Ester Matiko: Kama Chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

Ester Matiko: Kama Chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

Bila siasa watakufa njaa.
Mimi naona yaliyopita yashapita na hayawezekani kuyarekebisha. Maana cdm kukaa miaka 5 bila kusikika inaweza poteza umaarufu. Muhimu wapeleke viti maalumu majembe ili wakaendelee kuuwasha Moto bungeni.
 
We dada ule udhalilishaji uliofanyiwa na wale Mapolice umeukubali kwa kukisaliti chama kwa kulipwa ujira huu? Kweli dunia ina mambo!!

Action - reaction. Siamini Mtii wa sheria angeumizwa tu.
 
Matiko Yuko vizuri yeye kaambiwa kateuliwa na mamlaka husika inatosha mamlaka husika ni Mweyekiti wa Chama na NEC katibu mkuu kazi yake kuandika Minute tu za vikao vikivyoitishwa na mwenyekiti akijisikia kuitisha

Si kila kitu katibu lazima ashirikishwe
 
We dada ule udhalilishaji uliofanyiwa na wale Mapolice umeukubali kwa kukisaliti chama kwa kulipwa ujira huu? Kweli dunia ina mambo!!
Hivi mnadhani wanasiasa wana-survive kwa kula hewa?
 
Wasaliti ni ninyi wananchi....Hahahahaaa

Sasa mlitaka wafanyaje? Ninyi mnasema kura ziliibwa... Wakawaita mwende barabarani mkaandamane hamkuwaunga mkono... Mnataka nini sasa???

Eti oooo wasaliti??? Wasaliti ni nyinyiiii....
 
Kumbukeni hao mabinti bado wadogo, hawajui biashara, wakikaa mtaani watafanya nini?
 
Kwa maoni yangu, wananchi tunahitaji watu wa kutusemea Bungeni hata kama ni wachache. Wale wengi wapo upande wa serikali hivyo hawatakuwa upande wetu sana; hawa 20 ni bora waachwe tuu kwani wachache hupewa nafasi kubwa ya kusikilizwa naamini tutawakilishwa vyema.

Hayo mengine yaliyotokea kwa kuwa wanasiasa wengi huubiri suala la KUJIAJIRI ni vizuri NAO wakajiajiri hii miaka mitano.
Sio maoni yako. Kazi ya mbunge ni kuwasemea na kuwasilisha kero za wananchi, awe CCM au Upinzani. Kwa hiyo hakuna huyu ni wa wananchi na huyu si wa wananchi tofauti ni uwasilishaji tu. Wengine wanaongea uhalisia, wambeya na wako wakuongeza chumvi.
 
Sio maoni yako. Kazi ya mbunge ni kuwasemea na kuwasilisha kero za wananchi, awe CCM au Upinzani. Kwa hiyo hakuna huyu ni wa wananchi na huyu si wa wananchi tofauti ni uwasilishaji tu. Wengine wanaongea uhalisia, wambeya na wako wakuongeza chumvi.
Sheria kandamizi zinapitaje Bungeni na tuna wa kutusemea?
 
Sheria kandamizi zinapitaje Bungeni na tuna wa kutusemea?
Hakuna sheria kandamizi, sheria inatungwa kudhibiti uharifu. Una uhuru wa kutoa mawazo sio uhuru wa kutukana na kutoa uongo kuzua taharuki. Una uhuru wa kutoa taarifa zilizohakikiwa sio za kuzua. WAJIBIKA hakuna atakaye kugusa.
 
Wewe si ndo yule dada uliyedhalilishwa kwa kupigwa fingers na Policcm wa Tarime baada ya hao jamaa kuvamia mkutano wako? Leo umejiunga na hiyo dola iliyopelekea upigwe finger?

Ningejua kwamba wewe nawe ni mpuuzi kiasi hiki, nami ningesogea nikazamisha. Najilaumu kwa kukosa fursa hiyo.
Siku Shangazi nae akija kuunga juhudi napo pia utajolaumu kukosa fursa maana nae si alifanyiwa hivyo hivyo na polisi.
 
Nimewalaumu sana hawa kina dada waheshimiwa, baadae nikajaribu kujiweka kwenye nafasi zao nikaona huenda hata mimi ningechukua maamuzi kama yao.

Guys, hebu fikiria ulikuwa kila mwezi kuna mzigo unaingia kwenye account yako alafu gafla zinakata na hauna plan B. Kukaa bila kazi kwa miaka hii sio mchezo. Alafu gafla inakuja ofa ya kuingia kwenye orodha ya wafaidi keki ya taifa, na wanaokupa hiyo ofa wana nguvu, mamlaka na uwezo wa kukulinda unapokula ugali wako. Nafikiri tukiangalia kwa angle hii hatutoendelea kuwalaumu hawa kina dada.

Hebu angalia wenzao waliopita njia hizo; Silinde, Slaa, Mollel, Waitara etc alafu wao wakatae ofa hiyo eti wafe njaa kisa waonekane mashujaa? Tuwe wakweli kizazi hiki hakipo tena kwa sasa.
Ujue watu wa humu Jf wanashanaza sana,wao hawajulikani humu maisha yao yakoje usikute nao wanakula keki ya taifa kwa namna yao ila wakija humu ndio wanawaambia wenzao wanajali matumbo sijui ni wasaliti,wakati wao ukiwaambia waingia road wafanye maandamano hawatoki wamejificha tu mitandaoni wao zao kuongea tu.
 
Hii mechi kacheza Mbowe na Mnyika ata Lissu hii chenga amebaki kajishika kiuna
Lissu mwenyewe baada ya maji kumfika shingoni alisema anataka maridhiano na serikali, kwa taarifa yenu hayo ndo maridhiano. Hii ishu ya kukubali kupeleka viti maalum bungeni ni kwamba wameshirikiana wote mbowe, lissu na mnyika, sema wanataka waipotezee kwa wananchi ili wasiaibike, ndo kina mnyika wanajifanya hawajui wala hawana taarifa kuhusu hilo. Wanasiasa wahuni sana, wanaweza kuwasababishia watu wakapigana vita mwisho wa siku wanakutana kwa pamoja meza ya bata na kugonga cheears. Sema nini?, watanzania wajanja wanajitambua walikataa kuingizwa kwenye maandamano kwasababu walisha tambua hilo zamani. Cha msingi serikali iliyopo ipambanie maendeleo kwa kila raia na nchi kiujumla.
 
Njaa mbaya sana..
Kwa maoni yangu, wananchi tunahitaji watu wa kutusemea Bungeni hata kama ni wachache. Wale wengi wapo upande wa serikali hivyo hawatakuwa upande wetu sana; hawa 20 ni bora waachwe tuu kwani wachache hupewa nafasi kubwa ya kusikilizwa naamini tutawakilishwa vyema.

Hayo mengine yaliyotokea kwa kuwa wanasiasa wengi huubiri suala la KUJIAJIRI ni vizuri NAO wakajiajiri hii miaka mitano.
 
Huu ni udhalilishaji wa wanawake.. kwamba wanawake hawana misimamo
Baada ya jana wabunge wa viti maalum kuapishwa, waandishi wa habari walifanikiwa kufanya mahojiano madogo na mbunge mmojawapo, Ester Matiko huku wengine wakigoma. Yafuatayo ni maswali kutoka kwa waandishi na majibu kutoka kwa Ester Matiko.

MWANDISHI: Mmepata baraka za chama?

MATIKO: Nadhani wote tunajua taratibu za viti maalum mpaka kuweza kufika wabunge kuteuliwa, kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia wings mbalimbali na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya Taifa ya uchaguzi, binafsi nilitaarifiwa nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa.

MWANDISHI: Ulitaarifiwa na katibu?

MATIKO: Na mamlaka husika

MWANDISHI: Lakini katibu wa chama anasema hana taarifa na hilo na watachukua hatua kali dhidi yenu, hili unalizungumziaje?

MATIKO: Sijui zaidi ya hapo, kwa uchache wetu ambao tumekuja hapa, nipende tu kuwaambia watanzania, wategemee makubwa kwetu pamoja na kwamba tuko 19. Tunajua yote yaliyojiri kwenye uchaguzi mkuu ulioisha hadi tukapata hiki kidogo katika ushindi wetu mkubwa tuliokuwa nao.

MWANDISHI: Endapo chama kikiwafuta uanachama, mmejiandaa kuchukua hatua?

MATIKO: Tupo hapa kwa sababu ya chama kwa hiyo kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari.

MWANDISHI: Awali msimamo wa chama chenu ilionekana haukubaliani kuweza nyie kushiriki hapa

MATIKO: Nadhani leo jukumu kubwa ni kuapa na tumetimiza hilo, yanayojiri mengine yote yanawezwa kuzungumzwa kwa wakati muafaka. Katika neno letu la shukrani tumesema dhahiri kabisa tunakishkuru chama cha demokrasia na maendeleo kututeua sisi watu 19 kukiwakilisha katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuweza kuwasemea watanzania na chama chetu sasa mengine kama yalijiri yakaenda yakarudi, yatazungumzwa kwa wakati muafaka. Asante.

MWANDISHI: Ndio kusema mmesalimu amri

MATIKO: Sio msemaji wa chama, mimi ni mbunge mteule, ASANTENI SANA.


 
Back
Top Bottom