ngosha wa mwanza
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 3,832
- 11,964
Hivi kumbe tantaw ni ME.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Shikamoo mapenz[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Hii thread nimecheka sana hadi nashindwa nimquote nani maana nyote mmetishaaa.
BTW zamani hiyo mnazungumzia ipi? Mimi mwaka 2009 nikiwa form 3 ndio nilianza kuandika haya mavitu.
Lazima niende stationery nikanunue zile karatasi za mauwa,kichwani nimekariri nyimbo zote za kizungu forever and for always,when you kiss me,my love,Soledad n.k
Nakumbuka barua yangu ya kwanza kujibu ombi niliandika wiki nzima,nilipomaliza kuiandika nikapulizia perfume ya Red Rose [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Dah!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Hii thread nimecheka sana hadi nashindwa nimquote nani maana nyote mmetishaaa.
BTW zamani hiyo mnazungumzia ipi? Mimi mwaka 2009 nikiwa form 3 ndio nilianza kuandika haya mavitu.
Lazima niende stationery nikanunue zile karatasi za mauwa,kichwani nimekariri nyimbo zote za kizungu forever and for always,when you kiss me,my love,Soledad n.k
Nakumbuka barua yangu ya kwanza kujibu ombi niliandika wiki nzima,nilipomaliza kuiandika nikapulizia perfume ya Red Rose [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Dah!
Hyo ya mauwa na kadi nilizipata sana aiseeeeeeeJamaa anachora ua la love anaandika mwandiko wa kufa mtu, anadondosha na machozi kwenye barua halafu anaandika ona machozi yamelowanisha barua, pafyum kali hadi maticha wanashtukia, yaani zamani raha sana
AhaaaaaaaaaENZI ZETU
Mpenzi wangu nikupendaye kwa dhati.
Salamu nyingi sana zikufikie huko ulipo. Utakapo kujua khali yangu mie ni bukheri kabisa. Hofu na mashaka ni juu yako ewe mpenzi wangu uliye mbali na upeo wa macho yangu.
Dhumuni la barua yangu ni kutaka kukusabahi na kukushukuru kwa barua yako niliyoipata leo mchana. Ahsante sana kwa barua yenye maneno matamu kweli mpenzi wangu. Ama hakika moyo wangu ulijawa shauku kubwa niliposikia jina langu likiitwa pale assemble wakati barua zikigawiwa. Wajua ni namna gani nakupenda ewe kidani cha moyo wangu, chakula cha ubongo wangu, na tulizo la nafsi yangu.
Umeniambia kuwa shuleni kwenu huwa wanafungua barua wakiona ina mwandiko wa kiume. Safari hii nitamwomba monitress wetu aniandikie juu ya bahasha ili nisikuponze mpenzi wangu ukafukuzwa shule. Najua jinsi baba yako alivyo mkali mithili ya mbogo asije akakuchapa bure kishtobe wangu nikupendaye kiasi cha kukosa usingizi kwa ajili yako hadi naiona taswira yako kwenye bilauri ninywapo maji.
Mwezi ujao shule yetu itakuja shuleni kwenu kwenye debate. Ingawa mimi sijui mambo hayo ya debate nitafanya mchongo na msela wangu kiongozi wa debate aniandike jina ili nami nije. Nimekukumbuka sana. Nakumbuka wakati wa likizo tulivyokuwa tunakaa juu ya jiwe lile pembeni ya mto huku nikivichezea vidole vyako nawe ukiniimbia nyimbo za taratibu. Yaani sauti yako ni tamu utadhani kinanda. Kila siku huwa naisikia sauti yako ikiniimbia kwa mahaba ya dhati.
Nisikuchoshe kwa barua ndefu mpenzi wangu. Ila fahamu kuwa mwenzio juu yako sina hali. Nakupenda hadi nimepitiliza maana yenyewe ya neno kupenda. Daima umo mawazoni mwangu.
Msalimie sana yule rafiki yako uliyekuwa naye siku ile. Kuna rafiki yangu anampenda sana. Nitakuja naye kwenye debate.
Ndimi nikupendaye daima,
Mahabuba wako.
HD Wako peke yako
UJUMBE:
If you love three, you are not free,
If you love two, you are not true,
Love only one, that one is ME.
DEDICATION:
(1) Always Be My Baby - by Mariah Carey
(2) I Swear - by All 4 One.
#Zamani_raha_sana[emoji23][emoji23][emoji23]
Ndio nilijua ke, maana hilo jina limekaa ki utam..Ulijua ni KE.!??
Ndio nilijua ke, maana hilo jina limekaa ki utam..
Daaaaaa ilikuwa raha sana, unasubiri wiki mbili kupata mrejesho wa baruaENZI ZETU

Umenikumbusha mbali sana! nikinywa maji nakuona haaaaaaa!Hahahahhahaha, hatari sana..!! Nilikua na Counter book quire 3 nilikua nimeijaza mistari ya haja, lyrics za nyimbo..Nilikua nalitunza kuliko kitu choochote..!!
Lilinisaidia sana kuwa na mistari ya kuwang'oa warembo..!!