Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete

Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Screenshot_20221013-182630.png

Legacy inazidi kuzamishwa chini zaidi. Mwendazake alikuwa wa hovyo sana

====
Aliyoandika Kabendera

Wale mliouza mali zenu kupata pesa za kuhonga kusaidia plea bargain zenu zikubaliwe mjitokeze kutoa ushahidi. Wafanyabiashara mliopelekwa ofisi maarufu ya serikali, mkatishwa kwa mitutu ya bunduki wakati Mwendazake akiangalia kupitia CCTV, mkalazimishwa kutoa pesa mjitokeze.

Kuna mfanyabiashara maarufu alipitia mateso makali kwa kipindi cha miaka minne, ikiwemo kubinywa korodani, akilazimishwa aseme uongo kuwa alitoa dola milioni 100 kwa Rais Kikwete. Mwendazake alitaka kutumia ushahidi huo kumkamata Kikwete. Ni lazima atendewe haki.

Tuhuma dhidi ya Mwendazake kuanzisha na kuendesha genge la kihalifu nje ya mfumo wa serikali na kutoa maelekezo kwa genge hili kuwaua viongozi wa vyama vya upinzani, CCM na viongozi wakuu wastaafu ambao wangekuwa kikwazo kwake kutawala milele zichunguzwe pia.

Si mara ya kwanza zoezi kama hili kufanyika; Rais Mwinyi aliunda tume ya kupitia upya kesi zote ya uhujumu uchumi alizoziendesha Sokoine baada ya kuingia madarakani na kuna watu walirudishiwa mali zao.

Binafsi nimeombwa kuwasilisha maelezo ya maandishi kwa mamlaka husika kuhusu vitisho alivyovitoa Ndugu Biswalo dhidi yangu mara kwa mara baada kuachiwa huru na nimefanya hivyo.
 
Duh!

Ndio maana alisema kuna wastaafu wanawashwawashwa.

Huyu Bwana alikuwa ni mtu hatari sana!

Ukiangalia ile picha aliyokuwa amepiga magoti akiomba kura kwenye kampeni za 2020, unaweza hata kumuonea huruma na ukapata picha kuwa ni mtu mpole na humble, kumbe ni kinyume chake kabisa!

Niliwahi sema humu na leo narudia: Mwendazake alikuwa na kipaji kikubwa sana cha uigizaji, sema tu hakuingia kwenye hiyo sanaa ange-fit zaidi huko.
 
View attachment 2386088
Legacy inazidi kuzamishwa chini zaidi. Mwendazake alikuwa wa hovyo sana
Yaani mtu mwitu wa Chato ndanindani afanikiwe kumkamata mtoto wa mjini@?? Tena mafia,kitambo sana katika hizi kazi..Mawazo ya mwendazake sasa yalifikia hatua ya mwisho kabisa ya kuwa mawazo mfu,angalau angesikiliza washauri bais dah!!
 
Unamtetea?
Namaanisha, yeye,saa10 ,katelephone na huyu makamu mpaka piko ni kitu kimoja, sioni sababu mtu kusema zama zile zilikuwa za giza wakati hadi sasa kero tu

Tena bora wakati wa jiwe hakukuwa na tozo na tulitumia mbs kwa raha, hawa wa sasa ni hovyo tu ,hivo basi ,hoja yangu ni kwamba tutafute namna ya kuitoa CCM
 
Mnyonge hutaki kulipa kodi ila Unataka serikali ikulipie ada wanao?
 
Back
Top Bottom