Ester Bulaya: Mkandarasi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere anataka kushtaki alipwe nyongeza wakati mradi haujakamilika

Ester Bulaya: Mkandarasi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere anataka kushtaki alipwe nyongeza wakati mradi haujakamilika

Tuendelee kuwa wapole huku hela za Umma zinapigwa.

Hapo unakuta kuna watu ndani ya Serikali wamemwambia Mkandarasi kashitaki utalipwa labda Bilioni 30, kwenye hizo 30 zetu 15.

Baada ya muda mnasika sijui fulani ameagiza mabasi mapya 200 kumbe ni hela zetu, na ukisema unaambiwa una wivu

Poor Tanzania 🙆
 

Mbunge Ester Bulaya amesema “Mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere unaeleza mkandarasi akichelewa kukamilisha mradi anatakiwa kutozwa tozo, mradi ulitakiw akukamilika 2022 na taarifa zilizopi hautakamilika mwaka huu.

Amesema hayo Bungeni na kuhoji kwanini TANESCO hawajamtoza tozo Tsh. Bilioni 329 wakati Serikali ikichelewa kumlipa Mkandarasi inatozwa Tozo.

Aidha, amesema Mkandarasi alitakiwa kujenga miradi kwa ajili ya huduma za kijamii ya zaidi ya Tsh. Bilioni 200 lakini huduma hizo hazionekani, pia inadaiwa anajiandaa kufungua kesi Mahakamani dhidi ya Serikali akidai nyongeza.


Wameshaona bibi yetu ni tepe tepe ukigusa tu unalipwa
 
Inasikitisha sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Acha alipwe tu ,mbona yeye Bulaya analipwa pesa wakati siyo mbunge!
Uelewe hoja mkuu kwanza ndo ujibu , na sio kuanzisha hoja nyingine ambayo Haina uhasiano,
Unajua wakilipwa hizo fedha NJ za nani ?
 
Tuliwambia mwendazake majanga oneni mabomu yanavyo lipuka. Yy kakufa zake uko
 
Back
Top Bottom