Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019

Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019

Duh pesa ndefu sana hiii
Voda ana kadiriwa kua na wateja 19M nchi nzima
Endapo wateja 1,000,000 tu wata nunua vocha za jero (500) kwa siku 7 tu ako kapesa kana lipwa kwa M pesa ya kabenda chap

1M × 500 × 7
= 3,500,000,000
 
Mwandishi wa Habari, ERICK KABENDERA ameitaka Kampuni ya Simu ya VODACOM TANZANIA kumlipa USD 1,000,000 MILIONI ndani ya SIKU 14 kwa Kufanikisha kutekwa kwake mwaka 2019.

Amefanya hivyo kupitia kwa WAKILI wake Peter Madeleka.

View attachment 2974231
Kesi hii iko very genuine indeed. Personally, I have a worse similar experience like this with Tigo service provider. Naona wa-Tanzania wengi ambao wanatoa maoni hawajui bayana namna jinsi makampuni ya mitandao ya simu inavyoshirikiana na 'Wadhalimu' ktk kuwafanyia watu mashamhulizi ya kimtandao Kama haya. Kimsingi Hali siyo shwari kabisa kwenye masuala Kama haya.
Hilo shambulizi la kimtandao alilofanyiwa linaitwa 'Denial of Service Attack', Mimi binafsi nilipofanyiwa mashamhulizi ya namna hii nilikuwa nayadhibiti kwa kufanya 'mbinu za kuyaepuka', nilifanikiwa kufanya hivyo baada ya kupata ushauri wa kitaalamu ktk masuala haya ya ICT kutoka kwa Mhindi mmoja ambaye alikuwa expert sana kwenye masuala haya, ubarikiwe Sana Bw. Murkhejee huko India uliko hivi Sasa.
 
Mwandishi wa Habari, ERICK KABENDERA ameitaka Kampuni ya Simu ya VODACOM TANZANIA kumlipa USD 1,000,000 MILIONI ndani ya SIKU 14 kwa Kufanikisha kutekwa kwake mwaka 2019.

Amefanya hivyo kupitia kwa WAKILI wake Peter Madeleka.

View attachment 2974231
Mkuu Kabendera nadhani namba yangu ya simu bado unayo , nicheki , niko tayari kusaidia huo mchakato bure kabisa , tukishughulikia hawa hata hao wengine watakataa kutumika
 
Katika kesi ya tuhuma za Mbowe ni Gaid Shahid kutoka kampuni ya simu ya Tigo ambaye pia ni mwanasheria wa kampuni hiyo akihojiwa na Wakili msomi Mh Peter Kibatala alitamka waziwazi kwamba suala la kulinda Usalama wa mteja anayetumia lakini ya Tigo wao haliwahusu.
 
Unajua jambo kubwa wanalikosea watu ni aina ya mawakili wanaotumia Peter Madeleke akishatumiwa jambo linabadilishwa kuwa la Kisiasa na uhuru wa mahakama hakuna siasa ndio inaendesha kila kitu, yule mama Singida kaibiwa ushahidi upo watuhumiwa wamekamatwa Babati ila hakuna kilichofanyika hadi sasa wakili wake ni Peter Madeleke jifunzeni kusoma upepo.
 
Back
Top Bottom