Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka

Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka

Informer,
Kwa jinsi nchi ilivyo sasa hivi kila kinachosemwa na muhimili wowote kwa Great Thinker wa JamiiForums lazima usome na mazingira..

Jakaya Kikwete alituasa kila "Unachoambiwa changanya Akili yako"

Hivyo mimi pia sakata hili lilivyomalizwa na changanya na akili zangu.
 
Kwani si alikuwa anazipata kutoka kwenye chanzo huko, vipi walio kuwa wanampatia hizo habari au siri wamefanywa nini?

Au wao wamewachwa bila msuko suko wowote ili kesho waendelee kuzitoa kwa wengine?
Kuvujisha siri za serikali yoyote duniani ni sawa na kuisaliti nchi husika.
Afanyae mchezo huo adhabu yake ndogo kabisa ni kukaa jela maisha yake yote,mara nyingi hua ni death sentence tu.

Naiomba serikali isifanye ajizi kwa yoyote yule atakaebanika kuhujumu serikali kwani atakua kahujumu nchi kwa ujumla.

Serikali hupatikana kwa njia ya uchaguzi hivyo afanyae hujuma huathiri ufanisi kwa wananchi walioiweka serikali hiyo na nchi kwa ujumla

In God we Trust
 
Tujifunze kuheshimu sheria

Wanasiasa waliomtumia wamemwacha peke yake

If you really believe that this case has anything to do with legitimate legal procedures then you will believe if the chief perpetrator of this charade tells you your mother is a donkey.
 
You can do nothing with my opinions,you have to take the charge
If you really believe that this case has anything to do with legitimate legal procedures then you will believe if the chief perpetrator of this charade tells you your mother is a donkey.
 
Tujifunze kuheshimu sheria

Wanasiasa waliomtumia wamemwacha peke yake
This is a two way trafic. Mfumo uliojitokeza kwa kasi awamu hii wa kubambikizia raia kesi uachwe na raia waheshimu sheria. Kama raia ana haki, basi hiyo haki iheshimiwe na ionekane kuheshimiwa.
 
Naamini kuwa kuanzia sasa kila Mtanzania ( hasa siye wa Mitandaoni ) ambao huwa tunakuwa na Viherehere kujifanya Kuwatetea Watu ambao Machoni mwetu huonekana ni Wema na wanaonewa lakini kumbe kwa Jicho Kali na Madhubuti la Serikali kupitia Vyombo vyake Imara vya Ulinzi na Usalama huwa wanakuwa sahihi kabisa Kuwakamata.

Kuna Mtanzania Mmoja alipokamatwa mwaka jana kila sehemu Sisi Team Viherehere wa Kutetea tuliwa tukimpazia Sauti kila Siku kuwa aachiwe Huru huku na Yeye Mhusika ambaye wakati anakamatwa alikuwa hana Mindevu mingi wala Nywele Kipilipili kama alivyo sasa alikuwa akionyesha Ujeuri wake wa Kimajivuno ambao pia uliratibiwa vyema tu na Asili ya Kabila lake analotoka.

Binafsi nakumbuka nililazimika hadi Siku moja kwenda Kanisani Kuombewa nikiamini kuwa Kukamatwa Kwake kulikuwa ni Uonevu na hata Yeye pia Mfungwa Huru Midevu na Nywele Kipilipili alituaminisha hivyo hadi wengine tukachuma dhambi za bure Kuichukia Serikali na hadi Kuanza Kuwahisi Watu wengine hasa Waandishi Wenzake wa Habari kuwa ndiyo wamemchoma Mwenzao ( Midevu na Nywele Kipilipili )

Hatimaye huyo Mlengwa ambaye tulimpigania Mitandaoni kwa Viherehere vyetu ametuumbua mno hasa baada ya Mwenyewe kabisa kwa Hiari yake Kukiri kuwa Makosa yote aliyoshtakiwa nayo ameyatenda na Kukubali Kulipa Faini. Na kama haitoshi katika muendelezo wake wa Kutuumbua pia amesifia sana Jeshi la Magereza kwa Kumjali na Kumtunza vyema alipokuwa huko wakati Sisi Team Viherehere wa Utetezi tulikuwa tunasema alikuwa akinyanyasika huko.

Kuanzia leo sitomtetea wala Kumpigia Kelele Mitandaoni Mwanaharakati yoyote yule kama akikamatwa na Serikali kwani nimegundua wengi Wao si tu kwamba huwa ni Wanafiki bali pia huwa ni Matapeli na Majizi vile vile. Na kuanzia sasa nitaanza Kuiamini Serikali hasa kupitia Vyombo vyake husika pale ikiwa inawakamata hawa Wapuuzi baadhi wanaojiita Wanaharakati.

Unajifanya Mwanaharakati wakati kumbe ni Mnafiki na Mwizi mtupu. Na ukome cha Moto ama hakika umekiona!
 
Hivi kuna sheria kama hiyo ..... unakubali kosa halafu unaachiwa. Au ndiyo wale wa Msamaha wa Rais ....!!

Awamu hii tunajifunza mengi ......!!
 
Back
Top Bottom