Hahahaaa,uko wapi Bertha wangu,nakumbuka baada ya kuonana na wewe Iringa Girls wakati wa likizo,nilijitahidi sana kuitafuta chance ya kuongea nawe,ilikuwa ukitetemeka sana japo tulikuwa tumekaa na rafiki yako Agnes,baada ya mazungumzo marefu tuliishia kuagana,wakati tunaagana kila mmoja wetu mikono yake ilikuwa imelowa jasho,(sijui kwanini).
Nikiwa safarini kurudi shule,(Minaki high school) akili yangu yote ilikuwa ilikuwa inawaza Bertha,Bertha Bertha tuuu!!!
Nilipofika shule nikaandika boonge la barua,na dedications za kutosha kama,
1.Show me the meaning the meaning of being lonely.......Backstreet boys
2.Love you more that..,..
Baada ya wiki mbili nikapokea barua ya mrejesho chanya,hahahaaa,nahisi ilichangia mimi kupata div.three aisee,maana asilimia kubwa ya muda wangu nlikuwa nawaza nkikutana Bertha itakuwaje,nikapunguza kazi ya kukoboa PCB.
Bertha na EGM yake akapata div.2,mtu mzima na li-PCB language nikaandika division 3.
Naomba ujinga ule usijirudie kwa wanangu kwa kweli!!!!