Mtanzania aliyekimbia Nchi yake kutokana na kuzorota kwa usalama wake ,kulikochangiwa na watawala , Ndugu Erick Kabendera , ametoa maoni yake kwenye Tume ya haki jinai na kufumua mazito sana .
Kabenderavamefichua mbele ya Tume hiyo kwamba , kumbe siku zote Mahakimu huwaogopa waendesha mashitaka kiasi cha kudhulumu haki za Watuhumiwa , yaani hata kama mtuhumiwa ni dhahiri anaonewa hata akiwa Mahakamani , Mh Hakimu hawezi kumsaidia kwa vile anawaogopa waendesha mashitaka , bali hakusema sababu hasa za Mahakimu kuwatetemekea waendesha mashitaka hao .
Pamoja na hilo Kabendera anasema kwa miezi 7 aliyolundikwa gerezani hakuona mahali popote ambapo panaelekeza mtuhumiwa kutoa maoni yake kuhusu utendaji wa Jeshi la Polisi .
Amependekeza kiundwe chombo Maalum cha kupokea malalamiko ya wananchi juu ya utendaji wa Jeshi la Polisi , kumbukeni kwamba hakuna mahali popote ambapo unaweza kupeleka malalamiko ya Utendaji wa Jeshi la polisi bila koneksheni ya viongozi wa ccm .
Mwisho Kabendera ameahidi kurejea Tanzania pale atakapohakikisha kweli kwamba Usalama wake utalindwa .
Chanzo : Azam Media