English Medium ziko Ovarated sana. Hakuna elimu pale zaidi ya utapeli. Shida ni tumekuwa Brainwashed sana

Sijakuelewa mkuu hapo, tutie effort form 4 au form 1 mpk 4?
 
Tatizo watz wengi ni kudhani kuwa kujua English ndo kuelimika.
Ndio ni kuelimika

Kujua kutumia lugha yoyote ni kuelimika ila kujua lugha ya kimataifa kama Kiingereza ni kuelimika zaidi na kuweza kupata fursa zaidi
 
Ndio ni kuelimika

Kujua kutumia lugha yoyote ni kuelimika ila kujua lugha ya kimataifa kama Kiingereza ni kuelimika zaidi na kuweza kupata fursa zaidi
Kwani walio somea kwenye hizo shule mnazo ita kayumba wao hawajui kiingereza?
Leo hii tukienda vyuoni unaweza kutofautisha kati ya walio somea kayumba na hizo EMS?
Uganda na Zambia lugha yao ni kiingereza sasa niambie wana kipi cha ajabu zaidi ya kunuka njaa?

Ni upumbavu wa hali ya juu kulipia ada ya 4,000,000 kwa miaka 7 eti mtoto wako ajifunze kiswahili ,hali yakuwa unaweza kujifunza hicho kiingereza kwa Simba kwa laki 3 ndani ya miezi 4 tu.
 
Nadhani mazingira ndo yanawafanya watu wafikie hayo maamuzi pia lugha ya kiingereza.


Sifikirii Kama mtu umebarikiwa uwezo unaweza kumpeleka mtoto shule ambayo haina miundombinu mizuri Kama madarassa , choo, chakula na usafiri.

So ubora wa Elimu utabidi uutengeneze wewe mzazi Kwa kuhakikisha unamjemga mtoto katika Elimu ya kujitambua , kujituma kujihamini na kujua lugha mbali Mbali za kimataifa.

Pia mwisho network inasaidia mtoto aliyesoma IST sifikirii Kama atakosa kukutana na potential people .
 
Niliwahi sema humu Baadhi ya hizi shule huwa hazina mtoto wa mwisho yaani kama Darasa lina wanafunzi 40 huwezi ona mtoto wa 40, wanaishia namba 10 na na wanadaia wamefungana. Namba 1 unaweza kuta watoto 10 huu mchezo wazazi hawajaushitukia.
Achana na mitihani hiyo ya ndani ambayo wanashindana wenyewe kwa wenyewe. Unatakiwa ulete mitihani ya kitaifa ambayo mtu anaweza akalinganisha shule hizo za English Medium (ambazo nyingi ni private) na zile za Swahili Medium (ambazo nyingi ni public). Ukilinganisha hizo, utaweza kuitetea hoja yako vizuri
Hebu tulinganishe ufaulu wa hizi shule mbili, Kivule (swahili) na Zawadi (english) ambazo zote zipo katika kata moja, mtihani wa darasa la saba 2024

 
Hawajui na hata wanaojaribu hawana confidence ya kukizungumza
 
Mitihani sio kipimo cha elimu Bora shituka, nchi nyingi wanaachana na huo ujinga naona nyie bado ndio kiti kinawapa jeuri. Hizo mitijani ndio kabisa zimejaa usanii
 
english medium hakuna kitu pale tunapigwa
 
Hakuna tofauti, hao English nedoum hata seconsary tu wanapoteana huko, hakuna elimu pale tunapigwa
 
Make Kayumba School Great Again Campaign
Hii inawezekana endapo atatokea kiongozi wa kariba ya Julius Nyerere. Miaka ya nyuma hadi kufikia miaka ya 80 mwishoni, mwanafunzi aliyeshindwa kufikisha wastani unaotakiwa baada ya matokeo ya mitihani ya darasa la 7 na Kidato cha 4, ndiye alipelekwa shule za private na mzazi/mlezi. Ilichukuliwa kuwa amefeli.
 
Mleta mada na wengine kama wewe sijawahi kuwaelewa. Unamaanisha hizi za kubeba kidumu na ufyagio tulizosoma sisi ndio bora ama?
 
U
Uzi ufungwe...
 
Narudia tena ni upuuzi wa hali ya juu kabisa kulipa milion 4 ili mtoto haende kujifunza kiingereza ambacho anaweza kujifunzia hata mitaani.
Inaweza kuwa ni upuuzi kwako ila kwa wengine sio
 
Mitihani sio kipimo cha elimu Bora shituka, nchi nyingi wanaachana na huo ujinga naona nyie bado ndio kiti kinawapa jeuri. Hizo mitijani ndio kabisa zimejaa usanii
Taja walau nchi 20 kati ya hizo 'nyingi' ambazo katika formal foundation education hakuna mtihani
 
Mitihani sio kipimo cha elimu Bora shituka, nchi nyingi wanaachana na huo ujinga naona nyie bado ndio kiti kinawapa jeuri. Hizo mitijani ndio kabisa zimejaa usanii
Kama mtihani sio kipimo, kwa nini umelaani kitendo cha walimu wa English medium schools kukwepesha kuweka mwanafunzi au wanafunzi fulani kushika namba za mkiani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…