TANZIA Ephraim R. Mwansasu, Nguli wa Nyimbo za Injili Afariki Dunia

TANZIA Ephraim R. Mwansasu, Nguli wa Nyimbo za Injili Afariki Dunia

Kuna movie flani hivi alikuwa producer jini lilikodisha Teksi majambazi wakaliua likawa linawatokea moja baada ya mwengine kulipiza kisasi
 
Mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili na Askofu wa Hossana Assemblies of God Ephraim R. Mwansasu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Mwasasu alikuwa akiumwa kwa muda mrefu, kwa sasa msiba upo Kimara Mwisho.

Mwansasu atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi alizoziimba kwa mvuto wa aina yake na kutoa ujumbe mzuri kwa kila aliyesikiliza na kuona video za nyimbo hizo zilizopendwa na kupata umaarufu Tanzania na nje ya Tanzania.

Baadhi ya nyimbo za Mwasasu ni:
  1. Siku nikilala mauti.
  2. Nangojea wakati.
  3. Kutesa kwa zamu.
  4. Dunia inapita.
  5. Tukimaliza kazi.
  6. Kiama.
  7. Heri wenye moyo safi.
  8. Tutatesa milele.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe, Pumzika kwa amani nguli wa nyimbo za injili Askofu Ephraim R. Mwansasu.

Chanzo: Chomoza TV

View attachment 1914996

View attachment 1915016
Huyu jamaa ana undugu na Don Nalimison?
 
Nimekua nikisikiliza nyimbo zake.

Nakumbuka nikiwa kwa mjomba wangu mchungaji mwanzoni mwa miaka ya 2000 ilikua ni ngoma zake 24/7.

Apumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom