Nimekwambia wewe shida ni elimu ndogo. DPP anaweza kuondoa kesi kama akiona ushahidi alionao hautoshi, kisha akakurudisha mahakamani hapo hapo kwa kesi hiyo hiyo na ushahidi mpya.
Ama akaiondoa mahakamani kwa sababu zake tu binafsi hata kama ushahidi upo wa kutosha. Hii haimzuii akijisikia tena kukurudisha mahakamani kwa mashtaka hayo hayo.
Ama akaiondoa mahakamani kwa kukuonya usirudie hilo kosa kama mashehe wa uamsho. Kwamba ukirudia kufanya makosa kama hayo ama yanayofanana na hayo atakurusisha mahakamani, hii inaitwa Nolle Prosequi.
Jitahidi kujielimisha zaidi ili uwe na uwezo wa kujadiliana ukiwa na uelewa wa kutosha.