kama Klabu itakuwa haina pesa ya kulipa hata posho za vikao basi ni ama klabu ipunguze idadi ya vikao au Wajumbe wajitegemee wenyewe kwa sababu HAKUNA hata mmoja ambae aliahidiwa malipo yoyote. Sasa wakati Hersi na wenzake wanaamua kufanya 100% charity work kwa mali yao, Mtine na watu wake watakuwa na haki ya kufungasha virago kwa sababu, awali ya yote, hawa walipewa mkataba wa kazi wenye ahadi ya mshahara wa kila mwezi. Na kubwa zaidi, hawa hawatakiwi kufanya kazi nyingine yoyote itakayoingiliana na ajira yao kwenye klabu lakini Hersi na wajumbe wake, wanakuwa na kazi zao na ndo maana kukutana kwao kunakuwa ni siku maalumu tu, na mara nyingi itakuwa weekend ili kazi za Yanga zisiingiliane na kazi zao za kila siku! Hata pale Unyamani, IPO HIVYO. Mangungu kilichompeleka pale ni "kiherehere" chake cha mapenzi kwa klabu kwahiyo hawezi kuwa na mshahara!