English Medium ziko Ovarated sana. Hakuna elimu pale zaidi ya utapeli. Shida ni tumekuwa Brainwashed sana

English Medium ziko Ovarated sana. Hakuna elimu pale zaidi ya utapeli. Shida ni tumekuwa Brainwashed sana

Kuna midogo fulani tulianza nayo shule ya vidumu na mfagio miaka hyo... tulipofika darasa la tatu ilikuwa inaongea kingereza kizuri sana..kuna siku walikuja wazungu shuleni kwetu kidogo kimoja kikamwaga ngeli na mmoja katiya wazungu wale..mzungu akakiambia upo vizuri natamani nikuchukue..Sasa unajiuliza huyu dogo wa kidumu na mfagio hyo ngeli kaipata wapi? kumbe ni kipawa tu chakuzaliwa nacho...kwahyo kama English medium mnafata kiingereza sio kweli nimatumizi yako ya pesa tu.
 
Niliwah kufika shule nikajua labda kuna watoto wanapiga ngeli hatar lakin hamna kitu,kwanza walimu wakiona mzazi yupo maeneo ya shule anajifanya kuwaongelesha kiingereza wanafunz na niliona wanafunz hawajibu chochote bali wakawa wanatikisa tu kichwa kama mabubu na kunyoosha mikono kimya kimya
 
Niliwah kufika shule nikajua labda kuna watoto wanapiga ngeli hatar lakin hamna kitu,kwanza walimu wakiona mzazi yupo maeneo ya shule anajifanya kuwaongelesha kiingereza wanafunz na niliona wanafunz hawajibu chochote bali wakawa wanatikisa tu kichwa kama mabubu na kunyoosha mikono kimya kimya
Shule hiyo inaitwaje?
 
Nasomesha Englisha Medoum ila ukweli ni kwamba sijawaji zikubali hizi shule, Shule zimejaa janja janja nyingi sana kuliko kutoa elimu ni full hadaa na wanajua fika kucheza na akili za wazazi wajinga

Sijawaji amini kwamba kuna elimu bora kwenye shule za English medoum, kuna elimu ya kawaida sana na tofauti yake na shiule za Serikali mimi sioni kabisa ukitoa sisi kuwa Barainwashed.

Niliwahi sema humu Baadhi ya hizi shule huwa hazina mtoto wa mwisho yaani kama Darasa lina wanafunzi 40 huwezi ona mtoto wa 40, wanaishia namba 10 na na wanadaia wamefungana. Namba 1 unaweza kuta watoto 10 huu mchezo wazazi hawajaushitukia.

Ukiondoa kupanda Mabasi asubuhi hakuna kingine ambacho nakiona kwa hizi shule. Wengi wanapondea shule za Serikali kwenda na Mifahia na vidumu vya maji ila ni sehemu ya kufundisha watoto na sio adhabu. Ni wazazi wajinga ndio wanao na mtoto kubeba fahioa kwrnda nao shule ni adhabu au ushamba.

Watoro wanakuwa legelege sana, mtoto wa shule ya Serikali anaweza panda Daladala na akenda shule mwenyewe umbali wa km 15 hapa ni mtoto mdogo darasa la 3, hii mtoto wa English medium hawezi, ni sawa na kuku wa Broiler tu. Matoto yanakuwa legelege tu.Basi la shule likiharibika hakuna kwenda shule.

English medium zimejaa janja janja sana, kuanzia kutoa elimu na hadi michango yao ya kihuni. Hakuna Englisha ya maana inafundishwa pale,watoto wanatoka pale wako kawaida sana hakuna maajabu pale.

Kucheza na akili za Wazazi na ziara zao za kwenda vijwana vya ndege kupigisha watoto picha kule ni full ujinga.Wanakuambia ziara za mafunzo, mtoto yuko Baby class anatakiwa atoe sh 50,000 ya ziara ya mafunzo.

Unatoa 50,000/ wanawanunulia watoto chips kavu, biskut na juice za azam, hapo 50,000/ imakata na ni ziara ya ndani ya mkoa. Mtoto anarudi nyumbani full njaaa ukiuliza mtoto anakuambia walitupatia juice, chips na biscut tu.
kweli kabisa, wezi wakubwa, wanauza mpaka vi jersey vya michezo, madarasa ya swimming ni uongo uongo mtupu, vi field trip ni vya kitapeli, Kiingereza chenyewe wanafundishwa na waswahili wenzetu wasiokijua kama sisi.

Lakini kuna maeneo umekosea.

Kwenye elimu, these schools own the NECTA exams. Wanatunga na kumiliki mtihani wa NECTA.

Shule ya mtoto wangu mwaka ulopita wa 2023 wamefanya NECTA watoto 78. Division 2 HAKUNA.

Mtoto wa mwisho, wa 78 kati ya 78 darasani eti na yeye ana WANI!

Kwa hiyo mtoto hata kama anashika namba za katikati darasani au hata wa mwisho, bado huyo ni kenge mzuri kwenye msafara wa mamba wakali sana watakaowinda nae, watakula nae, na watafika pamoja salama. Unakuwa na uhakika anaenda kupata WANI na ATACHAGUA mwenyewe admission ya akasome nini chuo. Unless augue siku ya mtihani.

Shule ambayo haina DIVISION 2, you have to roll out the red carpet for the administrators.
 
English medium ni kwa usalama wa mtoto tu. Mm najiuliza mbona watoto wa kiarabu hawasomi lakin wanaendesha ndinga Kali? Mwaka huu nimeamua kumtoa mtoto huko na kumpeleka kayumba. Then hela niliyokuwa nalipa kule nitakuwa namuwekea kwenye account then at the end nije nione which is better.
 
Tatizo watz wengi ni kudhani kuwa kujua English ndo kuelimika.
Ni ushamba sana kujivuna na lugha ya watu ingali kuna kiswahili lugha nzuri tu,
Kuna jamaangu kila siku namuimbia tofauti ya shule za serikali na e.medium ni lugha tu ila pia wakikutana huko juu hawanaga maajabu kabisa,
Mamilioni yote wazazi tunatoa ili tu mtoto akasome lugha ya kiingereza
Kuna shule moja iko arusha ngulelo na moivaro huko ina upigaji wa hali ya juu saaana,ziara ya kupanda hiace ya 600 x2, na kucheza tu 80,000 kwa mtoto wa baby class

Watanzania tubadilike,tuwaache watoto wasome shule za fagio na vidumu wajifunze mengi nje na shule kama kulima,usafi wake na darasa na mengine mengi,mtoto ajue akiamka afagie na kusaidia kazi yoyote nyumbani mana watoto wamekua laini sana na hivi mnawawekea dada wa kazi
Kazi iko kwenye malezi ya kizazi hiki
 
Hao hawajui wanacho ongelea neendeni vkjijini mjionee hizo shule zakayumba, shule ya watoto 800 ina waalimu watatu matundu ya choo mawili madawati ni tofari za majengo very poor learning environment kama kweli una huruma na mwanao mtafutie shule ya private.
Hiyo English darasa watoto 9 iyo shule sasa! Kumepoa km msibani
 
Enzi zetu kusoma Private school (ukiacha Catholic Seminary schools) ulikuwa ni upimbi. Huko walikuwa wanaenda 'waliofeli'.

Vipanga tulikuwa tunaenda Shule za Serikali. Ajabu eti leo kusoma Private school ni fahari kubwa, duuuuh! 🙆

Mfano;ndugu yangu aliyesoma St.Kayumba Primary (darasani kwao kulikuwa na madawati 2 tu) alikuja kupiga A ya Economics huko Advance, na kuwa Tanzania One (TO) kwa somo la Economics kwa mwaka huo. Na bado pale UDSM akatoka na First class degree - B.A Economics (Hons). Yuko mbele huko anakula maisha.

Halafu wapuuzi wanakwambia ukisoma Kayumba hakuna future. Kwanza nyie wote mlisoma Private? Mbona mmefanikiwa kimaisha?
 
Mie sijashawishika bado otherwise uniambie na yale matokeo ya mitihani ya Necta pia huwa janjajanja
Bado unaamini kwenye matokeo? huko Dunia isha hama kitambo, nchi nyingi ziko kwenye mchakato wa kuachana na huu ujinga na zingine zisha acha.
 
Back
Top Bottom