EPA na mambo yake

EPA na mambo yake

Wanabodi,

Kuna baadhi yetu humu wanachukulia kupelekwa mahakamani kama ni kitu kidogo. Naomba niwaambie mtu kama Jeetu Patel kukaa kwenye hilo bench la kizimbani kisutu kama maji mtungini akisikiliza mashitaka dhidi yake sio kitu kidogo.

Jana hawa wamenyimwa dhamana hivyo wamelala either Keko, Segerea au Ukonga...hili sio jambo dogo kwa mamilionea hawa. Hapo walipo hata kama wana watu wanawakingia kifua kichinichini lakini hawapati usingizi hawa mpaka pale Hakimu atakaposema nimewaachia huru.

Kesi Mahakamani hata kama ni ndogo inasumbua kichwa na kuthoofisha mwili. Tuombe Mungu hawa washitakiwa wote wawe na afya njema mpaka siku ya hukumu sababu sitoshangaa baadhi wakianza kusumbuliwa na magonjwa ya kisukari au shinikizo la damu.

Tuwe na subira; tujue mashitaka na tufuatilie ushahidi dhidi yao.
 
Utafutaji wa MAISHA na hasa fedha katika FAMILIA nyingi hapa Tanzania unafanana sana. Familia ya matapeli wote wanakuwa hivyo; sasa hivi familia za wanasiasa wote wanajitahidi kuwa wanasiasa!

Halafu ndiyo hao hao ni very positively vetted na usalama wa taifa. Uozo hung'ang'aniana na uozo wenzie.
 
Mbona sioni washirika wao wa Benki Kuu wakipelekwa mahakamani? AU kuna awamu ingine inakuja?
 
Utafutaji wa MAISHA na hasa fedha katika FAMILIA nyingi hapa Tanzania unafanana sana. Familia ya matapeli wote wanakuwa hivyo; sasa hivi familia za wanasiasa wote wanajitahidi kuwa wanasiasa!

Hahaha Mkuu WildCard mbona mimi mwalimu hakuna mwingine ukoo mzima? Lakini kama ulivyosema kama ingekuwa ni fani ya hela (tena za haraka haraka) ukoo na kabila lote litatazama huko...ila umeweka point makini sana
 
Mkuu Yebo..., hapo umesema ukweli wa mambo!! Unajua kwa wale majamaa kitendo cha kuitwa "MSHITAKIWA" kwa kweli ni hatua kubwa sana kwa nchi yetu ya Tanzania ambapo kukamatwa kwa mtu mkubwa (leave alone a well known fisadi) ni kama ndoto..... Tena kikubwa zaidi kujua kwamba wamelala lupango, aisee hata raha napata kumoyo manake ni ushindi ingawa inaonekana ni mdogo lakini wakuu "haba na haba jamani, kibaba kitajaa" very soon!!

Hivi mnakumbuka kwenye zile fomu za kuomba kazi zaidi kwenye mashirika makubwa kuna ka kipengele kanauliza "umewahi kuwa arrested on any charges apart from normal traffic offenses?"........... Well jamaa tayari wamekuwa arested na kuwekwa lupango "rumande" japo overnight so tayari hawatakuwa "their own selves" for as long as they live and records are kept safe!!

Kazi ndio imeanza ngoja tuzidi kungojea matokeo manake kama ni mpiri nadhani ndio dakika ya 5 tu wakuu!!!
 
Any reason why jamaa wanapelekwa kwa mafungu?ili mambo yawe endelevu?tusahau operesheni sangara?tusahau nini?wakuu mnaweza kulidadavua hili?
 
kuna tetesi kuwa mahakimu wote leo wameketishwa chini na wakuu wao juu za hili sakata, vi inzi vya hapo vijitume watupatie hiyo nyeti.

Inavyoelekea Mihimili miwili ya utawala imeamua kujivua lawama kwa kuwa wakali kama pilipili suala hili la EPA.

Bunge limekuwa kali mno kuhusiana na EPA na mhimili wa pili ambao ni Serikali nao hatimaye umeamuka na wamekuwa wakali.Sasa wamewasukumia mhimili wa tatu ambao ni mahakama.

Wananchi wakali kwa suala hili tunasubiri tuone kama hao majaji majoho yao wanayoyavaa yana thamani ile ya juu wanayotuambia au ni mitumba ambayo huivaa kujificha wakiwa wamejaa hofu kuwaogopa wanaowahukumu.

Na tunasubiri kuona hizo judgements zao kama zinaweza kuingia kwenye vitabu nukuu vya kesi kimataifa au zitaishia kuzomewa mahakama za kisutu?

Pia tunasubiri kuona kama hizo shule za sheria walizosoma walizielewa au walikariri na kuiba mitihani? Tutataka kujua kama walisoma sheria vyuo vya VETA au walisomea vyuo vikuu baada ya kutoa hukumu zao.

Pia tunasubiri kuona kama huo uhakimu na ujaji waliupata kihalali au walipewa gesti house kwa kuwafurahisha mahawara zao wa kike au kiume.
 
Well said.
This is a challenge to the Judiciary.Is this going to be business as usual....??
 
YES! hii habari kubwa sana...Kwa wanaomfahamu Jeetu nadhani mtakubaliana nami kwamba sasa Kikwete kaamua kufanya mambo!..
Kwanza fedha kisha kusanya, halafu imefuatia mahakama na kesho nasikia kundi jingine linavutwa ndani!.. Jamani sii haya ndio tulikuwa tunayaomba JF toka kitambo!
Wangechukuliwa mahakamani mwanzo tusingepata hata ndululu...Sii haba jamani sii haba hata kidogo.
Mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Mkuu Mkandara,

Kama JK kakusanya pesa zao na kisha kuwatia ndani wote atakuwa amefanya coup moja kubwa mno.

Wacha tuendelee kusubiri kinachoendelea.

Ila kuanza na Jeetu na Lukaza huenda ni taarifa tosha kwamba kumekucha.

JF itapata ushindi kwa hili maana haya mambo yote yalianzia hapa hata kama Sitta
alijifanya eti majungu ya kwenye internet.

Tuendelee kuwafunga kengere ili wapige kelele mpaka JK asikie hata kama alikuwa hataki kusikia.
 
Hivi kweli JK hana jema analolifanya kwa NCHI hii kama Rais wetu?

Grass root movement ya Kikwete-Nahodha 2010 imeanza kuwa excited na ukamataji wa Wahindi kafara watatu.

Kwa sababu Kikwete ameona imeshakuwa "soo" kutumia the Jeetu Patel's, and the Rostam Aziz's na CCM financiers wengine wa Kikwete-Shein 2005, sasa he is reaching directly to the base, the Wildcard's of the world. Kikwete atabadilisha playbook yake. Watch.
 
Huyo mwanamke anaitwa EDA ni mtu wa mambo ya urembo.Kuna mwanamke analalamika kuwa huyo dada ni kibaka mzoefu wa kutupwa kwani alimpora huyo mume Mwakale ambaye wanashistakiwa wote kwa kuiba hela za EPA.Alimpora huyo mume na kumfanya mumewe halafu wakaenda kushirikiana kupora hela za EPA.Sasa wote wako kizimbani.

Wameandika huyu mama naye ni mfanyakazi wa BOT, je ni kweli? Hiyo nyumba balaa tupu, baba na mama wote Matapeli? Huruma kwa watoto!
 
Kama wanao 🙂 wanaweza kuwa waliamua hawana muda wa kuwa na watoto wao ufisadi na utapeli ndiyo priority yao.
 
EPA kortini Kisutu

na Happiness Katabazi

HATIMAYE watuhumiwa 10 wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam chini ya ulinzi mkali wa polisi, kwa tuhuma za wizi huo.

Watuhumiwa hao, walifikishwa mahakamani hapo saa 4:35 asubuhi na kupitishiwa mlango wa nyuma wa mahakama hiyo na kisha kuhifadhiwa kwenye chumba cha waendesha mashitaka kwa ajili ya kuandaliwa mashitaka yao.

Watuhumiwa hao walivuta hisia za wengi na kusababisha wananchi kufurika katika chumba namba moja ambapo kesi mbalimbali za washitakiwa hao zilianza kusomwa saa 7:24, huku, makachero wa polisi wakiwa wametanda kila kona ya mahakama hiyo.

Mshitakiwa wa kwanza kusomewa mashitaka hayo, alikuwa Johnson Mutachukurwa Lukaza na Mwesiga Rutakakyamilwa Lukaza, ambaye hata hivyo mshitakiwa wa pili hakuwepo mahakamani.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Fredrick Mnyanda, mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Euphemia Mingi, alidai kuwa washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano, yakiwemo ya kughushi, wizi na kujipatia ingizo la fedha kwenye akaunti kwa njia ya udanganyifu ambazo ni mali ya BoT.

Wakili Mnyanda alidai kwamba kati ya mwaka 2003 na Desemba saba mwaka 2005, jijini Dar es Salaam, watuhumiwa hao wote kwa pamoja waliiba, sh 6, 300, 402, 224. 64 kwa madai kwamba wao ni wamiliki wa Kampuni ya KERNEL LIMITED ambayo imeteuliwa kukusanya madeni ya Kampuni ya Maruben Corporation ya Japan.

Washitakiwa hawa wanatetewa na wakili wa kujitegemea, Alex Mgongolwa.

Hata hivyo walikana mashitaka yote matano na upande wa mashitaka ulisema dhamana ipo wazi na Hakimu Mingi alitoa dhamana kwa mshitakiwa huyo kwa masharti kwamba kila mshitakiwa, alipe nusu ya fedha anazotuhumiwa kuiba, yaani sh bilioni tatu, wadhamini wawili, ambao watatoa bondi ya sh sh bilioni 150 au kuleta mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia mshitakiwa haruhusiwi kutoka nje ya jiji bila ruhusa ya mahakama na kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani.

Na upande wa mashitaka ulidai kwamba upelelezi umekamilika hivyo wanaiomba mahakama iwapangie tarehe ya siku ya kutaja ambapo Hakimu Mingi aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 18 mwaka huu.

Hata hivyo ilipoitimu saa 12 jioni, mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo alipelekwa rumande hadi leo atakapofikishwa mahakamani hapo tena kwa ajili ya kuja kutimiza masharti hayo.

Katika hatua nyingine watuhumiwa wengine wanne wenye asili ya Kiasia Jayantkumar Chandubhai Patel "Jeetu Patel, Devendra K. Vinodbhai Patel, Amit Nandy na Ketan Chohan ambao wanakabiliwa na kesi nne tofauti, walipandishwa katika kizimba hicho saa 8:20, wakikabiliwa na kesi za jinai.

Katika kesi ya kwanza ya jinai namba 1153, Mwanasheria wa Serikali Winfrida Koroso, alidai mbele ya Hakimu Neema Chusi kwamba mshitakiwa wa kwanza hadi tatu, wanakabiliwa na mashitaka matano ya wizi, kula njama na kughushi hati za makampuni, kujiingia ingizo la fedha kwenye akaunti kinyume cha sheria na kwamba Agosti 26 na Oktoba 27 mwaka 2005 katika jijini la Dar es Salaam, wote kwa pamoja walighushi hati za makampuni ya Navy Cut Tobacco (T) Ltd na Matsushita Electric Trading Company ya Japan kwamba zimewateua kukusanya madeni ya Kampuni ya Navy Cut Tobacco (T) Limited sh 3,323,974,942.30 na kufanikiwa kupata fedha hizo, mali ya Benki Kuu ya Tanzania.

Washitakiwa hao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea, Mpaya Kamala na Martin Matunda.

Upande wa mashitaka walidai kwamba hawana pingamizi na dhamana na hakimu Chusi aliamuru kila mshitakiwa kutoa nusu ya fedha taslimu wanazotuhumiwa kuiba na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya sh bilioni moja na kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika.

Wakati wakihangaikia kupata dhamana, washitakiwa hao walipandishwa tena kizimbani kwa kesi ya pili.

Katika kesi ya pili ya jinai namba 1155 ya mwaka huu, mshitakiwa Devernra Patel, Jakayantkumar Patel, Amit Nandy ambao wanakabiliwa na makosa matano yanafanana na ya kesi ya kwanza.

Mwanasheria wa serikali, Fredrick Manyanda, alidai kuwa katika tarehe tofauti Desemba 2005 jijini Dar es Salaam, walijipatia sh 4,924,494,477.03 kutoka BoT ambapo walighushi na kujifanya wamiliki wa kampuni hewa ya Maltan Mining Ltd na kwamba wameteuliwa kukusanya madeni ya Kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan.

Hata hivyo kwenye kesi hii ya pili, hakimu alisema hawezi kutoa uamuzi wa dhamana kwa sababu ya muda wa kazi, na badala yake, uamuzi huo utatolewa leo.

Aidha, katika kesi ya tatu ya jinai namba 1154 ya mwaka huu inayomkabili Jeetu Patel Devendra Patel na Amit Nandy ambapo wanakabiliwa na mashitaka manane yakiwemo ya kughushi nyaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Ilidaiwa kuwa katika tarehe tofauti, Septemba 2005, washitakiwa walijipatia sh 2,599,944,456.12 na sh 7,962,978,372.48 toka BoT kwa kisingizio kwamba wameteuliwa na kumpuni zaidi ya tatu hewa, kudai madeni ya kampuni ya Marubeni Corporation.

Katika kesi ya nne ya jinai namba 1157 ya mwaka huu, washtakiwa wote wanakabiliwa na makosa matano ya aina hiyo na walighushi hati za makampuni hewa ya C. ITOH & Company Ltd ya Japan na Bina Resorts Ltd yaliyokuwa yanaonyesha Bina Resort Ltd imewapatia jukumu la kukusanya deni sh bilioni 3,924,992,009,25 la C. ITOH Company Ltd, katika Benki Kuu ya Tanzania. Walikana shitaka hilo.

Wakati huo huo, watu watano akiwemo mume na mke walipandisha mahakamani hapo kwa kesi ya jinai ambapo wanakabiliwa na mashitaka 14, likiwemo la kughushi nyaraka mbalimbali ambazo zinaonyesha wao ni watumishi wa kampuni hewa ya Changanyikeni na kufanikiwa kuchukua fedha BoT.

Washtakiwa hao ni Bahati Mahenge, Manase Makale, Davis Kamungu, Godfrey Mosha na mwanamke mmoja Eda Makale ambaye ni mke wa mshitakiwa wa pili, wote wanadaiwa kuiba sh 2,887,267,249.65 ndani ya BoT.

Hata hivyo upande wa serikali upelelezi umekamilika na kwamba dhamana ipo wazi kwa maelezo kwamba kila mmoja wao anapaswa kulipa nusu ya kiasi fedha taslimu ambazo zikijumlisha kwa pamoja zitafikia kiwango hicho cha fedha wanazotuhumiwa kuiba na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho kutwa.

Washitakiwa walishindwa masharti ya dhamana, hivyo ilipofika saa 12:13 jioni walipakizwa kwenye magari mawili aina ya Defender, yenye namba za usajili T220 AMV na T 210 AMV na kupelekwa gereza la Segerea.

Msafara wa watuhumiwa hao, ulikuwa chini ya ulinzi mkali na ukiongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Mkumbo.

Leo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi, anatarajia kuwasilisha mashitaka ya watuhumiwa wengine wa wizi wa fedha za EPA.

Ijuma iliyopita Rais Jakaya Kikwete alimuagiza DPP, Feleshi kuanda mashtaka dhidi ya watuhumiwa ambao wamekaidi agizo lake alilolitoa bungeni Agosti 31 mwaka huu, kwamba ifikapo Oktoba 31 mwaka huu, wawe wamerejesha fedha walizoiba.
 
Jamani wana JF
Hamna mwenye data hawa watu wanamiliki vitu gani? na wapi?
Nimesikia mmjoa aliajiza range rover UK. Tunataka majumba n.k
 
Mkuu,
Unaweza kuwa na interest kujua wana nini ....lakini kuwa na kitu kama range rover is not a big deal!The bottom line ni kuwa wamekupua big money.....
mbona pia inasemekana wamehongea wanawake - kuongeza mistresses na kutelekeza familia.Haya pia unataka uambiwe?
 
Jamani, naomba muongozo...

Inamaanisha hawa ndo papa wenyewe wa EPA au vidagaa?

Isije ikawa imepangwa deal ya kwamba nendeni kortini lakini pesa zenu mtazikuta mkitoka jela hafu tutawaandalia VIP rooms Ukonga ila msimwage mchele kwenye kuku wengi au ndo mwanzo wa kufungua pandora box?

Shadow
 
EPA kortini Kisutu

na Happiness Katabazi

HATIMAYE watuhumiwa 10 wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam chini ya ulinzi mkali wa polisi, kwa tuhuma za wizi huo.

Watuhumiwa hao, walifikishwa mahakamani hapo saa 4:35 asubuhi na kupitishiwa mlango wa nyuma wa mahakama hiyo na kisha kuhifadhiwa kwenye chumba cha waendesha mashitaka kwa ajili ya kuandaliwa mashitaka yao.

Watuhumiwa hao walivuta hisia za wengi na kusababisha wananchi kufurika katika chumba namba moja ambapo kesi mbalimbali za washitakiwa hao zilianza kusomwa saa 7:24, huku, makachero wa polisi wakiwa wametanda kila kona ya mahakama hiyo.

Mshitakiwa wa kwanza kusomewa mashitaka hayo, alikuwa Johnson Mutachukurwa Lukaza na Mwesiga Rutakakyamilwa Lukaza, ambaye hata hivyo mshitakiwa wa pili hakuwepo mahakamani.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Fredrick Mnyanda, mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Euphemia Mingi, alidai kuwa washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano, yakiwemo ya kughushi, wizi na kujipatia ingizo la fedha kwenye akaunti kwa njia ya udanganyifu ambazo ni mali ya BoT.

Wakili Mnyanda alidai kwamba kati ya mwaka 2003 na Desemba saba mwaka 2005, jijini Dar es Salaam, watuhumiwa hao wote kwa pamoja waliiba, sh 6, 300, 402, 224. 64 kwa madai kwamba wao ni wamiliki wa Kampuni ya KERNEL LIMITED ambayo imeteuliwa kukusanya madeni ya Kampuni ya Maruben Corporation ya Japan.

Washitakiwa hawa wanatetewa na wakili wa kujitegemea, Alex Mgongolwa.

Hata hivyo walikana mashitaka yote matano na upande wa mashitaka ulisema dhamana ipo wazi na Hakimu Mingi alitoa dhamana kwa mshitakiwa huyo kwa masharti kwamba kila mshitakiwa, alipe nusu ya fedha anazotuhumiwa kuiba, yaani sh bilioni tatu, wadhamini wawili, ambao watatoa bondi ya sh sh bilioni 150 au kuleta mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia mshitakiwa haruhusiwi kutoka nje ya jiji bila ruhusa ya mahakama na kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani.

Na upande wa mashitaka ulidai kwamba upelelezi umekamilika hivyo wanaiomba mahakama iwapangie tarehe ya siku ya kutaja ambapo Hakimu Mingi aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 18 mwaka huu.

Hata hivyo ilipoitimu saa 12 jioni, mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo alipelekwa rumande hadi leo atakapofikishwa mahakamani hapo tena kwa ajili ya kuja kutimiza masharti hayo.

Katika hatua nyingine watuhumiwa wengine wanne wenye asili ya Kiasia Jayantkumar Chandubhai Patel “Jeetu Patel, Devendra K. Vinodbhai Patel, Amit Nandy na Ketan Chohan ambao wanakabiliwa na kesi nne tofauti, walipandishwa katika kizimba hicho saa 8:20, wakikabiliwa na kesi za jinai.

Katika kesi ya kwanza ya jinai namba 1153, Mwanasheria wa Serikali Winfrida Koroso, alidai mbele ya Hakimu Neema Chusi kwamba mshitakiwa wa kwanza hadi tatu, wanakabiliwa na mashitaka matano ya wizi, kula njama na kughushi hati za makampuni, kujiingia ingizo la fedha kwenye akaunti kinyume cha sheria na kwamba Agosti 26 na Oktoba 27 mwaka 2005 katika jijini la Dar es Salaam, wote kwa pamoja walighushi hati za makampuni ya Navy Cut Tobacco (T) Ltd na Matsushita Electric Trading Company ya Japan kwamba zimewateua kukusanya madeni ya Kampuni ya Navy Cut Tobacco (T) Limited sh 3,323,974,942.30 na kufanikiwa kupata fedha hizo, mali ya Benki Kuu ya Tanzania.

Washitakiwa hao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea, Mpaya Kamala na Martin Matunda.

Upande wa mashitaka walidai kwamba hawana pingamizi na dhamana na hakimu Chusi aliamuru kila mshitakiwa kutoa nusu ya fedha taslimu wanazotuhumiwa kuiba na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya sh bilioni moja na kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika.

Wakati wakihangaikia kupata dhamana, washitakiwa hao walipandishwa tena kizimbani kwa kesi ya pili.

Katika kesi ya pili ya jinai namba 1155 ya mwaka huu, mshitakiwa Devernra Patel, Jakayantkumar Patel, Amit Nandy ambao wanakabiliwa na makosa matano yanafanana na ya kesi ya kwanza.

Mwanasheria wa serikali, Fredrick Manyanda, alidai kuwa katika tarehe tofauti Desemba 2005 jijini Dar es Salaam, walijipatia sh 4,924,494,477.03 kutoka BoT ambapo walighushi na kujifanya wamiliki wa kampuni hewa ya Maltan Mining Ltd na kwamba wameteuliwa kukusanya madeni ya Kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan.

Hata hivyo kwenye kesi hii ya pili, hakimu alisema hawezi kutoa uamuzi wa dhamana kwa sababu ya muda wa kazi, na badala yake, uamuzi huo utatolewa leo.

Aidha, katika kesi ya tatu ya jinai namba 1154 ya mwaka huu inayomkabili Jeetu Patel Devendra Patel na Amit Nandy ambapo wanakabiliwa na mashitaka manane yakiwemo ya kughushi nyaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Ilidaiwa kuwa katika tarehe tofauti, Septemba 2005, washitakiwa walijipatia sh 2,599,944,456.12 na sh 7,962,978,372.48 toka BoT kwa kisingizio kwamba wameteuliwa na kumpuni zaidi ya tatu hewa, kudai madeni ya kampuni ya Marubeni Corporation.

Katika kesi ya nne ya jinai namba 1157 ya mwaka huu, washtakiwa wote wanakabiliwa na makosa matano ya aina hiyo na walighushi hati za makampuni hewa ya C. ITOH & Company Ltd ya Japan na Bina Resorts Ltd yaliyokuwa yanaonyesha Bina Resort Ltd imewapatia jukumu la kukusanya deni sh bilioni 3,924,992,009,25 la C. ITOH Company Ltd, katika Benki Kuu ya Tanzania. Walikana shitaka hilo.

Wakati huo huo, watu watano akiwemo mume na mke walipandisha mahakamani hapo kwa kesi ya jinai ambapo wanakabiliwa na mashitaka 14, likiwemo la kughushi nyaraka mbalimbali ambazo zinaonyesha wao ni watumishi wa kampuni hewa ya Changanyikeni na kufanikiwa kuchukua fedha BoT.

Washtakiwa hao ni Bahati Mahenge, Manase Makale, Davis Kamungu, Godfrey Mosha na mwanamke mmoja Eda Makale ambaye ni mke wa mshitakiwa wa pili, wote wanadaiwa kuiba sh 2,887,267,249.65 ndani ya BoT.

Hata hivyo upande wa serikali upelelezi umekamilika na kwamba dhamana ipo wazi kwa maelezo kwamba kila mmoja wao anapaswa kulipa nusu ya kiasi fedha taslimu ambazo zikijumlisha kwa pamoja zitafikia kiwango hicho cha fedha wanazotuhumiwa kuiba na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho kutwa.

Washitakiwa walishindwa masharti ya dhamana, hivyo ilipofika saa 12:13 jioni walipakizwa kwenye magari mawili aina ya Defender, yenye namba za usajili T220 AMV na T 210 AMV na kupelekwa gereza la Segerea.

Msafara wa watuhumiwa hao, ulikuwa chini ya ulinzi mkali na ukiongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Mkumbo.

Leo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi, anatarajia kuwasilisha mashitaka ya watuhumiwa wengine wa wizi wa fedha za EPA.

Ijuma iliyopita Rais Jakaya Kikwete alimuagiza DPP, Feleshi kuanda mashtaka dhidi ya watuhumiwa ambao wamekaidi agizo lake alilolitoa bungeni Agosti 31 mwaka huu, kwamba ifikapo Oktoba 31 mwaka huu, wawe wamerejesha fedha walizoiba.

Hapa 'machale' yanaanza kunicheza maana nani alithibitisha kwamba walikwenda Segrea? Kwanini hawajapanda yale mabasi ya Magereza na mahabusu wengine ili wawe mashahidi? Waandishi walioko Dar wafuatilie kwa mahabusu wengine kama waliwaona huko, vinginevyo tujue walifika mahali wakapelekwa Kempisk wakalala usingizi mnonooo!!!!!! na iwe ndio mwisho wa part I ya sinema hiyo ya EPA-Kisutu
 
Nashukuru kwa marekebisho.

Baada ya kukwapua hizo hela walifanya nini? wamefungua viwanda wakaajiri? etc...
 
eti JL hana class,wala taste,eti nyumba kapaka rangi pink.whats wrong na JF.mimi na wewe tunajali class na taste sababu every penny counts,we dont even know where the next meal will come from,yeye he is above this,anawaza where he will get the next billion.huyu JL ana streetcred ndio maana ameweza kujipenyeza kwenye hiyo circle,na for your information hao lukaza's hela imewatembelea siku nyingi.LETS hate the game not players please
 
Back
Top Bottom